Mh. January Makamba: Haya ni matusi kwa viongozi wote waliowahi kuiongoza nchi hii

OGTV

JF-Expert Member
May 22, 2016
353
167
Mh. January Makamba,alipochangia hoja kuhusu swala la Muungano wa Tanzania na Zanzibar.
 
Muungano Wa Tanganyika na Zanzibar unafaida gani?
Hauna faida yeyote zaidi ya Tanganyika kutumia pesa nyingi za watanganyika kuulea na kubembeleza muungano, pato la Zanzibar ni Dogo sana pia wamejilundikia Utitiri wa watumishi wa umma, wabunge nk kwa kutegemea pesa za Tanganyika, Pesa inayotoka Hazina kwenda Zanzibar kupitia Wizara ya January makamba nyingi hupigwa na wajanja, mfano kuna bajeti pesa za kumaliza Kero za muungano hiyo pesa inaliwa na wajanja ndiyo maana mpaka leo Kero hazimaliziki.
 
muungano ule wa Nyerere ulikuwa na faida kwanza Zanzibar haikuwa na Watumishi wengi kiasi cha kuilemea Tanganyika kuwalipa mishahara pia Rais wa muungano alikuwa na nguvu kwa Zanzibar tofauti na sasa Rais wa muungano hawezi kukagua gwaride siku ya Uhuru wa Zanzibar japo kwa sasa Zanzibar imekuwa jimbo la Tanganyika inatawaliwa kikoloni mambo leo Gavana kasimikwa na Tanganyika ingawa yupo huru na baraza lake la wakilishi na bunge lake lakini bado anabakia kuwa ni koloni la Tanganyika ambalo ni la gharama kubwa kulilea na kulilisha na kulilinda.
 
Tukiacha ushabiki wa kivyamaa, Makamba ni kichwa ndani ya ccm na tanzania.
Tatizo lake kubwa ni kutaka madaraka
Huo u kichwa wake ni useless, ni wa kufanikiwa mambo hasi tu kwa taifa ambayo ni chanya kwa ccm yake ana tofauti gani na yule mbobezi wa sharia kutoka Havard anaye acha kurekebisha mapungufu ya sharia na kisha kuyatumia hayo mapungufu kutuibia?. Hana tofauti na change.
 
Hivi kwanini tuulinde? Kwan nani atakuja kuuiba au kuuvunja kama kweli uko kwa misingi ya makubaliano ya pande zote mbili?

Hii comment bado ipo tu haijafutwa?? Ngoja niipe muda zaidi

Sent from my BlackBerry 9790 using JamiiForums
 
Kwa maendeleo ya Technologies yaliyopo sasa, inabidi tujitafakari upya hofu tulizokuwa nazo 1964+

Kama mtu ana weza kuset bom akiwa Misri kupiga Kondoa, are we really need to live in fear anymore au tunatakiwa kujipanga upya.
 
Tukiacha ushabiki wa kivyamaa, Makamba ni kichwa ndani ya ccm na tanzania.
Tatizo lake kubwa ni kutaka madaraka
Mkuu hapo umejichanganya, hakuna tatizo kutaka madaraka kwa kuwa bila hayo madaraka utamtambuaje kama ni kichwa? Hakuna mwanasiasa asiyependa madaraka.
 
Tuanzisheni Petition na kuiwakilisha,upigiwe kura na Watanganyika pamoja na Wazanzibar,tuone kama kuna haja ya kuendelea na Muungano.
Both parties are arguing. Kila pande unaona unadhulumiwa. Sasa tutafute suluhu. Kero za Muungano haziishi hizi.
Hiyo pesa iliyotengwa kwa ajili ya kumaliza kero za Muungano zitunzwe siku moja tufanyie kazi ya kupata maoni ya pande zote mbili.

Kama ni uoga,tutakwenda kaburini kwa Mwl Nyerere na kusem kwamba maneno yako ambayo daima ulikuwa ukiyarudia kuwa "wananchi wapo huru kujiamulia juu ya nchi yao", wananchi wameona kuwa hakuna haja ya Muungano.
Mwl atakubaliana na jambo hill litatatuliwa.
 
Makamba ni mdini mkubwa, nakumbuka mwaka jana alivyo kuwa akisambaza mesej za udini, amejaa chuki sana huyu mtu
 
Back
Top Bottom