BM Pesambili
Senior Member
- Jul 10, 2016
- 102
- 624
Mh Rais mtukufu John Pombe Magufuli, kwanza nikupongeze sana kwa hatua unazochukua kupambana na ufisadi, uzembe, rushwa, ubinafsi, unafiki, udhalimu, matumizi mabaya ya madaraka, wizi wa Mali za umma, ukwepaji kodi, udanganyifu na uongo.
Hali ilikuwa mbaya sana kabla yako, Mahakama zilikuwa zimepotoka, mahakimu waliongwa kwa rushwa na kudanganywa. Viongozi walisukumwa na tamaa ya kujilimbikizia Mali na kupenda anasa, kukosa uaminifu na uadilifu miongoni Mwa wale waliosimamia sheria. Hakuna Mtanzania anayebeza juhudi zako katika mapambano dhidi ya viongozi wazembe na wabadhirifu wa Mali za umma. Umejitoa mhanga kwa niaba ya watanzania wanyonge, nami nasema tuko nyuma yako katika mapambano haya. Enenda pamoja na wenye hekima nawe utakuwa na hekima, lawama ya wazi ni heri kuliko fedhea na ushenzi.
Mh Rais katika hotuba zako nyingi unapenda kutumia msemo huu sana "MSEMA KWELI NI MPENZI WA MUNGU" nami nakubaliana na wewe kuwa msema kweli siku zote ni mpenzi wa Mungu, kwani chimbuko la kweli ni Mungu, ndiye asili na chanzo cha hiyo kweli na popote unapokuta kweli, hiyo ni Mali ya Mungu.
Mh Rais, kama wewe ni muumini wa kusema kweli, Iweje sasa utake kuwaziba wananchi na viongozi wanaowawakilisha wananchi wao wasiseme kweli pale inapobidi? Je wao hawataki kusema kweli wanapoona demokrasia inachezewa au uozo unapoonekana katika serikali yao? Iweje mtu aseme kweli halafu viongozi waubatize na kuuita uchochezi? Niseme kweli viongozi wote wanaokwepa ukweli na kuubatiza jina uchochezi hawatufai hata kidogo.
Mh Rais; kweli na Uhuru ni dhana zinazoenda pamoja, penye kweli pana Uhuru na penye Uhuru pana kweli. Hali moja bila nyingine ni uongo unaosaliti. Uhuru wa kweli haujengeki katika misingi ya dhaifu ya ubinafsi (Umimi) na haulengi kumfanya mtu yeyote yule awe juu ya sheria za nchi na taratibu za uadilifu.
Katika nchi yoyote ukiminya watu kusema au kukosoa serikali yao pale inapobidi, basi Uhuru (Demokrasia) unapoteza msingi wake na mwananchi anakuwa mhanga wa dhuluma, unyonge, ukatili, vurugu, kutawaliwa kwa hila na mabavu. (Hakuna serikali duniani isiyo na mapungufu hivyo kukosoa ni lazima maana haiongozwi na Malaika).
Mh Rais, lazima ujenge uwezo wa kusikiliza hoja na ushauri wa wengine bila kuangalia anayetoa ushauri huo au hoja anatokea Chama gani, kabila gani, dini gani au jinsia gani. Maadamu mawazo hayo au hoja hiyo inatolewa kwa utaratibu unaokubarika bila kuhatarisha amani ya nchi yetu. Lazima watu wako huwasikilize maana nchi hii uwezi kuendesha kwa mawazo yako peke yako tu.
Tofauti ya mawazo ipo popote pale, unapokubali kusifiwa na kupigiwa makofi lakini pia ukubali kukoselewa na kuzomewa. Jenga tabia ya uvumilivu, usikivu, hekima, busara na ungwana. Tegemea kupata upinzani mkubwa zaidi ndani na nje ya chama chako. Na tena unaupinzani mkubwa sana ndani ya chama chako kuliko hawa wanaopiga kelele huko majukwani na kwenye vyombo vya habari. Ndani ya chama chako kuna wanafiki wengi wanaokuchekea mchana alafu usiku wanakubeza, kwani hatua unazochukua unawagusa wao na familia zao.
Mh Rais, namalizia kwa kusema hasira kwa watu wako isiyo takatifu haina haja ya kuimarishwa, Bali kudhibitiwa. Epuka kusema maneno yatakayo wagawa watanzania na kuwachukiza na wala usitamke neno lolote litakalochochea ugomvi ndani ya moyo wa mtu mwingine. Maneno yako siku zote yawe na mvuto kwa watanzania wote, kuliko kusema maneno yenye sumu yatakayowasha hasira ya watanzania. Wape watu wako Uhuru wakusema, kujadili ili kuimarisha taifa letu. Utafanya mengi mazuri lakini bila kuzingatia hili kwa upande wa demokrasia utaonekana ufanyi chochote.
Mh Rais kazi yetu kubwa kama wananchi wako kukuombea sana ili Mungu akuzidishee hekima, busara, ulinzi na afya tele.
Baba wa taifa aliwahi kusema " Ukweli una tabia moja nzuri sana. Haujali mkubwa wala mdogo. Haujali adui wala rafiki, kwake watu wote ni sawa. Pia ukweli unayo tabia ya kulipiza kisasi kama ukipuuzwa. Ukiniona nataka kulipiga teke jiwe kwa kuwa nafikiri kuwa ni digo au mpira natumaini utanionya. Lakini nikilipuuza onyo lako kwa sababu eti wewe ni mdogo au kwa sababu sikupendi, nikalipiga teke, basi litanivunja dole japo ningekuwa nani, ukweli haupendi kupuuzwapuuzwa" Tujisahihishe J.K Nyerere.
Mungu ibariki Afrika
Mungu ibariki Tanzania
Mungu mbariki Rais wetu John Pombe Magufuli.
Boniphace M. Pesambili.