Ndugu zangu,
Sina budi kumpongeza Mh. Mwigulu Nchemba kwa uvaaji wake wa magwanda. Natamani Watanzania wote tungebuni sare ya magwanda kama anayovaa Mh. Mwigulu Nchemba kwani inaashiria hali halisi ya nchi yetu na kwamba iwe ni kielelezo kuwa inabidi tufanye kazi kwa bidii ili kufikia malengo yetu hasa ya kuwakomboa watu wenye hali duni ambao wengi wao wanaishi vijijini.
Mimi huwa najiuliza, hivi ujasiri wa kuvaa suti na kufunga tai katika dimbwi la umaskini wa watu wetu tunaupata wapi?
Mh. Mbunge au Waziri au Kiongozi yeyote akivaa suti na tai utamtegemea atashika jembe kumsaidia mkulima katika ziara zake vijijini?
Mh. Mbunge au Waziri au Kiongozi yeyote akivaa suti na tai utamtegemea kushiriki katika kuchimba mashimo ya vyoo kwenye shule zenye upungufu wa matundu ya vyoo?
Mambo mengi katika nchi hii yangeweza kufanyika kwa kuwahamasisha wananchi kujiletea maendeleo yao. Lakini sitegemei hilo kutokea kama viongozi wetu wataendelea "kuvaa suti na tai" ndani la dimbwi la umaskini uliokithiri wa watu wetu.
Inabidi Waheshimiwa Wabunge walielewe hilo na warudi kwenye majimbo yao wavae magwanda na kufanya kazi na wananchi. Ni aibu kuona tangazo la Haki Elimu wanafunzi wa shule fulani wakisukumana kugombea kuingia chooni eti matundu ya choo hayatoshi! Tukiamua "kuvaa magwanda" na kufanya kazi na wananchi tunaweza kumaliza tatizo hilo ndani ya mwezi mmoja.
Yapo mambo mengi ambayo yanaweza kufanyika kwa kuwahamasisha wananchi. Kwa mfano, hali ya usafi kwenye masoko mengi mijini inatisha miaka nenda miaka rudi. Na tunaendelea "kudunda" tu!
Ni lazima Watanzania tubadilike. Ni lazima viongozi wetu wabadilike.