Nimemsikiliza Mh. Mwingulu katika hotubayake, alipo mwakilisha Mama Samia kwenye Tamasha la Pasaka na Uzinduzi wa Album za nyimbo za injili.
Pamoja na hutuba yake kuwa ya upole na kuonekana kuitoa Kwa utulivu mkubwa, nilishangazwa na makosa mengi katika sentensi zake.
Pamoja na hutuba yake kuwa ya Kufikirisha Sanaa, Kumekuwa na Fikra zisizo Sahihi na zenye kuonyesha mtazamo hatari walionao Viongozi wetu.
Mtazamo kuwa Viongozi watasimamia haki hata Kwa kupambana na Sheria pale ambapo Sheria itatumika kuondoa haki. Mambo yafuatayo ni Muhimu kuzingatiwa.
A:Muundo wa Sheria
1. Nchi yetu inaongozwa Kwa Mujibu wa Sheria, na Utawala wa Sheria. Hii inamaanisha Sheria ndio mtawala Mkuu wa Nchi, na Viongozi na Vyombo Vyote hufuata Sheria na hakuna aliye juu ya Sheria. Hii ina maana pia kwamba Sheria ni zao la mijadala mipana ya Wananchi na ndio muongozo katika namna wanavyo taka kuishi.
2. Pale ambapo kuna hitajika mabadiliko ya Sheria, Serikali ndio yenye nafasi ya haraka na rahisi ya kuibadilisha, Kwa kuleta muswada Bungeni. Pia Serikali ndio inayo toa Miongozo ya Utekelezaji na usimamizi wa Sheria. Na Kwa Wananchi mchakato ni Mgumu Sanaa.
3. Hata hii Mihimili mingine inayo Tunga (Bunge) au Kutafsiri (Mahakama) Sheria, Kwa kiasi kikubwa ina mkono wa Serikali Kwa Bunge kupitia wa Bunge wa Chama ambacho Raisi ni Mwenyekiti wake, na Mahakama ambapo Raisi ana teua Majaji.
B:Haki na Sheria
1. Ni hatari Sana kumpa mtu mmoja nguvu ya kuamua ni ipi haki ya Wanyonge na Kwa jinsi gani itolewe. Hili linaweza kuwa hatari Kwani mtazamo wa mtu hubadilika na mara nyingine hughafilika.Sheria zimeweka utaratibu Mzuri wa kukata rufaa pale hili linapo tokea.
2.Kama haki ikipatikana nje ya Sheria na kutumia Vyombo visivyo hakikiwa, itakuwa hatari Sanaa kwani haki ya mmoja inaweza kuwa dhuluma Kwa mwingine. Pia namna ya Ushahidi inaweza kupoteza muonekano wa haki. Mifumo hii ya Sheria imelijadili hili Kwa mda mrefu na kuweka Miongozo.
Maswali ya Kujiuliza.
1. Je Baada ya kushindwa Kwa baadhi ya kesi mahakamani, ndio haki hii anayo isemea waziri anaye husika na Vyombo vya Ulinzi, Vyombo hivi vimeunda kile kinacho daiwa kikosi cha kuteka na kutesa? Waziri anajaribu kutuambia hili ni sahihi?
2. Je historia inasemanini watu wanapo iona na kuitekeleza "haki" nje ya Sheria? Huu sindo mwanzo wa kinacho itwa Udicteta?
Wito
Niwakati mwafaka wa Mh. Tundulisu kuiongoza TLS, basi tushirikiane nae kutazama fikra hizi zinazo tamani kuondoa Utawala wa Sheria Nchini na kuzitokomeza Kwa nguvu ya hoja.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.