Mgombea wa Chadema Siha Kupinga Matokeo Mahakamani

Commodores

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2018
Posts
289
Reaction score
335
Na Ferdinand Shayo
Aliyekuwa Mgombea Ubunge kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CDM) jimbo la Siha Mkoani Kilimanjaro Bw elvis Mosi amesema kuwa ana mpango wa kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Dr Godwin Mollel wa CCM kwa madai kuwa taratibu na kanuni za uchaguzi zilikiukwa hivyo anatarajia kulifikisha suala hilo mahakamani.

Bw Mosi ambaye alipata kura 5905 dhidi ya kura 25611 za Dr Mollel amesema, wanakusanya ushahidi wa kutosha ambao utaiwezesha mahakama kutengua matokeo hayo na uchaguzi kurudiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake sanya juu bw mosi amezitaja baadhi ya taratibu hizo kuwa ni pamoja na kubadilisha matokeo ya kura zake katika vituo na kupewa dr mollel jambo ambalo lilimfanya asisaini fomu za matokeo..insert ya bw elvis mosi mgombea ubunge wa ccm jimbo la siha.

Afisa 0ganizesheni wa Halmashauri na serikali za mitaa wa cdm kanda ya kaskazini Bw Ndonde Totinan amesema, matokeo ya kata 11 kati ya 17 ya jimbo hilo yana utata mkubwa ambao hawaridhiki nao na idadi ya kura zilizopigwa ziliongezwa katika baadhi ya vituo....insert ya bw ndonde totinan afisa ognizesheni wa CMD kanda ya Kaskazini.

Naye Mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CUF Bw .Tumsifuel Mwanri ambaye hakusaini fomu za matokeo amesema, uchaguzi huo haukuwa huru na ulijaa ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadam.
Sources: Muungwana Blog
cf1606da86f6c92a286fadf9f208d512.jpg
 
Ni kupoteza muda tu na rasilimali za mahakama!
 
Hiyo ndio siasa tunayoitaka, siyo ile ya maandamano yasiyo na kichwa wala miguu!
Huyu aliyekuwa mgombea wa Siha kupitia Chadema ni mtu makini sana hata wakati wa kampeni aliendesha kampeni zake kiustaarabu sana. Nina uhakika mahakama zetu zipo huru na zitamtendea haki
 
Anapeleka kesi kwa hawa hawa ma-judge wanaopigwa biti kwenda SA kula bata
 
Ni uamuzi mzuri ikiwa hakuridhika na matokeo, ajipange tu kuwa na ushahidi wa kutosha kuishawishi mahakama.
 
Mahakama hizi hizi za ambazo wanasema ni za ccm au zingine, kura zike zile elf 25 kwa elf 5? hiyo hela si akafanyie mradi mwingine?
 
Tuombe tu Mola wetu akutangulie huko mahakamani ukakutane na watenda haki dhidi ya 'yule mwovu'
 
Back
Top Bottom