mkuu, tpaul usitokwe povu. Maendeleo huanzia nyumbani. Hivi chadema mpaka leo bado mmepanga ofisi pale ufipa nyumba ya mkwe wa mwenyekiti wenu, hayo ndio maendeleo? Mpaka sasa hela za harambee na ruzuku mmeshapiga hesabu ya mapato na matumizi? Kuhusu ufisadi, je ni nani aliyewauzia chagadema maspika na mafuso mabovu kwa mamilioni ya pesa kama sio mwenyekiti? Ni nani alijipa kazi ya ununuzi na uagizaji pikipiki toka japan na akapiga hela bila kutagaza zabuni wala wala kufuata kanuni za manunuzi? Yote inayowafanya mgawane majimbo na madaraka kabla ya uchaguzi ni kiu ya kufisadi mali za nchi kwa kuwatumia watanzania wasio waerevu wanaodhani chadema ina dhamira ya kweli ya kuleta maendeleo, kumbe wachaga wanajipanga kuigeuza nchi kuwa saccos yao. Kuna watu wamejikopesha ruzuku na hadi leo hawaulizwi maana wao ndio chagadema halisi! Kumbuka, kuna chadema chumbani na chadema sebuleni, sasa wewe uko upande upi!!
mkuu wewe utakuwa binadamu wa ajabu unayependa kuona wamama zetu na wanachi kwa ujumla tukikosa huduma bora mahospitalini, majengo mazuri ya madarasa lakini hayana walimu na miundombinu muhimu, walimu na watumishi wengi wa umma kutolipwa madai yao ya msingi kwa miaka kadhaa sasa, serikali kuwakopa hata wakulima wa kutumia jembe la mkono, wanavyuo kukosa mikopo yao na hivyo kuhatarisha maisha yao na hasa mabinti zetu, madereva wangi wa sekta ya umma kufanya kazi kama vibarua ktk maisha yao yote, waonevu wa wanyonge kupandishwa vyeo, wezi na mafisadi papa kuendelea kula bata huku wezi wa simu na kuku wakisurubiwa magerezani, barabara zimejengwa kwa lami lakini chini ya kiwango na mengine mengi yanayo fanana nayo.... Sasa watu wakisema oooh wapinzani ndy kazi yao, hapana ndg yangu jamii sasa wanajitambua na kama ulikuwa unasubiri wajitambue kwa hisani ya watu wa marekani basi pole sana.
chagadema nyie kazi yenu kuu ni kuratibu migomo kama mlivyotoa ahadi kwamba mtahakikisha nchi haitawaliki. Kwa habari hii, mmejidhihirisha wazi tena kijinga sana kwamba ndio mnaratibu civil disorder kwa kujinufaisha kisiasa. Lakini kumbukeni huu uratibu mnaofanya, wananchi wenye akili timamu wameshawabaini na wanawasubiri kwenye sanduku la kura. Unapoandaa mgomo tena kibaya zaidi unawaunganisha madaktari kwa kuweka vipicha vyenu vya uchochezi, unadhani nani hajui kuwa ndio mnaandaa migomo hiyo!! We kundi gani la wafanyakazi limewatuma mlisemee katika makundi haya? Yaani kwa habari hii chadema mmeumbuka bayana na kutambulika wazi kuwa ni wachochezi wa migogoro. We unadhani mtu akifiwa na mpendwa wake kwa mgomo ulioasisiwa na chadema unadhani atawachagua?! Hebu mjipange vizuri maana kila njia inawabana! Mmetumia wachungaji majukwaa ya siasa, baadhi ya mapadri akiwemo mgombea wenu wa urais, lakini bado mmeona nanga inapaa mnakuja humu jukwaani kuratibu migomo!! Shame on you chadema.
haa haa kwa walimu siamini labda madaktari.
Hawa inabidi wawe na mkakati wa kuachana na kugoma kundi moja tu la Wafanyakazi. Wawe na mawasiliano ili wakiamua kugoma wanagoma kwa pamoja wafanyakazi wote nchini wakiwemo madaktari, walimu wote nchini kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu, manesi na wafanyakazi wengine wote. Mgomo kama huu ndio utakaotikisa nchi na kuifanya hii "Serikali sikivu" kutia akili kichwani kwamba Wafanyakazi nchini wamechoshwa na porojo zao na nyimbo yao ya kila siku "Serikali haina pesa"
Wishful thinking.
Chadema baada ya kula virungu mara kwa mara na migomo yao huko nyuma sasa wamekuja na njia mpya kuwarubuni wengine.
Tumeshtukia.
Taarifa kutoka duru za walimu na madaktari zinadai kwamba watumishi hawa wa umma wapo mbioni kugoma ili kuishnikiza serikali ya CCM kuwalipa madai yao kama ilivyowaahidi miaka kadhaa iliyopita kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu:
MADAKTARI
Madaktari wanaidai serikali madai mbalimbali ikiwemo kuboresha maslahi yao na mazingira ya kufanyia kazi, kuwalipa oncall allowance na posho ya kufanyia kazi katika mazingira hatarishi, kuboresha huduma za hospitali (dawa, vitanda, vitendea kazi, nk), kuthamini taaluma ya udaktari, nk. Utaona kwamba madai yao yamejikita katika sehemu kuu mbili ambazo ni uboreshwaji wa mazingira ya kazi na vifaa vya tiba na uboreshwaji wa kipato, kinga na afya za madaktari (Mishahara, posho na Bima ya afya).
WALIMU
Walimu wanaidai serikali mabilioni ya shilingi ikiwemo posho, malimbikizo ya mishahara, kupandishwa vyeo, nk. Walimu ndio watumishi wa umma wanaolipwa fedha kidogo zaidi kuliko watumishi wote wa serikali; na pia kazi yao haithaminiwi hata kidogo na serikali ya CCM. Kumbuka siku za nyuma Waziri wa CCM, Bi Hawa Ghasia aliwahi kuwadhihaki kwamba kama hawataki kulipwa mishahara kidogo basi watafute kazi nyingine tofauti na ualimu kwa kuwa siku zote kada ya ualimu wataendelea kulipwa mishahara kidogo so long as ni wengi sana ukilinganisha na watumishi wengine wa serikali. Hivyo, kama serikali ikiwalipa vizuri, itafilisika!
WAFANYAKAZI WENGINE
Nao wafanyakazi wa kada zingine wanaoidai serikali mabilioni ya shilingi wanasubiri walimu na madaktari walibumbulie, nao waunge tela. Safari hii sioni namna ambavyo serikali itakavyoweza kuuzuia mgomo huu mtakatifu. Ni rahisi kuzuia mafuriko kwa mikono kuliko kuuzuia mgomo huu. Sisi yetu macho wafanyakazi wa serikali wakilianzisha nasi wananchi tuunge tela. Bila kufanya hivyo, serikali hii ya CCM itaendelea kuchezea maisha ya watanzania mpaka kiyama. Tazama jinsi hospitali na shule za makabwela zilivyo taabani huku kila kukicha tunasikia mafisadi wa CCM wakikwapua mabilioni ya shilingi bila kuchukuliwa hatua zozote.
View attachment 254823View attachment 254824View attachment 254825View attachment 254826View attachment 254827
MAONI YANGU
Mimi naona kama mgomo huu umechelewa sana. Ulipaswa ufanyike mapema na maslahi yanelikwishaboreshwa kitambo sana. Wafanyakazi wan chi hii ndio itakuwa chachu ya mabadiliko. Sisi raia wa kawaida tunapaswa kuwaunga mkono wafanyakazi kwani kuboreshwa kwa maslahi yao kuna manufaa makubwa sana kwa wananchi wa kawaida. Aidha, madai yao yanajumuisha uboreshaji wa huduma za tiba kwa wananchi; na hapa kila mwananchi atanufaika kwani ubovu wa huduma katika hospitali na shule zetu unamuathiri kila raia mnyonge isipokuwa wale mafisadi wachache wasiotibiwa katika hospitali za umma na wasiosoma katika shule za walalahoi (shule za kata).
:israel: