Shida na raha
JF-Expert Member
- Aug 8, 2014
- 3,773
- 3,474
Habari zenu wana MMU rudi kwenye mada hapo juu.
Sikuona shida kumtumia sms ya kwamba simtaki tena maana hana mapenzi ya kweli kwangu.
POINT: Niiko na Msichana wangu yapata miaka miwili sasa niliishi nae kwenye mazingira magumu, nilimsaidia kwa kila hali ilimradi nimridhishe asiwe na matamanio na vitu vya watu.
Punde, akapata safari ya kwenda Dar kwa shangazi yake ambae ni mwalim, maisha yakaanza kumkubali akaanza kupata kamwili kidogo, awali ya yote alikua ananisumbua kila kukicha nimsaidie hiki na kile, ikafika kipindi nikamwambia nataka tuonane mimi na wewe, kwavile mda umekwenda na bado tuko wapenzi, akakubaliana na lile akaniambia nimtumie nauli ili aje, sikua na tabu nikamtumia. Baada ya kumtumia akaanza visingizio eti amekatazwa na shangazi asije ili alinde nyumba.
Nikakubali na hili ikapita mwezi, nikamuuliza "bado hajakuruhusu shangazi yako?" akanijibu bado nikapotezea na ikafika kipindi mambo yangu yakawa mabaya kidogo nikamwelezea anitumie 20, na 10 achukue yeye akashindwa akabaki ananijibu "nikikutumia hii nitakufa maskini" nikaona isiwe tabu na hilo pia nikaachana nalo ikafika kipindi nikamuonea huruma sana nikamtumia kiwango cha pesa(.....) nikamwambia fanya biashara zako, ukipata faida mtaji nirudishie, kweli alifanikiwa na zaidi ila alikataa kunirudishia mtaji hadi leo.
Na hilo pia nimeachana nalo, nikabaki najiuliza huyu ananipenda kweli ama yuko kimaslahi zaidi?Nilipata jibu baada ya kumwambia njoo sasa tukutane akanijibu kwamba hawezi kuacha biashara na kuja kwangu kwanza nimuache, cha kushangaza zaidi hanipigii sim mpaka nimtafute mimi, nikamwambia basi jaribu kuweka voda maana ndo naitumia sana ila nayo akakataa eti watu wake wote wako airtel, ana line mbili za airtel na voda moja kwanini asiweke airtel 1 na voda 1?
Juzi akanipigia simu nikajua leo nimepata bahati ya kupigiwa na yeye lakini wapi, kumbe alikua na yake angalia sasa eti kunipigia kote sim ananiuliza picha zangu mbona kwenye fb sizioni umezifuta, alikua na maana yake kuniuliza hivyo maana akaunti yake na namba za siri niko nazo na nilishawahi kufanya hivyo.Wakati nina kama wiki sijaingia fb na kibaya zaidi nimeshaanza mahusiano na mwanamke mwengine wa kizanzibar na nimeshamwelezea yote haya, jamani mwenye ushauri, pendekezo, msaada wa kimawazo anipe matusi si pahala pake hauna cha kujenga pita kama ushuzi.