NGAZIJA YOGAYOGA
Member
- Aug 1, 2013
- 31
- 3
Wiiki mbili zilizopita baada ya wanafunzi wa chuo kikuu cha St. john's kugoma mnamo tarehe 19,Novemba,2014.Wanafunzi hao wameanza tena mgomo leo hii tarehe 4, Desemba,2014 baada ya Rais wa serikali ya wanafunzi, Bw. Daniel Damian na Waziri mkuu wa serikali yake kutangaza mgomo mpya baada ya kero ambazo zilisababisha mgomo hou kushindwa kutatuliwa.MGOMO HUO unatarajiwa kuisha kesho Ijumaa tarehe 5,Desemba,2014 saa 6 adhuhuri mbele ya waziri mkuu au Waziri wa Elimu. Mgomo huu umeanza baada ya wahadhiri pia kuanza mkutano usio na kikomo (EXTENDED MEETING) kushinikiza uongozi wa chuo hicho kuwalipa ujira wao.CHUO HICHO KINACHOMILIKIWA NA KANISA LA ANGLICAN KINAKABILIWA NA MATATIZO KEDEKEDE. HIVYO MGOMO WA wanafunzi hao utasaidia walimu kulipwa mshahara wao na hata kero lukuki za wanafunzi kutatuliwa kikamilifu.Kufuatia mgomo huo,serikali ya wanafunzi imetuma ujumbe kwa wanafunzi wote kuwa ;
hakuna mwenye ruhusa ya kuonekana mazingira ya chuo hicho mpaka hapo keshoo. JE NINI HATIMA YA ELIMU YETU WATANZANIA??.
JIBU TUNALO WENYEWE!!!
hakuna mwenye ruhusa ya kuonekana mazingira ya chuo hicho mpaka hapo keshoo. JE NINI HATIMA YA ELIMU YETU WATANZANIA??.
JIBU TUNALO WENYEWE!!!