Mh. Lembeli unakumbuka yaliyompata Dr. Mwakyembe?

Mh. Lembeli unakumbuka yaliyompata Dr. Mwakyembe?

Makamee

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2013
Posts
2,029
Reaction score
1,201
Baada ya sakata la Richmond lililopelekea waziri mkuu Edward Lowasa kujiuzuru,mambo kadhaa yalimuandama Dk. Mwakyembe ambaye alikua mwenyekiti ktk uchunguzi wa kashfa ya Richmond.

1.May 2009 alipata ajali mbaya ya gari mkoani Iringa,Wachunguzi wa mambo walidai ilikua ajali ya kutengenezwa.

2.October 2011 alipata ugonjwa wa ajabu wa kubabuka ngozi ya mwili na kutoa unga, Wachunguzi wa mambo walidai alipewa sumu imuondoe taratibu.

3.Alifanikiwa kuingia ktk baraza la mawaziri,Wachunguzi wa mambo walidai umahiri wake wa kuendesha tume ya richmond ulimsaidia kua waziri ingawa kuna mambo kadhaa mazito aliyoyasema ni vigumu kuyaweka hadharani.

Swali kwake Mh James Lembeli:
1.Kwakua repoti ya kamati yake imeangusha mawaziri wanne,
2.Kwakua amegusa maslahi ya baadhi ya watendaji,

3.Kwakua kuna nafasi za wazi za kupata kuingia ktk baraza la mawaziri.

JE AMEJIPANGAJE?
 
Acha kumtisha wewe... unaleta reference ya mwakyembe hapa unataka kutuaminisha ----- na ile movie ya kwenda kwa waganga sijui assassin ambao mpaka leo imebaki historia... Mwa alikuwa anachukua mzigo wenye ngwengwe akaihamishia hadi ofisini kwake, bahati mbaya hata huo mzigo ulishavuta kamba! Taarifa kusomwa na M/Kiti haina maana taarifa yote ni ya kwake! Taarifa ni ya Kamati nzima...Hata hivyo taarifa yenye ukiisoma kwa undani kama kweli walikuwa na dhamira ya dhaati Taarifa ile ingemsafisha Balozi Kagasheki kwa Juhudi zake za dhati ktk kupambana na Ujangili nchini...
 
Kagasheki kilichomshinda ni kusimamia Operation na kupata taarifa ya nini kinaendelea ktk operatio ile. Kwa stage ile unaanza wapi kumsafisha Kagasheki?
 
Kagasheki kilichomshinda ni kusimamia Operation na kupata taarifa ya nini kinaendelea ktk operatio ile. Kwa stage ile unaanza wapi kumsafisha Kagasheki?
Kama waziri alikuwa anapewa taarifa za mafanikio ya kuwakamata majangili siyo ya kubaka akina mama na watoto! Yeye aliomba msaada wa vyoombo vya ulinzi na usalama; waliompa msaada na kusimamia ile opereeshini ni Waziri wa Ulinzi, Mambo ya Ndani na TISS hapa waliokuwa wanatakiwa kuwajibishwa ni Nahodha, Nchimbi, yule wa TSS na yule wa mifugo aliekaa kimya wafugaji wakiwa wanauawa...
 
Kagasheki kilichomshinda ni kusimamia Operation na kupata taarifa ya nini kinaendelea ktk operatio ile. Kwa stage ile unaanza wapi kumsafisha Kagasheki?

Mkuu Makamee ni vema watu wakatambua tu kwamba kuna wakati mtu anawajibika "VICARIOUS LIABILITY" siyo kwa sababu ametenda kosalile ,hapana bali kwa kosa lililotendwa na mtu aliye chini yake au anaye wajibika kwake.Kwa wenzetu walioendelea utumbo kama huo uliofanyika Waziri Mkuu angewajibika maramoja tena ndiye aliye takiwa kuwa mtu wa kwanza na amebainika bayana akichochea vitendo vya majeshi kujichukulia sheria mkononi , huyu wakwetu anauma uma mdomo eti anahitajai utulivu anasubiri sikuu ipite ndipo atoe kauli hajui kwamba kuna watu wemenyimwa fursa ya kushehekea sikukuu hii na wapendwa wao , kwa ndugu zao kuuwawa kikatili na wengine kutojulikana waliko hadi sasa.

Hakuna namna ya kuwasafisha au kucompromise na watendaji hawa .Kwa sasa kinachotakiwa ni hawa wahusika wote wakiwamo wakuu wa majeshi (Mwamunyange na Mwema ) wakamatwe maramoja na kufikishwa Mahakamani kwa Mauaji na kujeruhi Raia.
 
Hadi lini tutaacha uoga?
Lembeli amethubutu na ameweza anapaswa kupongezwa na sio kuogopeshwa bila kujalisha Anatoka chama gani!!
 
Hadi lini tutaacha uoga?
Lembeli amethubutu na ameweza anapaswa kupongezwa na sio kuogopeshwa bila kujalisha Anatoka chama gani!!

Hata hili la kujiandaa kupata uwaziri ama unaibu ni kumuogopesha?
 
Sikumbuki na sitaki kukumbushwa,mwakyembe aliendekeza njaa akahongwa uwaziri,kama yeye jasiri na mkweli atuambie alilishwa sumu au????
 
Sikumbuki na sitaki kukumbushwa,mwakyembe aliendekeza njaa akahongwa uwaziri,kama yeye jasiri na mkweli atuambie alilishwa sumu au????

Hospitali ya Apollo ya nchini India ilituma serikalini report ya ugonjwa na matibabu ya Dk Mwakyembe labda aliyekua waziri wa afya Haji Mponda anafahamu kuhusu nini kimeandikwa.
 
Hakuna haja yakuogopa maana kila nafsi itaonja mauti.....tulitoka kwa udongo tutarudi tena huko na Roho kurudi ilikotoka uhai wa kila mtu uko mikonomi mwa Mungu.
 
Hadi lini tutaacha uoga?
Lembeli amethubutu na ameweza anapaswa kupongezwa na sio kuogopeshwa bila kujalisha Anatoka chama gani!!
Wanaomfahamu Lembeli... watasema... hoja na maksudi ya report ya team yake ililenga kumtoa Kagasheki. Maana yeye mwenyewe Lembeli ni mtuhumiwa wa ujangili wa kulisha mifugo yake katika hifadhi za wanyamapori. Hajali kitu bali anataka mambo yake yaende tu. Kama alikuwa na na niya ya dhati kwanini report yake haikutaja waliohusika? maana kila aliyehusika na kadhia ile anajulikana na serikali imewalipa DSA za kufanya kazi ile. Akina lembeli wameshindwa nini kuweka wazi wahusika? Ukiangalia kiundani nutaona kabisa ni visasi na waziri wa maliasili ....na Lembeli ameinyemelea ile nafari muda mrefu sana. Sijui Raisi Kikwete kama atampa hiyo nafasi huyu jangiri. yetu macho na masikio. Wanaomfikia Mkulu..wamueleze... Lembeli hafai kupewa uwaziri wowote...ni mnafiki na ......
 
Duh! Nchi ina sarakasi hii hadi basi.
 
Baada ya sakata la Richmond lililopelekea waziri mkuu Edward Lowasa kujiuzuru,mambo kadhaa yalimuandama Dk. Mwakyembe ambaye alikua mwenyekiti ktk uchunguzi wa kashfa ya Richmond.

1.May 2009 alipata ajali mbaya ya gari mkoani Iringa,Wachunguzi wa mambo walidai ilikua ajali ya kutengenezwa.

2.October 2011 alipata ugonjwa wa ajabu wa kubabuka ngozi ya mwili na kutoa unga, Wachunguzi wa mambo walidai alipewa sumu imuondoe taratibu.

3.Alifanikiwa kuingia ktk baraza la mawaziri,Wachunguzi wa mambo walidai umahiri wake wa kuendesha tume ya richmond ulimsaidia kua waziri ingawa kuna mambo kadhaa mazito aliyoyasema ni vigumu kuyaweka hadharani.

Swali kwake Mh James Lembeli:
1.Kwakua repoti ya kamati yake imeangusha mawaziri wanne,
2.Kwakua amegusa maslahi ya baadhi ya watendaji,

3.Kwakua kuna nafasi za wazi za kupata kuingia ktk baraza la mawaziri.

JE AMEJIPANGAJE?

kiongozi sio kuongoza kamati, kiongozi anazaliwa, yy mwenyewe anaweza kupewa uwaziri akafanya vibaya kuliko waliojiuzulu, hivyo inategemea kama ana kipawa cha uongozi
 
Kama kuna jambo linalochangia uduni katika nchi hii ni Ukosefu wa Ujasiri kisa kuogopo Kifo!

Amini ndgu maendeleo yoyote unayoyaona duniani ni kwa kwa kua wapo waliodhubutu na hata KUTOA MAISHA YAO!

Embu kumbuka ni wangapi walitoa roho zao hata uhuru ukapatikana Nchi hii?, Ukiona leo unaruka hewani na ndege wapo waliokufa na hata kuwa vileni hata ikajatokea hivo.

In fact kama Lembeli atauawa kwa ujasiri huu ni HERI SANA KWAKE kuliko angekufa kwa proteini za shetani (ufisadi).

Go Lembeli Go, Maana utake usitake utakufa tu. Kufa basi kifo chenye Heri!
 
kiongozi sio kuongoza kamati, kiongozi anazaliwa, yy mwenyewe anaweza kupewa uwaziri akafanya vibaya kuliko waliojiuzulu, hivyo inategemea kama ana kipawa cha uongozi

Hivi umeelewa kweli ? Topic inahusiana na kuepuka vitu vyenye ncha kali .
 
msiwe na wasiwasi tutamlinda na atakeyemgusa tambalamahimu hata chawa haatabaki kwao! chezea Gambushi nyie?

Ila ni vyema akatumalizia full report ya tokomeza nasikia kuna mengi makubwa hakuyasema.
 
Back
Top Bottom