Mgomo wa daladala jijini Mwanza

Mgomo wa daladala jijini Mwanza

Na mgomo wa leo ni wa kisayansi, sijaona polisi na mabomu wala nini, watu wametelekeza hiace katikati ya barabara, wakasepa zao. Mulongo jipange upya baba

Mabatini mabomu yameisharindima .... chezea polisi wewe!!! Wakiamrishwa huwa hawatafakari,
 
hahahahahaha,napenda watu wanaokubali ukweli na kuwa kama wewe,nunua king'amuzi ndugu yangu,utatuchosha vidole kukufafanulia na mengine outomatic kujulikana.
 
Mabatini mabomu yameisharindima .... chezea polisi wewe!!! Wakiamrishwa huwa hawatafakari,

Nimeshapandisha bugando mkuu hata sijui kinachoendelea hapo kati
 
Wadau kama tutakumbuka vizuri,jana katika taarifa za habari kulikuwa na habari ya wamachinga kupewa maeneo mawili katikati ya jiji la mwanza na mkuu mpya wa mkoa bwa magesa mulongo,maeneo waliyopewa ni standi ya Tanganyika na ile ya magari ya kwenda airport kutokea Igoma.katika pitapita zangu asubuhi ya leo mjini nilikuta machinga wameamka usiku kuwahi maeneo katika sehemu hizo,hivyo kukawa top hakuna gari kuingia wala kusha pale Stand ya Tanganyika,na ile nyingine.Kufuatia kitendo hicho,watu wa daladala wamejipanga vyema hasa wale waliokuwa wanatumia maeneo hayo wamegogoma,na wamezifunga barabara zote za katikati ya mji kwa kuegesha magari barabarani na wao kushuka.

My take: Wakati wa Ndikilo,kulikuwa na mpango wa halmashauri ya jiji la Mwanza kusafisha mji kwa kuwatoa wamachinga katikati ya mji,zoezi lililotumia million mia 2,sasa iweje leo warudishwe tena kwa kupewa maeneo makubwa zaidi?nadhani Mulongo anafanya hivi kuwafuta machozi machinga wa Mwanza,ili kumpiga kumbo Wenje ambae amekuwa mstari wa mbele kuwatetea,ili kuirahisishia CCM kupiga kampeni vizuri katika uchaguzi mkuu ujao,na baada ya hapo,wawafukuze tena.

Magesa hii ni Mwanza,usipotulia na kutumia Busara utaomba uhamisho mwenyewe,ila ukiwa mstaarabu kama wana Mwanza walivyo,hautatamani kuhamishwa.

Mmhhhh....2m au 200m? If the later tunaomba mchanganuo
 
Mimi binafsi leo nimepata taabu ya mwaka wakati nilipokuwa mjini na gari langu ndogo. Barabara ya kutoka mjini kuja Nyakato na ya Nyerere Road haipitiki. Kuna Mabus mengi yamesimama Nyerere Road tangu saa mbili asubuhi yakielekea Musoma, Sirari, Bariadi hakuna njia ya kupita. Watoto wanalia na hakuna njia ya kuwasaidia. Magari makubwa yamesimama njia nzima ya barabara ya Nyerere hakuna kupita. Wanaoenda Bugando kwenda kuona wagonjwa hakuna njia ya kupita. Pote pamezibwa na magari yaliyosimama njiani. Tunamwomba Mkuu wa Mkoa yeye ni mgeni, unapoingia kwenye mji wa watu kwanza uliza watu wa pale na baadaye achukue uamuzi. Uamuzi alioufanya ni wa kukurupuka na italeta madhara makubwa na atayajutia.
 
Bosi hufatilii taarifa za habari zinazoonyesha muheshimiwa mkuu wa mkoa maagizo anayoyatoa?
Nafikiri hakutakiwa kufanya hiki alicho kiagiza wala haifikirii Mwanza ya kesho.Pia kwa wamachinga ni changa la macho.Sisiti kuhisi baada ya uchaguzi mkuu vurugu za mgambo wa jiji na wamachinga zitarejea upya.Maana city Centre kwa sasa imekuwa ni vurugu tupu
 
Back
Top Bottom