Kuna mgomo wa daladala kituo cha Jamatini Dodoma. Nipo kwenye eneo la tukio na sababu ya madereva fikia hatua hiyo ni kutokubaliana na sheria ya level seat.
Dala dala za UDOM ndo hazipo kabisa kwa kua wao ndo vinara wa kubabanisha wanachuo ka ndizi. Mgomo huu umeathiri abiria wengi hasa wanafunzi wa UDOM kwa kua ndo abiria waliojaa hapa kituoni.
Kwa taarifa ni kwamba mazungumzo kati ya uongozi wa madereva na askari wa usalama barabarani bado yanaendelea kituo kikuu cha polisi kwa kua kuna baadhi ya daladala zimekamatwa.
Nashindwa weka picha kwa kua bado sina hako kautaalamu ila ndo kinachooendelea hapa eneo la tukio.