Mguu na mkono wa kushoto

Ziroseventytwo

Platinum Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
9,434
Reaction score
17,907
Wandugu! Kuna ukweli wowote kuwa mtu anayetumia mguu na mkono wa kushoto kwenye michezo, wanauwezo kuliko wanaotumia mkono/mguu wa kulia? Baadhi ya wanamichezo,wanaotumia miguu/mikono ya kushoto ni pa1 na Diego Armando Maradona, nguli la Argentina,Leonel Messi,mwanasoka bora wadunia 3 times, Kun Sergio Aguerro, mpachika mabao wa Man city, Arjen Robben winga wa ukweli pale klabuni Munich. Mwone Rafael Nadal,anavyotandika tenis,anapopambana na manguli kama Djonkovic, Andy Murry na hata 16 grand slam winner Roger Federra. Je? Kuna ukweli wowote,kuwa watu wa aina hiyo wanauwezo michezoni? Ni unadhani kinasababisha hawa wawe juu kuliko watu wa miguu/mikono ya kulia?
 
Unataka tuchukue katika tasnia hizo mbili tu(Football na Tenis) halafu tukufanyie uchambuzi makini wa kisayansi ili upate uhakika zaidi kuwa wapi ni zaidi kati ya hayo makundi mawili Mguu/mkono kushoto Vs. Mguu/mkono kulia ? Au tukuweke na tasnia nyingine mzee ili ujue ukweli
 

mkuu,itakuwa vema kama utaweka makundi yote au tasnia nyingine tofauti na football na tenis. Then ukiichambua kisayansi, itakuwa safi. Ila utumi kiswahili, kiingereza, sitakupata sana!
 
mkuu,itakuwa vema kama utaweka makundi yote au tasnia nyingine tofauti na football na tenis. Then ukiichambua kisayansi, itakuwa safi. Ila utumi kiswahili, kiingereza, sitakupata sana!

Nilipost hii some months ago kwenye huu uzi https://www.jamiiforums.com/mahusia...-mpenzi-mpya-anatumia-mkono-wa-kushoto-2.html hope itasadia

 
innawezekana wadau.
sasa mi ni maleft wa mguu na mkono. tatizo ninamwandiko mbaya msiombe. yaani kwenye mitihani ilikuwa ngumu walimu kuelewa nilichoandika japo wengi including walimu wa primary hadi chuo walinikubali kuwa nna uwezo sana.pia hata kazini wengi wanaona hivyo japo mwenyewe najiona wa kawaida sana.
 
hizo fiksi............tukianza kuorodhesha wanaotumia mguu/mkono wa kulia hapa c mtakimbia nyie.......
 

sio peke yako, na mimi nina mwandiko mbaya usiombee aisee kama bata kakatiza.. Gud to know tupo tupo wengi..
 
Kwa kuwa wanaotumia mköno/mguu wa kushoto ni wachache ndio maana tunaona kama wao wamebarikiwa vitu flani zaidi ya wa-kulia. Wao na cc ni walewale tu, hakuna tofauti. Mie natumia kulia na kushoto kuandikia na miandiko yote mizuri, pia enzi zangu nilikuwa nacheza soka kwa kugonga gozi kwa miguu yote lakini ndo ivo tena, nimefulia mbaya.! Sina ujiko wowote
 
Dah! Hapo kwnye mwandiko upo correct coz mie nikiwa chuo kuna prof alikataa kusahihsha pepa zangu kisa mwandiko wa left hand!
 
mi nimewaona sawa hao mashoto kadhaa ambao wako bright, lakini pia nimesoma darasa moja o level na mashoto wa mikono wawili, yaan walikuwa ni vilaza balaaaa, mmoja alifail form two, na mwengine cjui hata aliishia wapi ila mi naona ni kwa vile kwli wapo wachache ndio maana wanaonekana wako bright kiivo, naamin kuna wengi wa kawaida tu
 
mi natumia kushoto kwa kuandika, na kujichamba nkiwa toilet. Sioni cha ajabu.
 
mi natumia kushoto kwa kufua nguo, na kujichamba nkiwa toilet. Sioni cha ajabu.
 
Hahaha..nadhani asilimia kubwa tuna miandiko mibaya..same here,nina mwandiko mbaya mpka inabidi niwe naandika herufi moja moja bila kuunganisha. Kazini wananiita jembe,class ckuwa mhudhuriaji kbc nikienda kwenye pepa jamaa wanashangaa oya umekuja kujibu nn?class huwa huji? Ila yakija matokeo ndo utanisoma.
sio peke yako, na mimi nina mwandiko mbaya usiombee aisee kama bata kakatiza.. Gud to know tupo tupo wengi..
 
Nambe,ukikuta kilaza ni kilaza kweli..ila ukikuta bright ni bright mbaya..
 
Last edited by a moderator:
Mimi natumia kushoto kwa kila kitu! Mwandiko wangu sio mbaya kwa sababu unasomeka! Kuanzia O na A level nilipata division one na udsm nikapata upper second! So wanaotumia kushoto asilimia kubwa ni majembe!
 
Msijali wote mnaotumia kulia nafikiri kama amesha exaust hiyo orodha hapo juu, maana yake ni kwamba watu wote maarufu waliobakia wanatumia kulia, sasa utapima wapi ni wengi zaiadi, kama ni raisi ni moja kwenye kundi lao au wanasayansi wako watano maana yake waliobaki wote ni righties
 

Kuna natural born lefties mkuu na wanaoAdapt kuwa lefties either toka wadogo mkono wa kulia ulikuwa limited labda mobility issues, ulipanda mti ukaanguka ukawekewa hogo kwenye mkono wa kulia ikabidi kujifunza kutumia kushoto wewe sio mashoto ni adaptation tu, ajali umekatika mkono wa kulia. Kamwe huwezi kuwa mashoto kwa kuamua kutumia mashoto hiyo kitu inaanzia kwenye brain hemispheres..
 
Mimi chekechea ilibidi bakora zitumike kunibadili toka mkono wa kushoto kwenda kulia.Kilichotokea sasa ni balaa,nilikuwa na mwandiko kama wa daktari kwenye kadi ya mgonjwa.Ila kadri nilivyozidi kusonga mbele mwandiko umezidi kuboreka na kuhusu darasani from primary school to chuo watu walikuwa wanaona vumbi langu tu mpaka wakawa wananichukia kwasababu nilikuwa adui mkubwa wa prepo time ila matokeo yangu tembo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…