Mgomo mkubwa wanukia nchini


Tatizo hiyo migomo ya kimya kimya haiwasumbui watawala. Wanahangaika migomo ikiwa wazi. Si umeona mgomo wa made revamped ulivyowatesa!! Au ule mgomo wa Ulimboka ulivyowakimbiza juu chini!? Hii ya kimya kimya inawaumiza tu wananchi ambao hawajui hata haki zao.
 
Kama katibu mkuu wa CWT bado ni yule yule Oluochi niliyemuona wakati wa bunge la katiba, naweza ku bet kuwa mgomo utashindwa kabla ya kuanza.

Ni kweli huyu jamaa nina hakika yuko ile idara - tiss
 
Mkuu tatizo kubwa la nchi yetu ni wananchi,maana ndo wanahongwa T-shirt na kofia khanga na vitenge na kuweka
madarakani majanga badala ya viongozi,hivyo wananchi huenda wakiwa na hali ngumu akili itakaa sawa.

wananchi wanatakiwa kuitambua nguvu ya kura yao na waitumie ipasavyo.
ipo siku tutampata kiongozi sahihi.
 
Walimu wa shule za umma wamekuwa kwenye migomo siku zote, hii inadhihirishwa kwenye matokeo ya wanafunzi Wa shule za umma
 
Walimu hawawezi kugoma hata siku moja wanaingiza hela kwa siku kila mwalimu anaweza kuondoka shule na 20000 au zaidi hiyo ni posho ambazo wanazipata kwa kuwalazimisha watoto watoe ada za tuition
 
Walimu wa shule za umma wamekuwa kwenye migomo siku zote, hii inadhihirishwa kwenye matokeo ya wanafunzi Wa shule za umma

Mbona kila mwaka serikali inatuaminisha kwamba matokeo ni mazuri kwa kishindo...kwamba 95 ya wanafunzi hufaulu kuingia sekondari kila mwaka? Matokeo ni mazuri siku zote, hata kama yakiwa mabaya serikali itashusha GPA ili yakae vizuri. Unaona eeh?
 
walimu hawawez goma

kama ni kweli chadema wanahusika, basi wanastahili pongezi na wanafaa kuongoza nchi hii...tuwape kura zote oktoba watusaidie kurudisha maadili ya kitaifa yaliyopotezwa na CCM.
 

Chagadema nyie kazi yenu kuu ni kuratibu migomo kama mlivyotoa ahadi kwamba mtahakikisha nchi haitawaliki. Kwa habari hii, mmejidhihirisha wazi tena kijinga sana kwamba ndio mnaratibu civil disorder kwa kujinufaisha kisiasa. Lakini kumbukeni huu uratibu mnaofanya, wananchi wenye akili timamu wameshawabaini na wanawasubiri kwenye sanduku la kura. Unapoandaa mgomo tena kibaya zaidi unawaunganisha madaktari kwa kuweka vipicha vyenu vya uchochezi, unadhani nani hajui kuwa ndio mnaandaa migomo hiyo!! We kundi gani la wafanyakazi limewatuma mlisemee katika makundi haya? Yaani kwa habari hii chadema mmeumbuka bayana na kutambulika wazi kuwa ni wachochezi wa migogoro. We unadhani mtu akifiwa na mpendwa wake kwa mgomo ulioasisiwa na chadema unadhani atawachagua?! Hebu mjipange vizuri maana kila njia inawabana! Mmetumia wachungaji majukwaa ya siasa, baadhi ya mapadri akiwemo mgombea wenu wa urais, lakini bado mmeona nanga inapaa mnakuja humu jukwaani kuratibu migomo!! Shame on you chadema.
 
Ni kweli huyu jamaa nina hakika yuko ile idara - tiss

Kwani migomo ni sifa! Chadema mmechoka sana siasa, sasa mnatafuta shari kuratibu migomo, na kwa hili mmeshafeli kabala ya kuanza kwani tumewashtukia. Chama cha chadema ovyo kabisa!
 
mkuu rallphryder hebu jirudishie akili kidogo, utazame hizo picha jinsi wamama wanavyoteseka hospitalini huku CCM mkifisidi pesa za umma kila siku. hebu tazama jinsi huyo mjazito alivyobebwa kwenye ambulance ya toroli maskini! kuweni na huruma japo kidogo na ustawi wa wananchi kwani hao watoto wanaosomea chini ya miti ni binadamu na wanastahili kusomea katika mazingira bora. wewe unadhani mafisadi wa CCM wanavyokwapua fedha za umma na kuwaacha wananchi wakiteseka hivi ni sahihi mkuu?

SWALI LA KIZUSHI
Hivi ni kwanini kila hatua inayolenga kuboresha maslahi ya wananchi kwa ujumla mnaihusisha na CHADEMA? ina maana nyie CCM hampendi kuona wananchi wakiondokana kero za huduma mbovu za umma?
 
Last edited by a moderator:

Hapo sasa ndio umenyoosha maelezo vizuri kwamba ni kweli umetumwa kuratibu mgomo. Ila umechelewa, wananchi wanajua janja zenu chadema, na watawapa discipline ndani ya balot box.
 
Last edited by a moderator:

Sio Tanzania niijuayo leo hii. Kila mtu anajali maslahi yake mwenyewe..
 
Hapo sasa ndio umenyoosha maelezo vizuri kwamba ni kweli umetumwa kuratibu mgomo. Ila umechelewa, wananchi wanajua janja zenu chadema, na watawapa discipline ndani ya balot box.

kwa hiyo nyie CCM zile fedha bilion 300 za ESCROW za wananchi mlizokwiba ndizo zitawafanya wananchi wawape kura kwa kishindo au ni hizi bilion 600 mlilizokwapua juzi? hebu nyoosha maelezo wananchi waelewe ili wawape kura za kishindo kwenye ballot box (sio BALOT box kama ulivyoandika weye!).
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…