MWANAMAKOROKOCHO
Member
- Jun 25, 2015
- 23
- 5
Macho & masikio ya Watanzania ( wana CCM & upinzani) yako Dodoma kuona na kusikia Chama cha Mapinduzi kinapitisha jina lipi katika kinyanjiro cha kwenda Magogoni.
Mimi hili halinipi hofu maana mchakato unahusisha chama kimoja tu, ila wasiwasi wangu upo katika kusamabaratika kwa Umoja unaojiita UKAWA.
Kwa maana sidhani kama Wana CUF bara na Zanzibar watakubali kipenzi chao Mh. Professor Ibrahim H. Lipumba asiwanie nafasi nyeti ya Urasi kwa elimu yake aliyonayo halafu abaki anaelea elea tu na wakati katika mikutano yake wafuasi wa CUF wanamuita kuwa ndiye Rais.
Kwa upande mwingine CHADEMA sidhani kama wanaweza kukubali mgombea nafasi hiyo nyeti hasitoke ndani ya Chama hicho wakati wanaimani wao ndiyo chama cha upinzani chenye nguvu kubwa na watu makini.
Wakati huo tayari NCCR-MAGEUZI wao wana sumu moyoni kwa kutoridhika na mgawanyo wa majimbo katika nafasi ya Ubunge.
Najua nitapata comments za mashambulizi ila ukweli ni kwamba UKAWA upo katika wakati mgumu sana katika nafasi ya urais na ukilinganisha kuwa viongozi wa vyama hivyo hawajawahi kuachia Madaraka ya Umwenyekiti na wengine wametengua vifungu vya katiba zao ili waendelee kuwa Wenyeviti wa miaka mingi zaidi.
@ Hakuna Mpango Kazi Mkubwa Duniani Kama Binadamu kupangilia Maisha Yake Mwenye@