NYARUKURURU
JF-Expert Member
- Aug 22, 2016
- 349
- 199
MWANASHERIA MKUU WA CHADEMA MH,TUNDU LISSU HATARINI KUVULIWA UANACHAMA WA CHADEMA.
Ndugu msomaji wangu muda si mrefu mh,Lissu yatamkuta yaliyowapata akina Zitto Kabwe na Professor Kitila Mkumbo miaka michache iliyopita wakiwa Chadema.
Habari za kuaminika zinaeleza kuwa miongoni mwa mambo yatakayo muweka matatani mh,Lissu ni kwasababu ya ujio wa Edward Lowasa na mh,Fedrick Sumaye ndani ya chama hicho.
Ndugu msomaji kama utakumbuka mh,Lissu kwa muda kadhaa amekuwa akivunja sheria za nchi kwa makusudi na amekuwa akifanya hivi Mara kwa mara ndani ya mwaka huu, baada ya kufanya uchunguzi wa kina na kuhoji watu wake wa karibu yafuatayo yakabainika;
1,Inasemekana mh,Lissu anajiandaa kugombea nafasi ya umwenyekiti ndani ya Chadema mwaka 2019
2,Pia kuna taarifa za kuaminika kuwa Ndugu Lissu ana mkakati wa kugombea Urais wa nchi yetu kupitia Chadema na ndoo maana kwasasa anafanya juu chini kuhakikisha anakuwa maarufu nchi nzima ata ikiwa kwa kuvunja sheria za nchi.
Ndugu wapenzi na wanachama wa Chadema pamoja na watanzania kwa ujumla kama mtakumbuka miongoni mwa vitu vilivyopelekea zitto na mwenzie kufukuzwa ni kujaribu kuweka mikakati ya kugombea nafasi ya mwenyekiti Chadema,sio Zitto tu hata pale marehemu Chacha Wangwe alipojaribu kuonesha nia ya kugombea aliingia kwenye mgogoro mzito na viongozi wa juu wa Chadema, bila shaka na dalili zinavyoonesha Lissu akiendelea na mikakati yake hakika atavuliwa uanachama kabla ya mwaka 2019 kufika.
Wachambuzi wa mambo ya siasa na wasomi wanaamini ujuo wa Lowasa na mh,Fedrick Sumaye unasiri nzito hususani kwenye nafasi ya umwenyekiti ndani ya chama hicho, watu wa karibu wa Mh,Sumaye wanasema kitu kilicho sababisha Sumaye ajiunge na Chadema ni kwasababu mh,Mbowe alimuhaidi kuwa mwenyekiti mwaka 2019.
Wakati huo huo mh,Lowasa naye kwasasa yuko kwenye mkakati mzito wakuhakikisha baada ya Mbowe yeye ndie anakuwa mwenyekiti wa Chadema kwa namna yeyote ile.
Ndugu msomaji wangu utafiti wangu unaonesha kuwa miongoni mwa hawa watu,mtu pekee atakae kuwa mwenyekiti ni Lowasa kwa vile ananguvu ya kifedha kuhonga mh,Mbowe.
Katika utafiti wangu unaonesha muda huo itatokea vurugu kubwa sana ndani ya Chadema zaidi ya hii ya Cuf kwasasa, kwani wabunge wengi wengi wa Chadema watavuliwa madaraka hususani watakao muunga Mkono Lissu na Sumaye.
Wakati huohuo mh,Sumaye na Lissu wamekuwa wakifanya vikao vya kujihami endapo watafukuzwa katika Chama hicho na ndo maana Mh,Godluck Ole Medeye amehama Chadema ili kwenda chama kingine kuandaa mazingira ya wenzie kufikia.
Ndugu msomaji kama utakumbuka mh,Lissu kuhama vyama kwake ni swala la kawaida, mwaka 1989-1994 alikuwa mwanachama wa CCM na mwaka 1995-2004 alikuwa mwana chama wa NCCR na kipindi hiki Lissu alikuwa anaviita vyama vya ccm na Chadema kuwa ni vyama vya kigaidi.
Lakini kama ilivyokawaida ya Lissu kula matapishi yake mwaka 2005 akajiunga na Chadema chama alichokituhumu kuwa chama cha kigaidi na kidikiteta na speech zipo hata ukiitaji utazipata kwahiyo haitashangaza kumuona mh,Lissu baada ya kutimuliwa Chadema kahamia UDP alikoenda kuandaa makazi Ole Medeye, au hata kurejea kwao CCM, au hata kumupigia Magoti Zitto kabwe.
Ndugu wasomaji wangu, hakika siku za Lissu kuwa Chadema zinahesabika kwani amegusa nyeti za wakubwa ndani ya chama hicho za kuandaa mazingira ya umwenyekiti na Urais.
Mwisho nakuomba msomaji wangu uendelee kufuatilia makala zangu nitakujuza mengi zaidi kuhusiana na mgogoro huu ulioanza kujitokeza Chadema.
Imeandaliwa na wenu
MWITA NYARUKURURU
mwitanyarukururu@gmail.com