Mgomo wa MAs nchi nzima

Sungurampole

JF-Expert Member
Nov 17, 2007
984
205
Mgomo wa Mortuary Attendants (MAs) nchi nzima unakuja. Katika kikao chao kilichokaa mjini Sikonge mkoani Tabora juzi wameamua kuanza mgomo tarehe 1.7.2013 kama serikali haitawatimizia madai yao waliyoyawakilisha kwa waziri mkuu kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

UNASHANGAA NA KUTOKUAMINI?

Kwa nini ushangae kwani wao hawana haki ya kugoma? Naleta wazo pana kuhusu migomo na stahili za watu. Kwa muda mrefu serikali yetu imejikuta ikihitaji kupambana na tatizo la mgomo huu au ule. Mingi ya migomo imekuwa ya makundi ya waajiriwa(walio kazini na wastaafu) na pili wanafunzi. Kwa bahati mbaya mara zote tumeyashughulia kizima moto na kwa lengo la 'kuzima mgomo' hata kama utarudi tena mwezi ujao lakini angalau kwa leo mgomo usimame. Ili kufanikisha kuzima hiyo migomo serikali inakubali madai machache kati yale yaliyotolewa kwa serikali. Wasiporidhika tunaongeza idadi ya madai yatakayotekelezwa, hivyo hivyo mpaka wakubali kuacha mgomo. Mara nyingine tukiona madai ni 'magumu kutekelezeka’ tunaacha mazungumzo na kutumia suluhisho mbadala- mfano mabomu,virungu, kutishia kuwafukuza kazi, chuo au shule au kwenda mahakamani kupinga mgomo husika. Kuna wakati tumeamua kuanza moja kwa moja na suluhisho mbadala na liliposhindwa ndipo tukaenda mezani.

Tunaweza kujadili busara iliyopo katika masuluhisho haya na lipi wakati gani ila sipo huko leo, wengi wameshasema. Langu ni je, kwa nini kila mara serikali yetu inakua inajibu(reactive)? Hivi wao kama 'viongozi' si walitakiwa kutoa mwelekeo kwa hiari yao, kwa utashi wao(proactive)? Hivi hii manpower/human resource inayotumika kuzima migomo inakuwa inafanya nini wakati migomo haipo ukiacha kazi za kila siku tena kwa BAU(Business As Usual)?

Jeshi zuri ni lile linalopigana kila wakati kama hakuna vita wanavianzisha hata kama vitakua vya mezani au kufanya tafakari ya vita vilivyopita. Hapa ndipo naona serikali yetu kila mara imepwaya. Natamani ningekua na wa kumwambia ningemuomba aingize dhana mbili muhimu serikalini: Dhana ya kuwa 'Proactive' na dhana ya kuwa na ‘reflection/tafakari sessions' nasema dhana nikiwa na maana ya dhana siyo shughuli. Tukifanikiwa katika hizi dhana tutakuwa 'a learning government' hii ni sifa nzuri na muhimu sana kwa maendeleo yetu kama taifa. Kungekuwa na 'think tank' ya taifa ningewaambia.

Nikirudi kwenye hoja yangu nimeona watu wakitoa viwango vya mishahara vya madaktari, waalimu na wengine na kuanza kubishana kuwa nani anapunjwa. Sijui ni wangapi (kweli!!) wanategemea viwango hivyo. Na kama sivyo wanavyotegemea vile wavyovitegemea vinakaa wapi katika bajeti na nini lengo la kuvicha? Kwa kusema hivi sitaki kuingia katika ugomvi na ‘wachumi daraja la kwanza’ ila natamani tufike mahali serikali yetu ikubali 'KWA DHATI' kuufikirie mfumo mzima wa ajira na stahili na waajiriwa serikalini kwa upana wake siyo kwa anayegoma tukifanya hiyo MAs hawatagoma mwakani.

Nimesema ‘kwa dhati’ kwani majaribio yaliyopita yalikosa utashi na yakaishia kuwa miradi ya posho

Nawasilisha

Mods mkiona vema mwaweza kuihamisha jukwa jingine ili kushirikisha wengi
 
Back
Top Bottom