SUMUYANGE
Member
- Apr 5, 2017
- 31
- 67
Mh. NDALICHAKO RUDI DARASANI UKASOME Policy and Management in Education. ZAIDI YA HAPO TUTAANDAMANA KUKUNG'OA SOON.
Kwanza salaam,
Mh. Waziri wa elimu Joyce Ndalichako umeteleza. Kama nikihoji Ph D yako je nitapotezwa kama Ben Sanane?
Jifunze kuwa kuna tofauti kubwa kati ya Taaluma ya Ualimu na kazi ya ualimu. Zamani mwalimu wa shule za sekondari alipewa cheo cha Afisa Elimu daraja la tatu anapoajiriwa tu, huku mwalimu wa shule za msingi akipewa cheo cha Mwalimu pale anapoajiriwa. Je uliwahi kujiuliza kwanini ni hivyo? Na umewahi kujiuliza kwanini mfumo huo mmeubadili rasmi mwaka Jana 2016 na walimu wote kutumia Mwalimu? Tafakari tena.
Mfumo wa Chuoni mwalimu msingi anasoma kwa kiswahili masomo yote kasoro kiingereza maana anakwenda kufundisha kwa kiswahili, wakati Mwalimu sekondari anasoma kwa kiingereza masomo yote kasoro somo LA kiswahili maana anakwenda kufundisha kwa Kiingereza. Tafakari tena kama uko sahihi kuwapeleka walimu takribani 7000 wa sekondari kufundisha shule za Msingi.
Waziri wangu wa Elimu, Mwalimu Sekondari anaingia akiwa na Shahada au Stashahada au Astashada(Induction course) akiwa ameandaliwa kwa sekondari tu. Mwalimu msingi kwasasa anaingia akiwa na Grade 3A au Stashahada ya kufundishia shule za msingi akiwa ameandaliwa kufundisha msingi tu. Tafakari tena kama uko sahihi unachotaka kufanya.
Mh. Waziri wangu, Saikolojia anayosoma mwalimu wa sekondari ni kwa watoto matured wa sekondari, Saikolojia anayosoma mwalimu wa msingi ni kwa watoto wasio matured wa msingi. Tafakari tena kabula hujapeleka watu shule za msingi kutoka sekondari.
Mtukufu Waziri, nakukumbusha kuwa, kuna walimu karibia 7000 wa shule za msingi waliojiendeleza na kupata Shahada au stashahada na wakatolewa shule za msingi kupelekwa sekondari, hao ndio ulitakiwa uwarudishe shule za msingi kwa kuwa walianzia huko. Sijui kama unakumbuka mkuu labda kama ulikuwa bado hujazaliwa, lakini Mimi Deogratius Kisandu nimezaliwa juzi tu mwaka 1980 pale wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, na nimekuwa mwalimu wa Induction course(Leseni) pale Mwamala sekondari, Nzega, Tabora, na sasa ni Mwalimu hapa jijini Mwanza Mkolani sekondari nikiwa na Shahada ya Elimu Maalum. Pole kwa kazi ngumu bosi wangu.
Wizara yako imekaa trigivyogo kabisa haijui inapaswa kufanya nini na kwa wakati gani? Karibu Mwanza uje ule hata Samaki aina ya sato na sangara, mapanki siku hizi hakunaga. Msalimie Mzee Magufuli pale magogoni, mwambie Nitamtembelea 2020 baada ya Uchaguzi Mkuu wa Urais na Wabunge.
Lakini mbona walimu wanatosha sana shule za misingi, umejaribu kuchunguza mijini wake za vigogo walivyorundikana? Muulize Salma Kikwete na Janeth Magufuli wakwambie jinsi ilivyo nao siwalikuwa walimu shule za misingi. Majibu ni kuwa unapokosolewa kama hivi basi anza kufanyia kazi.
Jioni njema Waziri wangu, nimekusamehe hatufanyi maandamano nimeshakupa mwongozo, ila nirushie hata Laki moja kama kweli unajali maoni yangu, lakini sio rushwa. Kesho takuwa busy nasahisha mitihani Staff room.
Deogratius N Kisandu
Mwalimu Mkolani Sekondari, Mwanza. Tanzania.