karanga mbichi
JF-Expert Member
- Aug 8, 2014
- 269
- 222
Katika hali isiyo ya kawaida Jijini Arusha baada ya juzi CCM kuzindua kampeni zao katika uchaguzi mdogo wa serikali ya mtaa wa Olamuriaki na mgombea wake kuungwa mkono na mamia ya wakazi wa mtaa huo ambao hapo mwanzo ulikuwa ni ngome ya CHADEMA,mgombea wa CHADEMA, mr Selemani Said Haji {pichani}ameamua kujitoa.
Habari zilizotufikia mpaka sasa ni kuwa mgombea huyo alishuhudia umati mkubwa wa wapiga kura hao ambao walikuwa wameambatana na mgombea kupitia CCM mr. Godfrey Kitomary hali iliyosababisha taharuki kubwa kwa makada wa CHADEMA walioongozwa na diwani wa kata ya Sombetini bw. Ally Bananga,mwenyekiti wa banda mbili mr. Choka,mwenyekiti wa mtaa wa Simanjiro mr. Piniel na kuamua kujitoa ktk mbio za kuelekea uchaguzi huo unaotarajia kufanyika tarehe 17/4/2016.
Akihojiwa na chanzo chetu mgombea huyo aliyejitoa katika mbio hizo alithibitisha na kusema kuwa haungi mkono uongozi wa kata (CHADEMA)kwa sababu ndio waliomtengenezea mazingira ya kushindwa uchaguzi huu.
Pia Alienda mbali zaidi kwa kusema ktk uongozi wa Bananga kata ya Sombetini hatarajii miujiza kuibakisha CHADEMA 2020.
Nakala ya barua yake ya kujiuzulu ametuahidi kutupatia pindi tu akiikabidhi ktk ngazi husika.