Mgombea avamiwa na kucharazwa mapanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgombea avamiwa na kucharazwa mapanga

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MziziMkavu, Sep 12, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Mgombea udiwani Kata ya Kirumba, jijini Mwanza, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Novatus Manoko, amenusurika kufa baada ya kuvamiwa na kukatwa mapanga na watu wasiojulikana.
  Katika tukio hilo, Manoko alijeruhiwa sehemu za kichwani.
  Kamanda wa Polisi wa Mkoani wa Mwanza, Simon Sirro, alithibitisha kuwepo taarifa za tukio hilo, lakini alitaka kupewa muda kabla ya kufafanua undani wake.
  "Nimesikia tu kuhusu tukio hilo lakini bado nalifuatilia, nitafute baadaye naweza kuwa nimelipata vizuri," alisema Sirro alipozungumza na NIPASHE kwa njia ya simu
  Hata hivyo tukio hilo linahusishwa na mbinu chafu za kisiasa zenye lengo la kuwadhoofisha wagombea kupitia vyama vya upinzani ndani ya kata hiyo.
  Habari zilizolifikia NIPASHE kwa njia ya simu jana zilidai kuwa, Manoko ambaye pia ni Mwenyekiti wa soko la kimataifa la Mwaloni lililopo Kirumba jijini hapa, alivamiwa saa nne za usiku juzi, wakati akitoka kwenye vikao vya ndani vya Chadema.
  Katika tukio hilo, Manoko aliporwa simu mbili za mkononi na nyaraka kadhaa alizokuwa nazo.
  Ilidaiwa kuwa mgombea huyo alivamiwa na kundi la watu baada ya kufika kwenye geti la nyumba yake iliyopo Kirumba.
  Habari zinadai kuwa watu hao walimzingira Manoko ambaye wakati huo alikuwa kwenye gari lake na kumshambulia kwa mapanga.
  Manoko alikimbizwa katika hospitali ya serikali ya mkoa wa Mwanza, Sekou-Toure kwa matibabu.
  "Sisi wakazi wa Kirumba tunaamini hizi ni siasa tu kwa sababu jamaa anakubalika mno," alisema mmoja wa wakazi wa kata hiyo ambaye hata hivyo hakutaka kutajwa jina lake.
  NIPASHE ilijaribu kumtafuta Manoko ili aweze kuthibitisha juu ya tukio hilo, bila mafanikio kwa vile simu zake hazikupatikana.
  Hili ni tukio la kwanza kutokea Jijini Mwanza kwa mgombea wa chama cha siasa kuvamiwa na kukatwa mapanga tangu kuanza kwa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu.
  Pia, Katibu Mkuu wa Chadema mkoa wa Mwanza, Wilson Mushumbusi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
  Akizungumza na NIPASHE kwa njia simu kutoka nyumbani kwa Manoko, Mushumbusi alidai kwamba dalili zinaonyesha kuwepo sababu za kisiasa.
  Alisema baada ya tukio hilo, Manoko alikwenda hospitali alipopata matibabu na baadaye kuruhusiwa kujerea nyumbani.  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...