Mh. Bashe kama Sokoine

Mh. Bashe kama Sokoine

Trump Jr

Member
Joined
Jan 19, 2017
Posts
26
Reaction score
35
Uongozi ni kusema na kutenda, mipango na mikakati ya pamoja.

Huyu anaweka TOZO kwenye kila kitu, huyu anapunguza bei ya mbolea, anatafuta mbole ya ruzuku ambayo mkulima anachangia karibia 50% ya gharama.

Kiongozi lazima awe na hisia za kibinaadamu kwa anao waongoza, kuna muda serikali inabidi itoe huduma tu pasina kuingiza faida hata chembe kwani wakulima wakilima mazao kwa wingi watadhibiti mfumko wa bei ya mazao ya chakula na maisha yatakuwa mepesi.

Ziada ya chakula tutauza nje na serikali itapata kodi yake.

Tulichelewa kupata Waziri wa Kilimo, Mh Bashe anaitendea haki wazira hii japokuwa tupo katika kipindi kigumu, hili lazima tulitambue na site tulione.

Natamani kusikia kauli ya Mh waziri Mkuu ikisema nchi inaingia kwenye kufunga mikanda na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ili kupambana na uchumi unao tuama maana ukiona mbinu pekee ya kuongeza pato la Taifa ni kuweka TOZO kwenye kila kitu, TOZO kwenye kutunza pesa Bank, TOZO kwenye kuihamisha pesa hiyo kwenda kwenye simu, TOZO kwenye kuituma au kuitoa kwa wakala wa Mpesa basi ujue tunapitia kipindi kigumu.

Wizara ya Kilimo ndiyo wizara Mama katika mataifa yote Duniani, pamoja na vita iliyopo Ukraine lakini bado anauza ngano yake Africa na nchi nyingi za Ulaya, hivyo Mh Bashe anaweza kutukomboa kiuchumi kama atakwenda hivi na atapata washauri wazuri.

20220831_122009.jpg
 
Hoja ipo mezani deal nayo, mzalendo ukiona jambo lisemee iwe kwa kupinga au kuunga mkono tunajenga Taifa moja.
 
Back
Top Bottom