Mgomo wa Simu Utafeli...

ZeMarcopolo

Platinum Member
Joined
May 11, 2008
Posts
14,279
Reaction score
7,681
Harakati za kugomea huduma za simu zinazofanywa na mkazi wa Marekani anayejitambulisha kwa jina la kujificha kama Mzee Mwanakijiji UMEFELI.

Kilichosababisha kufeli kwa mgomo huu ni kukosa tija.

Mwanaharakati huyo ambaye pia ni kinara wa kuitengenezea Tanzania maadui duniani alitamani kuona watanzania wanazima simu zao na kukosa huduma hiyo muhimu wakati yeye akiendelea kupata huduma zake bila matatizo.

Ikumbukwe kuwa mgomo huo umeitishwa siku za kazi ambazo wanafunzi watakuwa shuleni. Hii ni kumaanisha kuwa Mwanakijiji anahamasisha wazazi wazime simu na kutojali iwapo kutatokea habari ya dharura toka shuleni kuhusu watoto wao!!!

Tabia hii ya Mwanakijiji ambaye ni mwanaharakati wa Chadema inafanana na kitendo alichokifanya Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dr. Wilbroad Slaa Iringa ambapo alihamasisha vijana kukaidi amri halali ya Polisi na yeye mwenyewe akaitii amri hiyo na kujifungia hotelini. Uchochezi huu wa Dr. Slaa ulisababisha kifo cha mwandishi Mwangosi. Kila anapoulizwa kwanini hakuwepo eneo la tukio wakati yeye ndiye aliyeitisha maandamano Dr. Slaa amekuwa akipepesapepesa macho kwa aibu.

Bado haijafahamika kwanini Mwanakijiji amekuwa mchochezi wa vurugu nchini Tanzania ilhali yeye mwenyewe hataki hata kutembelea nchi hiyo ambayo kuna taarifa ambazo bado hazithibitishwa kuwa uraia wake ameshaubwaga.

Miongoni mwa vurugu alizochochea Mwanakijiji ni pamoja na :
kuhamasisha walimu wasifundishe wanafunzi
Kuhamasisha madaktari wasitibie wagonjwa
Kuhamasisha watu wasilipe kodi
Kumchochea Kadinali Pengo aanzishe vita
Kuhamasisha watanzania kususia mchakato wa Katiba Mpya
Kuhamasishwa wananchi waikataze serikali kununua mitambo ya kuzalisha umeme
Kusambaza habari za uongo juu ya Rais wa Nchi
Kuhamasisha chama cha siasa kuanzisha kikundi cha vurugu
Kuhamasisha watu waukatae Muungano
Kuhamasisha wananchi wakatae kushiriki shughuli za maendeleo.

Ni bayana kuwa mwanya wa kodi mpya ya simu unatumiwa na wenzetu hawa wasioitakia mema nchi yetu ili kutuchonganisha na kutusahaulisha jukumu letu kuu la kuijenga nchi yetu. Kwa bahati mbaya pamoja na kwamba Tanzania ni nchi yetu sote, lakini wapo wenzetu wanaofurahi kuona nchi inakuwa kwenye matatizo na migogoro!

Kufeli kwa mgomo huu ni ujumbe muhimu kwa wachochezi wa vurugu. Watanzania wameshatambua kuwa wachochezi hawa hawana malengo mema.

Kuhusu kodi ya simu, nchi yetu ina mfumo wa uwakilishi kwa njia ya Bunge. Tutumie mfumo huu kutoa mapendekezo yetu ya jinsi tunavyotaka kodi zetu zilipwe. Mfumo umewekwa ili tuishi kama jamii iliyostaarabika inayopanga mambo yake kwa utaratibu maalum. Tuendelee kukataa hawa wanaoibuka na kutufanya tuvutane katika vitu ambavyo tumeshaweka utaratibu wa kuvishughulikia.

Hongereni watanzania kwa kukataa uchochezi...

Mungu Ibariki Afrika,
Mungu Ibariki Tanzania...
 
Nani kakudanganya kuwa umefeli?

Jipe moyo, subiri kesho utaipata freshi, leo tunamalizia vijisalio vyetu pamoja na kuagana na ndugu jamaa na marafiki... Kuanzia sa 6 usiku wa leo simu zote tunatia kwenye maji

Mimi ingekuwa hiyi kodi itapekekwa kweli kwenye maendeleo nisingeona tatizo kuchangia hata kama ingekuwa elfu 10 kwa mwezi, tatizo hiyo kodi mpya ya line za simu ni kwaajili ya kampeni za ccm mwaka 2015 .... Tumechoka kuwaneemesha ccm na familia zao!
 
Nani kakudanganya kuwa umefeli?

Jipe moyo, subiri kesho utaipata freshi, leo tunamalizia vijisalio vyetu pamoja na kuagana na ndugu jamaa na marafiki... Kuanzia sa 6 usiku wa leo simu zote tunatia kwenye maji

Kuna watu hapa kitaa wanasema "akili za kuambiwa,..."

Mimi ingekuwa hiyi kodi itapekekwa kweli kwenye maendeleo nisingeona tatizo kuchangia hata kama ingekuwa elfu 10 kwa mwezi, tatizo hiyo kodi mpya ya line za simu ni kwaajili ya kampeni za ccm mwaka 2015 .... Tumechoka kuwaneemesha ccm na familia zao!

Propaganda nyingine ni BURE kabisa. Sasa kama lengo ni kupeleka kodi kwenye kampeni si inaweza kuchukuliwa kodi yoyote tu, kwani mpaka itoke kwenye simu?
Hakuna kodi inayokusanywa kwa ajili ya kampeni.

Wananchi wameshashtuka...
 
Kuna watu hapa kitaa wanasema "akili za kuambiwa,..."

Huna jipya wewe... Mgomo uko pale pale

Propaganda nyingine ni BURE kabisa. Sasa kama lengo ni kupeleka kodi kwenye kampeni si inaweza kuchukuliwa kodi yoyote tu, kwani mpaka itoke kwenye simu?
Hakuna kodi inayokusanywa kwa ajili ya kampeni.

Wananchi wameshashtuka...

Aah wapi...... Hatudanganyiki asee, bora mchukue huko pengine kimya kimya kama mlivyofanya BOT kipindi kile.... Hakuna mwananchi mjinga zama hizi!
 
mzee Mwanakijiji yuko U.S anapiga Simu eti anahamasisha mgomo Tz huyu mzee ni janga la nchi yetu aje agomee hata Tz.
 
mzee mwanakijiji yuko u.s anapiga cm eti anahamasisha mgomo tz huyu mzee ni janga la nchi yetu aje agomee hata tz.

Huyu jamaa sijui kwanini anaichukia Tazania kiasi hicho. Hajawahi kuhamasisha anything positive, yeye kila siku ni kuhamasisha migomo, vurugu, maandamano na vita...
 
Mwanakijiji anatumika vibaya sana na hana nia njema na taifa hii.
 
Kwani waandishi wa habari wanaofika kwenye mikutano ya kivyama ni wafuasi wa hivyo vyama? unapoweka mfaano wa mwangosi je uliufahamu uhusika wake?
 
Mwanakijiji anazeeka vibaya.. hakuna Mtanzania atakayezima simu.. wataongea kishabiki tu humu JF
 
Kwani waandishi wa habari wanaofika kwenye mikutano ya kivyama ni wafuasi wa hivyo vyama? unapoweka mfaano wa mwangosi je uliufahamu uhusika wake?

Tukio zima lisingekuwepo iwapo Wananchi wasingelaghaiwa na hivyo Mwangosi pia asingedhurika.
 
Magamba naona mumeimizana kumshambulia Mzee Mwanakijiji kwa sababu amekuwa mwiba kwenu! ama kweli Mbwa wa alalale fofofo, hulinda mali ya jirani
 
Last edited by a moderator:
Huyu jamaa sijui kwanini anaichukia Tazania kiasi hicho. Hajawahi kuhamasisha anything positive, yeye kila siku ni kuhamasisha migomo, vurugu, maandamano na vita...
Hivi hizi hoja zako nazo ndizo za kizalendo! Unaipenda nchi au unapenda fedha za nchi unazopewa na wezi walioshika madaraka. Mwanakijiji ni mzalendo anayependa nchi na watu wake. Nyinyi na ccm yenu mnapenda tu fedha za nchi na mnawakamua hata maskini wasiokuwa na uwezo wa kupata elf 1 kwa mwezi huku mkiwasamehe matajiri na makampuni ya madini ili mpate rushwa. Sasa tumechoka na nyinyi makupe wa nchi yetu mnaonenepa na kufura matumbo kwa damu zetu.
Huu mgomo wa simu ni kukanyaga tu klach ili kuweka gia ya migomo kamili dhidi ya serikali hii ya wauza unga, wauaji na walipuaji wa wananchi wasiokuwa na hatia kwenye mikutano ya amani ya siasa.
Kesho mgomo unaanza na utaendelea.
 
Kama mnajua kuna bunge kwanini msingesubiri utaratibu kabla ya kuanzisha hilo?...mkajifanya ni dharula....ni kwa ajili ya kampeni 2014/2015 huo ndo ukweli japo mchungu....hamumpati mtu ccm na ndo mana mwanakijiji kaamua kubaki huko....me pia ingekuwa na uwezo hili li nchi ni la kulihama tu hadi waje cuf,chadema,nccr na wengineo co ccm na ndo maana hawataki uraia wa nchi mbili wengi tusingerudi tena...puuuumbav
 
Kwa hiyo wewe unataka sisi wananchi tunyonywe kupitia mapato fisadi wewe ukila raha na box mamtoni? Mwanakijiji ni Mzalendo wa ukweli.
 
Hivi,ndo tuseme mwanakijiji nae atazima simu akiwa hapo America?...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…