GE2025 Mgombea Ubunge wa Uyole, Dkt. Tulia Ackson apiga kura. Awahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi

GE2025 Mgombea Ubunge wa Uyole, Dkt. Tulia Ackson apiga kura. Awahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,559
Reaction score
3,953
Mgombea ubunge wa Jimbo la Uyole mkoani Mbeya, ambaye pia ni Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, ametoa wito kwa wananchi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kutimiza haki yao ya msingi ya kikatiba.

Dkt. Tulia ameyasema hayo leo Oktoba 29, 2025, mara baada ya kupiga kura katika Kituo cha Tambukaleli, ambapo amepongeza mwamko mkubwa wa wananchi waliojitokeza mapema asubuhi kushiriki zoezi hilo huku kukiwa na hali ya amani na utulivu.

Amesisitiza kuwa Jeshi la Polisi lipo kwa ajili ya kulinda usalama wa wananchi na siyo kuwatisha, hivyo wananchi waendelee kujitokeza kwa utulivu na nidhamu kutekeleza wajibu wao wa kiraia.

 
Back
Top Bottom