VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Huu mgomo umeshaanza muda mrefu wala si suala la tetesi. Hiyo Ijumaa ni kutekeleza hatua ya pili endapo serikali haitasikiliza madai yao. Hatua ya kwanza wameanza kwa kuendesha mabasi kulingana na alama za barabarani. Kwamba kama ni spidi 50 basi ni 50, kama ni spidi 30 basi ni 30. Na kwa upande fulani imeleta effect kubwa kwa wasafiri, mfano Dar - Iringa ilikuwa basi likitoka saa 12 asubuhi Ubungo linafika Iringa saa 7 mchana, ila kwa huu mgomo wao wanafika saa 11 jioni.
Walimu wa nchi hii wanashindwa na madereva na makondakta ambao kila siku tunawabeza ni wanywa viroba huku Walimu wakilipa kisasi kwa wanafunzi kuwafundisha hovyo na kuwafelisha baadala ya kuikaba serikali elimu iwe bora na mishahara yao"!
Mathalani,kwa nini nyumba za NHC katikati ya miji wasipewe watumishi wa umma ie WAALIMU na MADAKTARI ili wawe karibu na vituo kazi na kuwapa nafuu ya maisha baadala ya wahindi ambao wanapack magari ya 100 million nje wakati wanaishi nyumba ya umma na wanaweza kujenga huku waalimu wakiadhrika??!!! Kwa nini walimu hawagomi??!! Ama ndio kuwa kada ya ualimu na upolisi zinaongoza kuwa na watu vihio ambao hawawazi nje ya box zaidi ya rushwa na kumkomoa mwananchi??!!
Naamini siku WAALIMU wakigoma nchi nzima mwezi mmoja basi shule zetu za kata zitaboreshwa sanjari na maslahi ya walimu,mgomo ni haki na haki haitolewi bure kwenye kisahani,ukipewa bure basi unahongwa kama sio kutongozwa ili utumike,kwa nchi zetu zenye watawala wapuuzi!!!!
Huu mgomo umeshaanza muda mrefu wala si suala la tetesi. Hiyo Ijumaa ni kutekeleza hatua ya pili endapo serikali haitasikiliza madai yao. Hatua ya kwanza wameanza kwa kuendesha mabasi kulingana na alama za barabarani. Kwamba kama ni spidi 50 basi ni 50, kama ni spidi 30 basi ni 30. Na kwa upande fulani imeleta effect kubwa kwa wasafiri, mfano Dar - Iringa ilikuwa basi likitoka saa 12 asubuhi Ubungo linafika Iringa saa 7 mchana, ila kwa huu mgomo wao wanafika saa 11 jioni.
Na wavuvi wanapanga kugoma