MH Rais: Hakuna kuchoka Una Maono.

Sinamboga

Member
Joined
Dec 6, 2012
Posts
86
Reaction score
38
Sio jambo rahisi lakini kwakua tupo duniani penye kila aina ya binadamu usikate tamaa. Watu wema wapo Peponi tu hapa duniani kuna kila aina ya binadamu hivyo vyema kutafuta namna ya kutengemaa nao.
Nakumbuka wakati Fulani Baba wa taifa enzi hizo uwanja wa uhuru alifanya mkutano mkubwa kuwataja wanafiki 7 wapika majungu Tanzania. Kwa wakati huo kiongozi wa nchi kufanya mkutano kuwataja wapika majungu 7 nchini bila shaka ni jambo alilimkwaza sana.
Lakini kwenye mahojiano na BBC na Zuhura Yunus Mzee wetu pendwa Ally Hassan Mwinyi[Ruksa] alisema wakati wa utawala wake kulikua na Mamba na kenge kwamba kenge waliokuwepo walimkwamisha ndoto zake.
Pia wakati Fulani Rais Mstaafu Jakaya kikwete aliwahi kusema pale Udom kumwambia Rais mstaafu Mkapa kwamba kazi ya urais afrika ni Thankless Job kama kumpoza pamoja na mateso yote ya urais aliambulia matusi wakati alivyostaafu.
Nakukumbusha pia maneno uliyoyasema wakati unazindua mtambo wa TCRA kwamba changamoto zilizopo ukizishindwa kutatua basi hazitatatulika kamwe.
Wanasema kama uwezi pigana nao basi utaungana nao endelea kukomaa Tumeshafika
Rai yangu Imarisha wizara yako ikiwezekana tengeneza task force kwenye wizara yako badala ya mpaka ufanye ziara hii task force ipite kwenye mikoa wilaya, kata kero, za wanyonge zipate majibu haraka nchi hii sio maskini ni zaidi ya Brazil kwa kila hali.
Pia Kunywa chai na hawa jamaa kwa maoni yangu mara moja moja Sugu, Pro J, Zamaradi, Geah , Dahuu ,Rebeca Mulesi, Ritha Tarimo James Mwigamba Jukwaa la Fursa KIba&Samatta Millard ayo hawa wamebadilisha maisha ya wengi wemewapa furaha watu wengi tukiwa na watu 500 kama hawa ukiwamotivate as president watatengezeza wengine na pengine tutakua na wananchi wengi wenye furaha na pengine na kupunguza sana miserable people.
Utaona watakuja ndondo Cup,TFF,SIMBA,YANGA na wao wataona inafaa angalau kila mechi yao moja wanamlipia school fees yatima moja ama wamlipia kodi mjane ama mtaji kwa mjasilimali kwa utaratibu hata wa kuchanga mia tano.
We make Beautiful Tanzania.
Nawasilisha
 
Dah we jamaa aisee!

Masaa 4 hakuna mtu ana comment uzi wako. Unadhani ni kwanini?
sio kweli thread zote lazima zijibiwe. wamesoma wangapi Halifuuuu. Kingine Ame ni PM nadhani mtu wa TFF kwanza nimetoa idea nzuri na wataaanza na makonda wa daladala za Dar wale ambao watawapa huduma nzuri wanafunzi basi angalau katika baadhi ya mechi watapigiwa makofi kwa uungwana na kujali watoto wadogo wanafunzi. Imefanya kazi right???
 
Halipendwi hilo unalo zungumzia ila mnatumia nguvu mingi sana kumpendezesha kwa wa tz ,anaemsifia ananufaika nae kwa namna moja ama ingine mara yangu ya mwisho kuipigia kula sisiyenu ni 2015 tuna wasubilieni kwa hamu sana2020
 
Ila kuna thread jamani ukisoma unahisi kuzeeka au kupata kiharusi cha macho😏😏😏😏😏😏😏😏😏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…