Mh pengo anamuhujumu kikwete?

Mh pengo anamuhujumu kikwete?

Status
Not open for further replies.

ugasa

Senior Member
Joined
Oct 21, 2013
Posts
193
Reaction score
52
Msimamo wa kanisa ni serekali 3.
Leo hii Mh Pengo anataka serekali 2.
Hii ni wazi inawezekana Katiba ikakwama kupata theluthi inayotakiwa na kutumika ile ile ya 1977.
Inaamana kwamba kazi yote iliofanywa ni bure

GAZETI LA HABARI LEO

MUUNDO wa serikali tatu uliomo ndani ya Rasimu ya Katiba iliyokabidhiwa kwa Rais Jakaya Kikwete mwanzoni mwa wiki hii, umezua hofu kwa baadhi ya viongozi wa dini nchini, wakisema huenda ukachangia kuvunjika kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliodumu kwa miaka 50 sasa.

Aidha, mawazo ya kutaka serikali tatu yameelezwa yanatokana na watu kutokuwa na upendo wa kutosha na hofu ya Mungu.

Hayo yalisemwa jana na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo wakati wa ufunguzi wa ibada ya misa ya shukrani, iliyoandaliwa na Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA) Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

Alisema wanaolalamika juu ya muungano wa sasa wana yao, kwa kuwa unawazuia kufanya mambo yao wenyewe na kuingia mikataba kwa manufaa yao wenyewe.

“Kutokana na kuona kuwa wenzao ni kuzuizi, wanalalamika kwa kuwa Muungano unawazuia watu kuingia mikataba kama ya OIC (Jumuiya ya Kimataifa ya Kiislamu). Sidhani kama huu ni umoja,” alisema Pengo na kuongeza kuwa, “Hofu yangu kubwa ni kwamba, kuwa na serikali tatu ndio mwisho wa Muungano. Tuombe ili tufikie malengo ya umoja.”

Alisema inapofikia hatua ya watu kuwaona wenzao kama ni mzigo na kutaka kujitenga haipendezi hata machoni pa Mwenyezi Mungu, badala yake wanapaswa kukaa na kuzungumza ili kujenga umoja thabiti, badala ya kufikiria kujitenga.

Hata hivyo alitoa mwito kwa wanasiasa na wananchi wote kuombea upendano na umoja katika vyama vya siasa ili vifikie maamuzi yaliyosahihi ya haki na yenye kujenga taifa.

Alisema ubinafsi ndio unaochochea mifarakano katika vyama; na watu kujitokeza tu kujitangaza uongozi bila chama husika kukubaliana hali inakuwa mbaya zaidi.

“Kamati za chama zikae kwa haki, ziseme zinamteua nani kwa sifa alizonazo kugombea nafasi fulani la hasha mtu mmoja anajitokeza na kuanza kusema anagombea nafasi fulani bila matakwa ya chama matokeo yake yanakuwa mabaya sana,” alisema Pengo.

Katika misa hiyo iliyoongozwa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Titus Mdoe, WAWATA walitoa matoleo kwa wagonjwa walioko Taasisi ya Saratani ya Ocean Road yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni nane.

Askofu Mdoe aliwaasa WAWATA kuwa walezi bora wa familia ili watoto wanaotoka katika familia zao wawe na maadili na hofu ya Mungu. Alisema pia wanatakiwa kuwa kioo cha kutenda mema popote walipo bila kujali ni kazini, nyumbani au barabarani.

“Mama uwe mstari wa mbele kutimiza wajibu wako na kutenda yale ambayo ni haki kwa wote, na haki ya msingi kwa mtoto ni malezi mema. Mkishindwa kuwalea vema watalelewa na ibilisi na atawapa misingi ya kiibilisi, unatakiwa uwe mwakilishi mzuri sana wa Kristo popote ulipo, iwe kazini, mtaani, nyumbani au njiani,” alisema Askofu Mdoe.

Alisema katika kumshukuru Mungu kumaliza mwaka na kuwezesha kuanza mwaka mpya wapambane na changamoto walizozipata mwaka uliopita ili kuimarisha imani na umoja wao na pale walipoharibu wamwombe Mungu awaongoze na kuwatia nguvu.

Labda ungesema Mwenyekiti wa CCM anamhujumu Kikwete...hapo ungeeleweka.

Viongozi wa dini wafanye kazi ya dini na kama wanatoa maoni yawe ni binafsi kama mtz yeyote yasiwe ya kitaasisi

Viongozi wa dini wafanye kazi ya dini na kama wanatoa maoni yawe ni binafsi kama mtz yeyote yasiwe ya kitaasisi

Siamini na sitokaa niamini kuwa Pengo kaongea upuuzi huo bali nadhani mnataka kumlisha maneno yenu CCM

askof pengo amesema wapi? Lini na kwani? Maliza habari, kingine watu wenye heshima kwa jamii sio unaletaleta habar zao kwenye jukwaa la siasa.

Msimamo wa kanisa ni serekali 3.
Leo hii Mh Pengo anataka serekali 2.
Hii ni wazi inawezekana Katiba ikakwama kupata theluthi inayotakiwa na kutumika ile ile ya 1977.
Inaamana kwamba kazi yote iliofanywa ni bure
Acha longolongo hapa.Tupe chanzo cha habari na tupia picha hapa.

Pengo ni mmoja wa watu wanaojitambua,siwezi amini anaweza sema upuuzi wa aina hii

pengo ametamka wapi ili tupate kujua vyema...

muheshimiwa pengo ni mwanasiasa wa chama gani?!

Msimamo wa kanisa ni serekali 3.
Leo hii Mh Pengo anataka serekali 2.
Hii ni wazi inawezekana Katiba ikakwama kupata theluthi inayotakiwa na kutumika ile ile ya 1977.
Inaamana kwamba kazi yote iliofanywa ni bure

Watanzania tunakosea sana kuhusu serikali 3, wala haziwezi kutuweka pamoja zaidi itazidi kutuachanisha mbali. Tulikua hatua nzuri kutoka serikali 2 hadi 1 ndo njia pekee ya kutuleta pamoja. Au itengenezwe serikali ya majimbo na visiwani iwe sehem ya majimbo ya tz, nje ya hapo tuukatae muungano. Tuwaache wazanzibar waende zao maana hakuna wanachotuongezea zaidi ya kutunyonya rasilimali zetu watanganyika. Wanaingia bara watakavyo, wanamiliki ardhi na majengo, wanafanya biashara kwa uhuru zaidi na kupewa nafasi za kazi kwa mgongo wa muungano. Wakati huohuo sisi watanganyika tukiwa hatuna uhuru kama huo kwenye ardhi ya wenzetu, zaidi tukienda zanzibar tunaonekana kama wawekezaji badala ya watanzania.

nasubiri kauli ya BAKWATA..; MSIMAMO WA WAKRISTO NDO HUO,... PERIOD

Pengo ni mmoja wa watu wanaojitambua,siwezi amini anaweza sema upuuzi wa aina hii
tuacheni unafiki kila mtu anajua kuwa hatima ya serikali tatu ni kuvunjika kwa muungano na kila mtu kwenda kivyake.sasa kama ndivyo kwanini tusipite njia ya mkato badala ya kuzunguka mbuyu?.

Pengo yuko sawa kabisa.

mbona kwa warioba kapendekeza serekali 3?

Watanzania tunakosea sana kuhusu serikali 3, wala haziwezi kutuweka pamoja zaidi itazidi kutuachanisha mbali. Tulikua hatua nzuri kutoka serikali 2 hadi 1 ndo njia pekee ya kutuleta pamoja. Au itengenezwe serikali ya majimbo na visiwani iwe sehem ya majimbo ya tz, nje ya hapo tuukatae muungano. Tuwaache wazanzibar waende zao maana hakuna wanachotuongezea zaidi ya kutunyonya rasilimali zetu watanganyika. Wanaingia bara watakavyo, wanamiliki ardhi na majengo, wanafanya biashara kwa uhuru zaidi na kupewa nafasi za kazi kwa mgongo wa muungano. Wakati huohuo sisi watanganyika tukiwa hatuna uhuru kama huo kwenye ardhi ya wenzetu, zaidi tukienda zanzibar tunaonekana kama wawekezaji badala ya watanzania.
ukweli ni kuwa serikali ya Tanganyika ilikua ni serikali ya muungano na ndio ilikua na madaraka ya kidola hadi zanzibar.mengine ni kiinimacho tu.

Ulieanzish thread ni mbumbumbu coz wewe hujui kuwaa hata ccm wenyewe hwataki serikali tatu..any way vijana sikuizi hmusomi mna muda wa kusikilizaa porojo kwenye vilabu vya bia na nyama chomaa

Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom