Mgogoro wa Zanzibar Kumuumbua Kikwete?

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
HATIMAYE, Dk. Ali Mohamed Shein ametangazwa kuwa “mshindi wa urais” Zanzibar. Aliapishwa Alhamisi iliyopita, anaandika Mwandishi Wetu.

Urais wa Dk. Shein unatokana na kilichoitwa “uchaguzi wa marudio” Visiwani uliofanyika 20 Machi 2016.

Uchaguzi wa marudio Zanzibar ni tunda la Jecha Salim Jecha, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), aliyefuta uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana kwa madai kuwa “kulikuwa na kasoro nyingi.”

Huu ni uchaguzi ambao waangalizi wa ndani na nje walisema “ulikuwa huru na wa haki” na ambamo Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, alidai alikuwa amechaguliwa “kwa kishindo.”

Ripoti za waangalizi zinazoonyesha uchaguzi wa 25 Oktoba, Visiwani ulikuwa huru na haki, ni pamoja na ile iliyotolewa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya (SADC) na Umoja wa Africa (AU).

Aidha, uchaguzi wa marudio umefanyika bila kushirikisha chama kikuu cha upinzani Visiwani (CUF).

Sasa hapa kuna maswali muhimu ya kujiuliza. Je, kufanyika kwa uchaguzi wa marudio kulikohitimishwa na kumtangaza Dk. Shein kuwa mshindi, kutakuwa mwisho wa migogoro ya kisiasa Visiwani?

Hatua ya CUF kususia uchaguzi huo, inaweza kuwa mwanzo mpya ya mifakarano – kwa sababu za msingi kwamba sehemu kubwa ya jamii imebaguliwa?

Kipi kitatokea katika miaka mitano kuanzia leo; na nani atawajibika iwapo itazuka minyukano ya kisiasa na hata mapigano? Tujadili.

Kwanza, hatua ya kufuta uchaguzi na matokeo yake yote, haiwezi kuwa mwisho wa mgogoro wa kisiasa Visiwani. Huu tayari ni mwanzo wa mifarakano, minyukano, uhasama, kutoaminiana na uvunjifu wa sheria.

Kitendo cha kufuta matokeo ya uchaguzi halali, huru na haki, kitaishia kuibuka upya kwa vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu na ukiukwaji wa utawala bora.

Kufuta uchaguzi, kinyume cha taratibu, kunairudisha Zanzibar, katika giza la fikra na utawala wa mabavu.

Kilichotendeka kinajenga msingi mbovu kwa watu kutaka watii “batili,” wapinge haki na kufunika demokrasia kwa blanketi. Hili siyo rahisi kukubalika kwa wote.

Kufuta uchaguzi, bila kutafuta suluhu ya kilichosababisha hatua hiyo kutendeka, kisha ukaitishwa uchaguzi mwingine katikati ya giza, ni kuficha moto kwenye majani makavu. Yatalipuka.

Jecha ameitishia uchaguzi mpya kutoka mafichoni na bila kueleza kilichosababisha uchaguzi wa awali kufutwa.

Hakufanya mikutano na vyama vilivyoshiriki uchaguzi wa 25 Oktoba na vilivyoshiriki uchaguzi wa marudio; hakukutana na wajumbe wenzake ndani ya ZEC wala vyombo vya habari na waangalizi wa uchaguzi kutoka ndani na nje ya nchi.

Aliyekuwa makamu mwenyekiti wa ZEC, Jaji Abdulhakim Ameir Issa, alimaliza kazi yake, 28 Oktoba 2015. Alikuwa anakaribia kutangaza mshindi halali wa uchaguzi.

Lakini hakufanya hivyo. Jaji Ameir anasimulia alivyotekwa na kushikiliwa kwa saa nane makao makuu ya polisi Zanzibar.

Ilikuwa muda mfupi baada ya kuanza majumuisho ya mwisho ya matokeo ya kura katika majimbo 54. Kazi hii ya majumuisho, ilifanyika katika hoteli ya Bwawani, Unguja.

Jaji Ameir anasema, alitekwa muda mfupi kabla ya Jecha kutangaza kufuta uchaguzi. Hivyo, uchaguzi hauwezi kuwa suluhu kwa kuwa Jaji Ameir alikamatwa kama mhuni.

Aidha, hatua ya Jecha ya kufuta matokeo ya uchaguzi na uchaguzi wote na kisha kuitisha uchaguzi mpya, haiwezi kuwa suluhu ya migogoro Visiwani.

Hii ni kwa sababu, uchaguzi wa marudio umefanyika bila kupata majibu mwafaka ya uhalali wa uamuzi wa Jecha kufuta uchaguzi wa 25 Oktoba.

Uchaguzi wa marudio hauwezi kuwa suluhu kwa kuwa Jecha na ZEC wamepoteza sifa ya kusimamia uchaguzi; pande zote zinazovutana kwenye mgogoro zimeshindwa kukubaliana juu ya uchaguzi mpya.

Uamuzi wa kurejea uchaguzi hauwezi kuwa suluhu kwa kuwa mvutano wa uhalali wa urais wa Dk. Shein, haukupatiwa ufumbuzi.

Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, rais anaweza kuendelea katika nafasi yake katika kipindi cha miezi sita, ikiwa Jamhuri ya Muungano itaingia katika vita.

Zanzibar haikuingia katika vita. Lakini Dk. Shein aliendelea kubaki madarakani. Aliongoza nchi bila Baraza la Wawakilishi. Bila baraza la mawaziri. Baraza la Wawakilishi lilivunjwa Julai mwaka jana.

Pili, hii siyo mara ya kwanza kuibuka mgogoro wa kisiasa Zanzibar. Waweza kuwa siyo wa mwisho pia. Kuna migogoro mingi imeibuka. Mingine imetatuliwa na mingine imeshindikana.

Hata hivyo, mgogoro ambao bado unakumbukwa na wengi, ni ule wa mwaka 2000. Machafuko makubwa ya kisiasa, vurugu na mauaji yalitokea 26 na 27 Januari 2001 huko Unguja na Pemba.

Taarifa huru zinasema, watu zaidi ya 40 walifariki dunia katika machafuko hayo. Wengine mamia waliomba hifadhi ya ukimbizi nchini Kenya. Taifa ambalo lilikuwa kimbilio la wakimbizi, kwa mara ya kwanza, likazalisha wakimbizi wake.

Lakini mifarakano ya kisiasa Visiwani imeshindwa kupatiwa ufumbuzi kwa kuwa walioko madarakani hawataki kusikia sauti za busara kutoka nje ya duara la utawala. Wamejifanya wapofu. Hoja iliyoko mbele yao, siyo jinsi ya kujiepusha na migogoro, bali kutawala katika mazingira yoyote yale.

Ilani zote za uchaguzi za CCM, hakuna ambako kumezungumzia utatuzi wa migogoro ya Zanzibar. Hakuna!

Maafikiano yaliyoasisiwa na rais mstaafu, Amani Abeid Karume – kushirikisha wapinzani wake katika serikali – hayakuonekana muhimu kwa washirika wenzake ndani ya Muungano na Zanzibar kwenyewe.

Tatu, hatua ya Jecha kukubali kutumika kufuta matokeo na kuitisha uchaguzi mpya, imeibua mgogoro mwingine mkubwa wa kikatiba Zanzibar na Bara.

Kwa mfano, Katiba ya Zanzibar, toleo la mwaka 2010, linatambua kuwapo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Kwa matokeo yaliyotangazwa, bila shaka serikali itakayoundwa, siyo ile ya umoja wa kitaifa, hata kama yaweza kupewa jina hilo.

Kutenda kinyume na katiba ni kutaka kuingiza nchi katika machafuko. Ni kuvunja taratibu za nchi na kusigina demokrasia na utawala wa sheria.

Ndani ya Bunge la Muungano, ambako Baraza la Wawakilishi (BWZ) linatuma wawakilishi watano, takwa hilo la kikatiba litashindikana kutimiza.

Hii ni kwa sababu, katiba ya Zanzibar inaelekeza kuwa miongoni mwa wawakilishi hao watano, sharti wawili watoke upinzani.

Wakiamua kuwaleta – kutoka vyama vingine mamluki – kwa kuwavisha kofia ya upinzani, bado watakuwa siyo wawakilishi wa wananchi. Ni CCM iliyojivika kilemba cha upinzani.

Nne, mgogoro mpya ulioibuka Zanzibar, “utamvua nguo” Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, kuliko utakavyomuaibisha rais wa sasa, John Pombe Magufuli.

Kikwete anaijua vema Zanzibar kuliko Magufuli. Aliwahi kufanya kazi Zanzibar. Ameishi Zanzibar na amekuwa ndani ya chama chake – Chama Cha Mapinduzi – kwa miaka mingi, ukilinganisha na mrithi wake.

Hili amelithibitisha katika hotuba yake ya kwanza mbele ya Bunge, tarehe 30 Desemba 2005. Alikiri “Zanzibar kuna mpasuko wa kisiasa.”

Alitamka kwa sauti ya ukakamavu kuwa atafanya kila awezalo kumaliza mpasuko wa Zanzibar. Hakuishia kusema tu. Aliunda kamati ya maridhiano iliyoshirikisha chama chake (CCM) na CUF, ili kutafuta njia ya kumaliza mgogoro.

Vikao kadhaa vilifanyika, tena kwa maelekezo yake kwa lengo la kutafuta suluhu. Mazungumzo yaliyochukua miezi 14 yalimalizika; ikawa sasa kazi ya vikao vya juu vya vyama hivyo kuidhinisha kile kilichokubaliwa.

Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, uliofanyika Butiama mkoani Mara, tarehe 2 na 3 Machi 2008, ulimalizika bila makubaliano. Ni baada ya CCM kuibua hoja mpya ya kutaka kufanyika kura ya maoni.

Alhamisi, 21 Agosti 2008, Kikwete aliliambia Bunge mjini Dodoma, kwamba CCM na CUF, haviaminiani. Alikuwa akielezea mazungumzo kati ya vyama hivyo viwili yenye shabaha ya kuleta mwafaka mpya katika kile alichoita “kumaliza mpasuko Zanzibar.”

Alisema yeye, Rais Kikwete, ni mtu mzima; anajua kuna tatizo; anatafuta njia mwafaka ya kuhakikisha anafika anakokwenda.

“Sijakata tamaa. Najua lipo tatizo kubwa la kutoaminiana. Tutaangalia kama kura ya maoni au makubaliano ya vyama yanatosha,” alisema Kikwete.

Lakini alikuwa ni kada wa CCM na muasisi wa Afro-Shirazi Party (ASP), Hassan Nassor Moyo, aliyemaliza mvutano Visiwani. Aliwakutanisha Maalim Seif na Rais Amani Karume. Serikali mpya ikaundwa. Utulivu ukapatikana.

Lakini ni Kikwete huyohuyo anayetuhumiwa kuchochea mgogoro huu wa sasa; na au kuunyamazia. Anatuhumiwa kuamuru vyombo vya usalama, kuzuia kutangazwa mshindi halali wa uchaguzi wa 25 Oktoba.

Haikutarajiwa mtu ambaye miaka 10 iliyopita, amekiri bungeni kuwa “Zanzibar kuna tatizo na linahitaji ufumbuzi wa haraka kwa manufaa ya nchi na wananchi wake,” ndiye huyohuyo aliyeshindwa kutambua tatizo kwa sababu ya kutaka kulazimisha ushindi kwa chama chake.

Kikwete anafahamu kuwa ni rahisi kwa CUF kushirikiana na CCM kuliko CCM kukubali kushirikiana na CUF. Hivyo ndivyo ilivyotokea pale CUF ilipoonekana kuelekea kushinda uchaguzi.

Hii ni kwa sababu, chama kilichozeekea madarakani, hakiko tayari hata kuona chama kingine kikiunda utawala kwa ngazi ya halmashauri, jiji na manipaa ambako kimeshindwa.

Panahitajika ukomavu kisiasa – Bara na Visiwani. Kwamba mtu yumo katika chama kilichoko madarakani haina maana kwamba ndiye mwenye akili nyingi na hekima.

Wananchi wamechoka chokochoko na malumbano ya mwaka hadi mwaka. Wasilazimishwe na watu wanaong’ang’ania madaraka.

Ni vema ikaeleweka kwamba watu wanaothamini akili nje ya vyama vyao, huchota akili hizo na kuzitumia ndani ya serikali zao na kwa pamoja kutumikia wananchi wote bila ubaguzi.
 
Uchaguzi umefanyika tusonge Mbele. Mapovu ya nini?
 
Mzee wa msoga sasa hivi anatalii duniani, anafanya kazi za usuluhishi, zanzibar hausiki, hivi wakiamua kumtuma zanzibar kuutatua mgogoro wa zanzibar itakuwaje?
 
Ni wakati sasa wa kuweka ushabiki wa vyama vyetu pembeni tuongee ukweli.

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
 
Ali Karume ameshasema cuf waishie kugombea udiwani na ubunge urais ni wa ccm, nyinyi watu ni wagumu kuelewa
 
Back
Top Bottom