Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,437
- 5,235
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Saashisha Mafuwe leo Ijumaa Septemba 5,2025 amefanya ziara yakuwatambulisha kwa wajumbe na wanachama wa chama hicho, wagombea wa Udiwani wa Halmashauri ya Hai waliopitishwa na CCM kugombea nafasi hiyo.
Saashisha Mafuwe ametumia usafiri wa anga (Helikopta) kupita kwenye baadhi ya kata ikiwemo kata ya Kia, Kata ya Rundugai, Machame Kaskazini, Masama Magharibi na kufanya mikutano ya hadhara na wanachama hao.
Katika ziara hiyo ameeleza kuwa katika kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja atahakikisha kuwa sera yake ya Kilimo utalii kwenye mashamba ya Ushirika inafanikiwa ili mashamba hayo yakawe na tija.
Hata hivyo Saashisha ameeleza kuwa uzinduzi rasmi wa kampeni zake atafanya Septemba 20, 2025 nakusisitiza kuwa bado hajaanza rasmi kampeni zake zakuomba kura kwa wananchi wa Hai kumchagua tena kuwa Mbunge wao kwakipindi cha pili.