Mgombea CHADEMA awatolea wenzie bastola

Mgombea CHADEMA awatolea wenzie bastola

JACOB MAKAME

New Member
Joined
Jun 23, 2014
Posts
2
Reaction score
0
Kada wa CHADEMA DAUDI NTINONU leo majira ya saa sita mchana nusura ampige risasi Kiongozi wa Vijana wa Mkoa wa Geita aitwaye Neema Chozaile.

Ntinonu ambaye alikuwa ameongozana na Diwani viti mahalumu wa Nyamagana Bi Neema Mafuma na Elikana Paschael ambae ni mtumishi wa Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Ziwa Magharibi, mala tu baada ya kushuka katika gari la CHADEMA aina ya Ford ranger lenye no CDA 156 katika ofisi za jimbo la geita waliingia ofisini na kuanza kumtupia maneno makali ya uzalilishaji na kisha Ntinonu akatoa Bastola yake yenye rangi nyeusi na kutaka kumfyatua Neema.

Chanzo cha mzozo huo ni mambo ya kusikitisha kwani imebainika kuwa Ntinonu na Peter Makere[mkt Kanda] wanatumiwa na Kada wa CCM aitwaye Mabina ambaye ni ndugu wa Ntinonu na mtia nia waubunge CCM kutengeneza mtandao Jambo ambalo Kamanda Mawazo[mkt mkoa] na Viongozi wa Jimbo la geita akiwemo Rogers na Neema CHOZAIRE wamekuwa wakilipinga

========================================

attachment.php

Freeman Mbowe

Mmoja wa wagombea kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anadaiwa kuwatishia wanachama wenzake kwa bastola baada ya kuibuka makundi yanayohasimiana ndani ya chama hicho.

Tukio hilo linadaiwa kutokea juzi katika kitongoji cha Mkoani kwenye viwanja vya ofisi ya serikali ya mtaa, muda mfupi kabla ya uchaguzi wa uongozi kata ya Kalangalala mjini.

Akithibitisha taarifa hiyo jana, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Peter Kakamba, alimtaja anayedaiwa kuwatishia wenzake kuwa ni Daud Ntinonu.

Walalamikaji katika tukio hilo ni Neema Chozaire (25), Elikana Gideon (30) na Duba Jackson (35).

Walalamikaji hao wamefungua jalada namba GE/RB/5301/2014 la kutishiwa na bastola. ''Ni kweli taarifa ipo na tayari uchunguzi umeanza wa kumtafuta mtuhumiwa…tukimpata tutamhoji na upelelezi ukikamilika tutawasilisha jalada kwa mwanasheria mkuu wa serikali, hilo ndilo jukumu letu," alisema Kakamba.

Hata hivyo, alisema bastola inayodaiwa kutumika itafahamika baada ya upelelezi kukamilika.

Awali akizungumzia madai hayo, Chozaire alisema tukio hilo lilitokea juzi kati ya saa 5:30 asubuhi katika mtaa wa Mkoani, baada ya kutokea kutoelewana kati yake na mtuhumiwa pamoja na wapambe wake kwa kutomuunga mkono.

"Wakati watu walipojitokeza kuamua ugomvi, Ntinonu alitoa bastola yake na kunielekeza kichwani, lakini baadhi ya watu waliingilia kati kumzuia," alisema Chozaire.

Chozaire ambaye ni Mratibu wa Baraza la Vijana mkoa wa Geita (Bavicha), alikiri kuwapo makundi yanayolumbana ndani ya Chadema akihofiwa ni mamluki baada ya kuhamia chama hicho akitokea CCM.

Akizungumzia tuhuma hizo, Ntononu, aliyewahi kuwa mwenyekiti wa CCM wilaya ya Geita kabla ya kuhamia Chadema, alikanusha tuhuma hizo.

Malumbano ndani ya chama hicho mkoani hapa, yamechukua sura mpya baada ya uongozi wa kanda kutoa tamko la kumvua uongozi aliyekuwa katibu wake wa wilaya, Rogers Luhega, aliyewania ubunge jimbo la Geita 2010.

CHANZO: NIPASHE
 
uongo mtupu.. Hiyo yote ni mipango miovu ya ALFONCE MAWAZO.. Mawazo anawafitinisha wana geita ili apate nafasi ya kugombea ubunge.. Mawazo acha kujisumbua ubunge utausikia redion tu
 
attachment.php

Freeman Mbowe

Na Renatus Masuguliko

16th August 2014

Attachments

  • Mbowe.jpeg
    Mbowe.jpeg
    7.5 KB · Views: 6,159
Watanzania tusipokuwa makini na Chadema tutakuja kujuta uchaguzi wa wenyewe lakini wanataka kutoana roho je wakishachukuwa dola wapinzani wao wataishi vipi.
 
uchaguzi wa uongozi wa kata ni hivyo 🙁 tatizo la watu kutaka kuongoza kabla hawajaweza kujiongoza wenyewe.
 
Watanzania tusipokuwa makini na Chadema tutakuja kujuta uchaguzi wa wenyewe lakini wanataka kutoana roho je wakishachukuwa dola wapinzani wao wataishi vipi.
siyo tatizo la chadema ni tatizo ilo ni tatizo la mtu binafsi na matatizo yako na watu wa kila chama, chadema inaweza kuwa na matatizo lakini sio ilo mkuu.
 
Siwezi kushangaa ndiyo tabia za wafuasi wa Chadema.
 
Hiyo picha ya mbowe ina uhusiano gani na hiyo habari yako?umeshakunywa viroba ?
 
Acheni hizo wanatumiwa na mtandao wa CCM fanyeni yenu nyinyi muwekewe mtandao watu wenyewe hamtishi kama njaa na wepesi kama pamba
 
Mawazo kwanini alifukuzwa Arusha ?kwanini anang'ang' ania Geita ??
 
uongo mtupu.. Hiyo yote ni mipango miovu ya ALFONCE MAWAZO.. Mawazo anawafitinisha wana geita ili apate nafasi ya kugombea ubunge.. Mawazo acha kujisumbua ubunge utausikia redion tu

mkuu,alphonce mawazo bado ana kesi mahakamani ya kubaka mwanafunzi,tangu amekuja huku mwanza ameharibu chadema mwanza kote anatakiwa achukuliwe hatua kali na mbowe
 
Baada ya uchaguzi wa 2010 kanda ya ziwa tulitumia nguvu nyingi kukijenga chama kahama, geita, sengerema, nzega na kwingineko cha ajabu miezi ya karibuni wamejiingiza mamluki wengi tuu toka Kwa ma-ccm na kuanza kusambaratisha harakati na misingi yote tuliojenga maeneo mengi toka 2010, ila hatutakata tamaa na tutapambana tuu adi kieleweke
 
Kaangalie kwanza hali za maisha ya ndugu zako mkoa ndiyo utoe kauli hiyo.miaka 50 ya uhuru na hamna kitu
 
Back
Top Bottom