Mh najua una majukumu mengi sana ya kitaifa. Lakini hili linahitaji ufuatiliaji wako ama wa serikali kuwasaidia watanzania maskini. Mh waziri na Naibu katibu mkuu chama tawala, mwigulu kuna clinic ya wakorea pale maeneo ya jangwani Dar es Salaam (Inaitwa KOREA MEDICAL CLINIC) inatibu magonjwa yanayoitwa kleoid yaani uvimbe wa nyama mwilini. Mkorea yule anatoa dawa kwa madai kuwa ugonjwa huo mtu atapona baada ya miezi 6 na anatoa dawa kidogokidogo kwa maana anakupa za siku 2 tu kwanza nakumtaka mgonjwa aende kliniki ya kila siku kwa miezi hiyo 6 na kwa siku lazima ulipe 10,000 (elfu kumi) na pesa yote hiyo haina risiti.
Kilichonikera ni gharama kubwa ya matibabu pasipo mtu huyo yaani mkorea huyo kutoa risiti. Maanake ni kuwa halipi kodi halisi ama halipi kabisa. Naomba serikali isaidie kupata kodi toka kwa mkorea huyo na pia gharama hiyo ni kubwa mno kwa watanzania maana kwa mwezi kliniki pekee unalipa 300,000 na dawa anatoa 30,000 kwa siku 2 na unatakiwa ulipe hivyo kwa miezi 6. Watanzania wangapi wataweza?