Mh. Pinda Awasihi UKAWA!!


Wewe ndo hujaelewa ila sisi wenye chama chetu mbona tunaelewana tu
 
Awasihi kukaa meza moja kuangalia ni namna gani watasuluhishana na kuondoa tofauti zao!!

Naamini sasa Serikali ya CCM imeona umuhimu wa UKAWA bungeni,.


Kwa mujibu wa Tamko la Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM, Kijana shupavu NAPE MWANA WA MNAWIE, Kamati Kuu cya CCM imeazimia kuwa kiongozi yeyote wa CCM asiwabembeleze UKAWA wala kuwaita kwenye mazungumzo ya maridhiano maana CCM inahakika walioko Bungeni watapata Katiba safi ambayo itakubaliwa na wananchi.

Maswali ya Uchokonozi:-
1. Sasa tumwamini nani Nape kwa niaba ya Kamati Kuu ya CCM au Mh. Pinda Waziri Mkuu
2. Je ni uthibitisho kwamba kweli CCM haina Uongozi thabiti maana kila mmoja anakurupuka na kauli yake
3. Je hayo matamko yanayotolewa huria huria kama kuku wa kienyeji wanajua madhara yake?
4. CCM inatambua kwamba wananchi wameshaanza kuwa na wasiwasi juu ya uimara tunaoambiwa wanao?
5. CCM walimwelewa Mh. Amos Wako alipoalikwa Bungeni kuelezea kilichojiri Kenya mara mchakato ulipoingiliwa na vyombo vya dola na serikali ya Kenya?
6. CCM wanatamba kwamba wingi wao usiwe kigezo cha kuhukumiwa kwa maamuzi yao Bungeni, Je wanajua kwamba wamewaamsha wananchi kufanya uamuzi mgumu wa kuwapa fursa vyama vya upinzani ili kuhakikisha uamuzi wa maslahi yao unazingatiwa?
7. CCM imejiandaaje kisaikolojia kama alivyowahi kuambiwa na Mwenyekiti wa CCM kitaifa?
 
wewe ndiyo hukumuelewa mkuu, ccm wanaanza kuhaha,.

ni kweli, wameshikwa pabaya. Ukawa mkiacha msimamo tu, ccm wataanza tena dharau na kuwaburuza. Lazima muhakikishe wanafuata utaratibu na si kuburuza wengine.
Tumechoka sasa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…