Mgombea CCM aahidi makubwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgombea CCM aahidi makubwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 30, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  [h=2][/h]JUMAMOSI, SEPTEMBA 29, 2012 08:45 NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

  MGOMBEA wa nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Sango Kasera, amesema anaamini ana sifa za kuitumia nafasi hiyo, huku akiwataka wajumbe wa UVCCM kumuunga mkono.

  Kasera ambaye alikuwa anawania nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, alisema, hatua ya kukatwa jina lake katika kuwania nafasi hiyo na kupata nafasi ya kugombea nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kupitia UVCCM, ni mchakato wa kawaida ndani ya CCM, hasa inapotokea idadi ya wagombea kuwa zaidi ya mmoja.

  Akizungumza na MTANZANIA jijini Dar es Salaam jana, Kasera alisema kwa kuwa CCM ndiyo inayoongoza Serikali ni wazi Halmashauri Kuu ya CCM itakapokuwa na wajumbe mahiri kama yeye, itaweza kumudu na kupigania maslahi ya Watanzania kwa vitendo.

  “Agenda kubwa zinazoyakabili maisha ya Watanzania, ni pamoja na vijana kukosa ajira na akina mama kuwa na mazingira magumu katika kupata huduma za afya na utunzaji wa familia.

  “Mbali na hayo, pia wanaume wanakabiliana na hali ya mdororo wa uchumi, ambao unaathiri maisha ya watu wengi katika dunia ya sasa.

  “Kwa maana hiyo, nitakapochaguliwa kuwa mjumbe wa NEC kama ninavyogombea, nitahakikisha ninakuwa daraja huru la kusaidia kusukuma agenda zinazolenga kuiamsha Serikali kuhusu namna njema ya kujenga nchi yetu.

  “Sambamba na kuhamasisha chama chetu kubakia kuwa chama bora kwa maslahi ya Watanzania, ninatambua kuwa, jukumu la mjumbe wa NEC pamoja na mambo mengine ni kuifahamisha, kuitaarifu na kuieleza Serikali juu ya hali ya maisha ya wananchi, sambamba na mtazamo wao kwa mantiki ya kukiendeleza na kukidumisha chama chetu.

  “Kwa bahati nzuri, nina muda wa kutosha kutumikia nafasi hii na hili nalisema kwa kuwa nina mapenzi ya dhati kwa chama chetu na ninaamini kuwa, bila uwepo wa CCM madhubuti nchi hii itayumba.

  “Sikushinikizwa na yeyote kuomba nafasi hii na wala sina agenda zaidi ya kukisaidia chama chetu, ili kibakie katika duru za kuongoza Serikali ya nchi yetu.

  “Kwa kuwa mimi ni kijana makini na wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Taifa wananijua vizuri, ninawaomba kwa heshima kubwa kuwekeza kura zao kwangu, ili niwalipe utumishi uliotukuka,” alisema Kasera.

  Mgombea huyo wa NEC, aliushukuru uongozi wa CCM Taifa, pamoja na viongozi na wanachama wote nchini kwa kumpa nguvu wakati wote hasa katika kuwania nafasi hiyo.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Sema tu kinakuuma kukatwa kuwa Makamu Mwenyekiti UVCCM
   
 3. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [TABLE="class: MsoNormalTable"]
  [TR]
  [TD]
  [FONT=&quot]TAARIFA YA NDG. SANGO KASERA MGOMBEA NAFASI YA NEC-TAIFA KUPITIA UVCCM KWA VYOMBO VYA HABARI[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]Ndugu wana habari;[/FONT] [FONT=&quot]Wanachama wa CCM;[/FONT] [FONT=&quot]Makomredi wanachama wa UVCCM;[/FONT] [FONT=&quot]Watanzania wenzangu.[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]Natumia Nafasi hii kutoa heshima zangu kwenu kwa kazi kubwa mnayoifanya kila siku katika kujenga taifa letu na kuhakikisha kuwa Tanzania inabakia nchi ya mfano katika dunia. Natumia nafasi hii pia kukuombeni mpokee taarifa yangu kwenu ikiwa na lengo moja kubwa, kuwashukuru kwa majitoleo yenu, kwa kuipenda nchi yetu na kwa namna mnavyoenzi umoja na mshikamano baina yetu. Nawashukuru kwa kulinda amani na kuibakiza nchi yetu katika usalama.[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]Ndugu wana habari;[/FONT] [FONT=&quot]Agosti 3, mwaka huu nilichukua fomu za kuwania nafasi mbili katika jumuiya ya Vijana wa CCM. Moja, niliomba nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa UVCCM na pia nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kupitia nafasi za Vijana. Kwa namna ya pekee kabisa naomba kutumia nafasi hii kuwashukuru Viongozi wa CCM ambao wameshiriki zoezi zima la kuchuja majina ya wagombea na kisha kubakiza jina langu katika nafasi ya kuwania Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa. Kama nilivyoandika katika taarifa yangu kwa waandishi wa Habari baada ya kuchukua fomu za kuwania nafasi hizo, nilibainisha wazi kuwa mimi ni kijana mwenye uwezo, fikra na mtazamo unaolenga kuisaidia Tanzania kuendelea kuwa taifa linalothamini utu na watu, linaloheshimu utoaji fursa sawa kwa wananchi wote na linalothamini ukuzaji wa fursa za maendeleo kwa wananchi maskini.[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]Kwa kutambua ukweli huo, nakishukuru chama chetu kwa kuniamini na kunipa nafasi ya kuwa mgombea wa nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu. Nafasi hii ni kubwa na inatoa fursa kwa wajumbe watakaochaguliwa pamoja nami, kubadili muelekeo na njia ya namna ya kuiendeleza nchi yetu. Halmashauri Kuu ya chama chetu ni sawa na Bunge la Chama. Kwa kuwa CCM ndiyo inayoongoza serikali, ni wazi kuwa Halmashauri Kuu ya CCM itakapokuwa na wajumbe kama mimi, tutamudu kusukuma kwa vitendo agenda kubwa zinazoyakabili maisha ya watanzania na hasa vijana ambao kwa sasa wanakabiliwa na tatizo kubwa la ajira, akina mama ambao wanakabiliwa mazingira magumu katika kupata huduma za afya na utunzaji wa familia, watoto ambao wanataka kuona Tanzania inakuwa nchi yenye kuweza kutimiza ndoto zao na akina baba ambao wanakabiliana na hali ya mdororo wa uchumi ambao unaathiri maisha ya watu wengi katika dunia ya sasa.[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]Nitakapochaguliwa kuwa mjumbe wa NEC, jambo ambalo nina hakika kabisa kuwa wajumbe wa Baraza la UVCCM Taifa watalifanya, nitahakikisha ninakuwa daraja huru la kusaidia kusukuma agenda zinazolenga kuiamsha serikali kuhusu namna njema ya kujenga nchi inayotambua matakwa ya wananchi, sambamba na kuhamasisha chama chetu kubakia kuwa chama bora kwa maslahi ya Watanzania. Natambua kuwa jukumu la mjumbe wa NEC pamoja mambo mengine ni kuifahamisha, kuitaarifu na kuieleza serikali juu ya hali ya maisha ya wananchi sambamba na mtazamo wao kwa mankiti ya kukiendeleza na kukidumisha chama chetu. Natambua pia kuwa jukumu linguine ni hili la kuhamaisha siku zote nchi yetu ipate maendeleo huku ikibakia katika hali ya amani na utuliuvu.[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]Ndugu wanahabari;[/FONT] [FONT=&quot]Jina langu halikupitishwa kwa bahati hata kidogo. Ninazo sifa zinazostahili kuwa mjumbe bora na makini wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa. Ninao muda wa kutosha kutumikia nafasi hii na hili nalisema kwa kuwa nina mapenzi ya dhati kwa chama chetu na ninaamini kuwa bila uwepo wa CCM madhubuti, nchi hii itayumba. Historia yangu na maisha yangu yanaonyesha njia ya namna kijana wa Kitanzania anavyotakiwa kuwa na kuishi katika nchi hii. Ninaishi maisha ya kawaida wanayoishi vijana wengi wa Tanzania na pia popote nilipopata nafasi ya kufanya kazi, nimefanya kazi kwa kutanguliza utumishi uliotukuka. [/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]Nikufahamisheni pia kuwa, sikushinikizwa na yeyote kuomba nafasi hii na wala sina agenda zaidi ya kukisaidia chama chetu kibakie katika duru za kuongoza serikali na nchi yetu. Kwa kuwa mimi ni kijana makini wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Taifa ninawaomba kwa heshima kubwa kuwekeza kura zetu kwangu ili niwalipe utumishi uliotukuka. Ili kuijenga Tanzania ya leo, tambueni mnao wajibu wa kuchagua viongozi makini kama mimi ili vijana wenzetu ambao hawana nafasi katika vyombo vya maamuzi wapate uwakilishi unaogusa maisha yao.[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]Mwisho naomba nitumie nafasi hii kuushukuru uongozi wa CCM Taifa pamoja na viongozi na wanachama wote wa CCM nchini. Niwashukuru Watanzania wenzangu. Ndugu wana Habari na wote ambao nimeshirikiana nao katika harakati hizi za kutaka kuzidi kuiboresha Tanzania yetu. Naamini ushindi watakaonipatia vijana wa CCM ni ushindi wetu sote. Uchaguzi huu si kwa maslahi yangu bali ya vijana wote wa Tanzania. Nawashukuru sana kwa kupokea taarifa hii.[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]Mungu Ibariki Tanzania[/FONT] [FONT=&quot]Kidumu Chama cha Mapinduzi[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]Imetolewa na: Sango Kasera -Mwenyekiti wa UVCCM wilaya RORYA[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
Loading...