Mgombea wa CCM hatarini kufilisika.

Idimulwa

JF-Expert Member
May 27, 2011
4,503
1,722
Aliye kuwa mgombea wa udiwani kata ya Kirumba jijini Mwanza, katika uchaguzi mdogo uliofanyika mwanzoni mwa mwezi huu kupitia CCM na mfanyabiashara mashuhuri bwana Jackson Robert maarufu kama 'Masamaki' ameripotiwa kuyumba vibaya katika biashara zake kiasi cha kushindwa kuwalipa mishahara wafanyakazi wake kwa takribani miezi miwili sasa.

Mpaka sasa bwana Masamaki yuko kwenye mgogoro mkubwa na wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi anayoimiliki ijulikanayo kwa jina la Victoria Support Services Ltd yenye makao yake makuu jijini Mwanza-Mtaa wa Nera,kwa kushindwa kuwalipa mishahara yao kuanzia mwezi Februari mpaka sasa.

Pia amelazimika kuifunga klabu yake maarufu hapa jijini Mwanza ijulikanayo kwa jina la 'The Stone Club' huku wafanyakazi wake pia wakilalamika kutolipwa mishahara yao kwa takribani miezi mitatu.

Wengi wa wafanyakazi wake wamekuwa wakihusisha hali hiyo kuwa imesababishwa na bosi wao kujiingiza katika kinyang'anyiro cha kugombea udiwani hali iliyo mlazimu kutumia kiasi kikubwa cha fedha ili kupata ushindi kuanzia kwenye kura za maoni ndani ya chama chake na kwenye kampeni za kuwania kuchaguliwa na wananchi ambapo alichuana vikali na mgombea wa CHADEMA,ndugu DANIEL KAHUNGU.“...Tulijaribu kumshauri bosi wetu kupitia watu walio karibu naye kumuomba asigombee kwani nguvu ya CHADEMA Mwanza kwa sasa inatisha
maana sisi ndito tunaishi na watu wengi huku mitaani na tunaijua hali halisi vizuri lakini hakuwa tayari kushaurika...”Alilalamika dada mmoja aliyejitambulisha kuwa mmoja wa wafanyakazi wa klabu ya The Stone..na alikwenda mbali zaidi kwa kudai kuwa matatizo ya mishahara yalianza mara tu bosi wao alipotangaza nia.

Uchaguzi wa udiwani Kirumba ulifanyika kufuatia kifo cha diwani NOVATUSI MANOKO(CHADEMA) kilichotokea mwaka jana.Hata hivyo CHADEMA kupitia mgombea wao walifanikiwa kutetea tena kiti hicho katika uchaguzi uliokuwa na upinzani mkali kati ya vyama vya CDM na CCM.

Wakati ngome ya CCM iliongozwa na waheshimiwa mawaziri SITTA na NGEREJA,Lameck Airo-Mbunge wa Rorya na Mwita Gachuma-Mjumbe wa NEC ngome ya CDM ilikuwa chini Mheshimiwa ZITTO KABWE mbunge wa Kigoma Kaskazini,akisaidiwa na wabunge wote wa Mwanza,Kiwia-Ilemela,Wenje-Nyamagana na Machemuli-Ukerewe.

Hata hivyo Kiwia na Machemuli walishindwa kushuhudia zoezi la upigaji kura baada ya kucharangwa mapanga na watu waliodhaniwa kuwa wafuasi wa CCM usiku wa kuamkia siku ya upigaji kura na kulazimika kupelekwa Muhimbili kwa matibabu.


Nawasilisha.
 
Huyo bwn, masangara(masamaki)mwambieni aende kwa chama cha magamba,wamchangie,kwani ni wao waliomtuma agombee!!
 
Zamani ukipita magamba unapata za raia pia,cku izi kugombea magamba ni mzigo wa familia
 
Dawa ishamwingia huyo! maumiv anayasikilizia peke yake,wapambe washaanza mbele!!!! Hatothubutu tena huyo!!!
 
Ahsante mkuu kwa taarifa.Mwenye habari za SIOI atupie tujuzane
 
Ahsante mkuu kwa taarifa.Mwenye habari za SIOI atupie tujuzane maana nasikia alipata DEGEDEGE.
 
Alifikiri siasa za sasa ni mambo ya alfu ulela akapiga kampeni za kizamani. Siku hizi muhimu kusoma mwelekeo wa upepo kwani ni mara chache nguvu ya fweza kufanya kazi. Nguvu ya fedha siku hizi inakwenda opposite direction? Sasa mikopo ya benki atalipaje kama si kufilisiwa?
 
fedha za laana upotea hivyo hivyo kilaana laana tu, kwanini watumie fedha kwenye chaguzi? wajifunze cdm kinatakiwa kichwa chako si fedha mfano kwa ticha pale igunga hana kitu lakini kaikimbiza ccm mpaka imetumia kama b 2 hivi
 
Nimeamini hata Mengi akigombea udiwani kwa tiketi ya CCM atashindwa. Watu wanamkubali Mzee Yusufu; Alamba, alamba tena, aaam. Ukiwapa kitu wanalamba na wanakutosa vilevile.
 
Back
Top Bottom