Nimepata taarifa kutoka kwa wadau fulani kwamba kesho mwenyekiti wa wafanyabiashara Tanzania Bwana Minja anapandishwa kizimbani Dodoma.
Kwa hiyo wafanyabiashara wanaendeleza mgomo wao wa kutofungua biashara siku mwenyekiti wao anapopandishwa kizimbani.
My take: Nimemsikiliza Minja kwenye power breakfast asubuhi anasema suala hili lilikuwa kwenye mazungumzo Kati jumuiya ya Wafanyabiashara na TRA, so kwanini serikali imfungulie kesi huyu Minja wakati suala liko katika mazungumzo.
hata mimi nimemsikiliza kwa umakini mkubwa sana Bw. Minja! ... Kudos Wafanyabiashara kwa kumpata kiongozi bora mwenye weledi mpana sana ... Huyu Jamaa akiamua kuiangusha serikali ya CCM anaweza ...
Aisee kazi kweli.
Maana watu wa nchi jirani walikuwa wanaanza kuja kuchukua mzigo baada yakusikia mgomo umeisha.
Mara wakija wanakuta tena yale yale.
Mombassa wanapanua bandari yao,sasa kuna kipindi itafika watu wataona bora waende kenya kuchukua mzigo nakukuta soko la hapa linashuka kwa kasi au wanagawa Customers.Hatime serikali kukosa mapatao.
Wangefanya kama Francis cheka tu,piga kifungo cha nje huku watu wanaendelea na yao,ila hii panda shuka hii ina hatari zake kwa taifa
Hii serikali legelege haiwezi hata kutekeleza sheria ya kodi ambayo imejadiliwa na kupitishwa na bunge! Ningekuwa waziri Mkuu ningefuta leseni za wafanyabiashara wote wanaofunga maduka kwa shinikizo la kukwepa mashine za efd. Mashine hizi ndizo zinatumika dunia nzima kuhakiki mapato na kukadiria kodi. Huko ulaya ambako tunatembeza bakuli hata wauza mboga sokoni wanazitumia na mboga zinatozwa vat! Futa leseni tuone jeuri yao ccm isibembeleze kura za wafanyabiashara za wafanyakazi na wakulima zinatosha.
Tatizo ni Elimu Ndogo waliyonayo. Kwanza wengi biashara zao za Mazindiko na kutoa kafara. Mtu wa vile unafikiri ni rahisi kumwambia aendeshe biashara kisasa akakuelewa?