maroon7
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 11,345
- 15,854
Kuanzia asubuhi ya leo kumetokea mgomo mkubwa wa daladala Iringa mjini na kusababisha adha kubwa ya usafiri manispaa yote ya Iringa.
Vituo mbali mbali vimeonekana kujaa abiria huku wengi wakionekana kutembea kwa miguu kuelekea maeneo ya katikati ya mji hasa wanafunzi, nimepita maeneo ya Kihesa mida ya sa 2 kamili asubuhi hii na kushuhudia idadi kubwa ya watu kituoni huku mawe yakiwa pembeni mwa barabara ambayo inasemekana yaliwekwa kuzuia magari binafsi kusimama ili kulazimisha kutoa lifti hali iliyopelekea askari kufika na kufanikiwa kuyaondoa.
Kwa upande mwingine taxi na bodaboda zimekua adimu kwenye vituo vyao kutokana na kuwa bize na abiria wengi waliokua wanawahi makazini. Maeneo ya NMB na Posta sikuona taxi yoyote tofauti na ilivyozoeleka. Inasemekana chanzo cha mgomo ni SUMATRA kuingilia hali ya daladala kukatiza route na kuishia kituo miyomboni na posta ambavyo havipaswi kuwa vituo vya mwisho kama wanavyofanya madereva wa daladala. Tofauti na kawaida ambapo Miyomboni ndio daladala zinapopaki,asubuhi hii hakuna daladala hata moja.​