Taarifa nilizonazo kutoka Kojani Kisiwani Pemba ni kuwa watawala wamevichukuwa vyombo vya wananchi ambao wanakataa kuwavuusha wana-CCM na sasa Kojani nzima inatoka kwenda kukomboa vyombo vyao. Tuombe salama na busara itawale.
Kojani ni kisiwa kipo kaskazini mwa Pemba.
==============================
UPDATE
Nimearifiwa kuwa mzozo umemalizika salama usalimini. KMKM na JKU walitaka kuichafua hali kwa kupiga risasi juu lakini wananchi wakagoma kurudi nyuma na badala yake wakaichukuwa boti ya KMKM wakaipandisha juu uwanja wa mpira wakiwaambia kuwa hawaitoi mpaka wapewe vyombo vyao.
Baada ya mazungumzo marefu, wamerejeshewa vyombo vyao na wao sasa wanairejesha boti.