Mgogoro wa TTCL na Bharti Airtel: Airtel yauza Minara 1,350 kinyemela

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,575
Tanzania is the ninth African country where Bharti has executed such a deal since buying Kuwait-based Zain’s Africa assets across 17 countries, in the continent. Photo: Reuters


New Delhi: Bharti Airtel Ltd, the world’s third largest communications services provider, has signed an agreement with American Tower Corp., to sell approximately 1,350 towers in Tanzania.

“Under the agreement, American Tower may acquire up to approximately 100 additional sites currently in development for an additional consideration,” Bharti said in a statement on Monday. “Airtel will be the anchor tenant on the portfolio under a lease with a 10-year initial term,” the statement added.

This is the ninth African country where Bharti has executed such a deal since buying Kuwait-based Zain’s Africa assets across 17 countries, in the continent.

The deal is valued at around $179 million, according to a statement by American Tower to US stock exchanges. With this, Bharti has raised more than $2 billion from tower sales in Africa.

The deal is expected to be completed by the first half of 2016 and is aimed at improving Bharti’s ability to focus on its core business and help reduce debt, by reducing ongoing capital expenditure on passive infrastructure.

As reported by Mint in October, Bharti concluded the sale of around 8,300 towers in Africa across the continent. Bharti has thus far sold around 2,500 towers to Eaton in four countries, including Ghana, Uganda and Kenya, and another 700 towers in Burkina Faso.

Bharti was earlier in talks with Eaton to sell the Tanzania based telecom towers, but that deal lapsed.

The latest deal takes the number of towers sold to around 10,500, of the around 13,000 towers that the telco owns in the African continent.

On 21 October, Bharti announced that it had signed a total of seven deals to sell its towers for a total of $1.7 billion. Other companies that Bharti has sold its towers include Helios Towers Africa and IHS Holding Ltd.

ATC has also bought Bharti’s towers in Nigeria.

On 14 January, Bharti announced that it had finalised a deal to sell its telecom operations in Burkina Faso and Sierra Leone to France-based telecom operator Orange, for an estimated $900 million.

MADUDU YA KAMPUNI HII YA AMERICAN TOWER CORP.
More sneaky options schemes
Amidst backdating options scandals,
1.American Tower uses another legal tactic for hiding executive compensation - backdoor options filtered through a subsidiary.
By Bethany McLean, Fortune editor-at-large
October 17 2006: 11:06 AM EDT

(Fortune Magazine) -- Just when backdating options seemed like the state-of-the-art method for executives to line their pockets, along comes a crafty yet legal tactic that involves stashing stock grants in the furthest corners of the footnotes: Call them backdoor options.

A primer for firms hit by stock options scandal
As backdating options continues to ensnare corporate officers, a Boston-based company called American Tower has faced questions from the SEC and U.S. Attorney's office over its use of backdating. But backdating isn't the only eyebrow-raising element of their compensation strategies.


How Backdoor Options Work
Deep in American Tower's proxy lurks a sneaky scheme.
1. American Tower sets up a subsidiary.
2. Executives are allowed to purchase stock in the subsidiary.
3. Execs acquire stock through cash and a loan; they also get options to buy more shares.
4. The executives can force AT to buy them out within a certain period of time.
5. AT's purchases net employees millions in profits.
American Tower (Charts) has a market cap of $15 billion and owns the infrastructure, such as towers and rooftop structures, that wireless companies lease. Last May the company announced that a special committee of independent directors was reviewing its option-granting practices; in September, American Tower said it will have to restate more than three years of financial results. But a close look at its filings also reveals that top executives have made tens of millions from stock in subsidiary companies - information you won't see in the compensation table of its proxy statement.

hidden numbers
In the standard table in American Tower's proxy - the one that lists the salaries, bonuses and other compensation for the five highest-paid employees - you see that an executive named Michael Gearon, the company's vice chairman and the president of its international business, has earned $2 million in cash over the past three years and has gotten 665,000 options.

In 1998, Gearon sold Gearon Communications to American Tower and joined the company. He still lives in Atlanta, where his firm was based, and is a part-owner of the Atlanta Hawks. General counsel William Hess earned $1.8 million in cash and got 370,000 options over the past three years.

But in the tables detailing options exercises there's a footnote that says that during 2004, American Tower's Brazil operation, called ATC South America, granted "certain employees," including Gearon and Hess, options to purchase common stock of ATC South America at an exercise price of $1,349 per share. Those separate options were exercised in October 2005.

The footnote says that the "value realized" by Gearon and Hess was approximately $11.5 million and $2.7 million, respectively, and refers you to another section of the proxy called "Related Party Transactions." This section of proxies became notorious in the wake of Enron, because it's where CFO Andy Fastow's infamous partnerships were actually disclosed to investors.

In this section of American Tower's proxy, you learn that in March 2004 Gearon paid $1.2 million for a 1.6 percent stake in ATC South America; in October 2005, American Tower expects to pay him $3.7 million for that stake. Plus, Gearon got options - worth some $11.5 million a year and a half later - to acquire 6.7 percent of ATC South America. (Hess's options allowed him to acquire 1.6 percent of ATC South America.)

And you learn about another entity, ATC Mexico. Back in 2004, Gearon and Hess exercised their "previously disclosed" rights to require American Tower to buy their stakes in that entity. Afterward Gearon collected $36.2 million, much of it in American Tower stock that has since more than tripled.

If you check American Tower's 2005 10-K, you'll learn - in footnote 11 - that Gearon used just $1.7 million of cash plus a $6.7 million loan from American Tower to buy his stake in ATC Mexico.

So Gearon picked up cash and stock worth well over $30 million (a figure that doesn't take into account the stock's recent uptick) in these side deals - payments that aren't reflected in the compensation table in the proxy.

Hess and the others got some $20 million. Why would Gearon get all this additional money for running the international business when his job description is to run the international business? Why isn't this compensation disclosed in the compensation tables?

"It's a matter of judgment on the part of the company and its advisors," says Kenneth Laverriere, a partner at New York law firm Shearman & Sterling. "It's a close call."

James Taiclet, American Tower's CEO, says these agreements were put in place in 2001 when the international business didn't exist, and were done to provide Gearon and his team with the "incentive to take the risk" of building the business. He points out that Brazil and Mexico now account for 13 percent of the company's revenues and says "shareholders have benefited tremendously." He also says the agreements are "very thoroughly disclosed in the appropriate places."

Not that investors seem to care about any of this. American Tower's stock has doubled since 2005. That has helped Gearon, who's sold stock worth $40 million over that time period, grow his fortune even more.

2. American Tower Pays $14M To Settle Backdating Case
By Christine Caulfield

Law360, New York (December 14, 2007, 12:00 AM ET) -- Wireless communication company American Tower Corp. has settled a class action over stock options backdating, agreeing to give its shareholders $14 million to drop the case.
In a statement released Thursday, American Tower said the settlement would resolve all the claims against the company and two of its top executives, if approved by the Massachusetts district court.

The Boston-based company said it would continue to negotiate with its insurers about their contribution to the settlement.

U.S. District Judge Mark L. Wolf stayed the case pending a hearing on the motion for preliminary settlement approval on Feb. 19, 2008.

The action was filed in the Massachusetts court in May 2006 on behalf of shareholders who bought stock in American Tower between Feb.1 and May 24, 2006.

Named as co-defendants in the suit were American Tower chief executive James Taiclet, who allegedly sold 37,5000 shares for an inflated profit of $900,000 on March 13, 2006; and chief financial officer Bradley Singer, who allegedly pocketed $800,000 after exercising his stock options on March 10 last year.

The suit claimed the communications company backdated the stock option grants of the two directors and/or other executives to maximize the stock's profitability.

American Tower allegedly misled its investors when, in numerous proxy statements, it claimed that “the exercise price per share of each option was equal to the fair market value per share of the underlying stock as valued by the Board of Directors on the date of the grant.”

Further, in its annual financial report to the U.S. Securities and Exchange Commission, dated Mar. 15, 2006, the company falsely reported a loss of $0.44 per share and an expense sheet total of $801 million, the complaint alleged.

According to the shareholders, these statements were materially false and misleading because they neglected to mention that the option grants were in fact not made at fair market value or the closing price of the shares on the New York Stock Exchange on the date of the grant.

They also played down the company's expenses and inflated earnings as a result of the improper backdating, said the plaintiffs.

“Initially, even as the wrongful practice of backdating of options grants became public for a number of companies, American Tower made no disclosures to the effect that it too had committed these wrongful practices,” the complaint stated.

It wasn't until May 19, 2006 that the company issued a statement announcing the creation of a special committee of independent directors to conduct an internal investigation into its historical stock options practices.

The company admitted in the statement that, depending on the outcome of that probe, it might need to restate its previous financial reports. It also revealed that the SEC had launched an informal inquiry into the company's options grants.

Four days later American Tower said it had received a subpoena from the U.S. District Attorney for the Eastern District of New York calling for documents in connection to its option grant practices. It also announced a temporary suspension of its stock repurchase program in view of the investigations.

“The company's ultimate destiny is dependent on the integrity of management. In this particular case, the backdating of stock option grants to increase the profitability of the options is a classic example of loss confidence on the part of investors since management is effectively taking from shareholders in order to line their own pockets,” the plaintiffs said.

American Tower was one of scores of companies to face scrutiny by shareholders and regulators over their stock options practices since May last year. The SEC's enforcement division is still actively reviewing the books of dozens of publicly-listed companies, and a number have settled claims of backdating.

The plaintiffs are represented by Adkins, Kelston & Zavez PC, Lovell Stewart Halebian LLP and Bishop & Associates PSC.

The case is John S. Greenebaum et al., v. American Tower Corp et al., case number 06-ca-10933, in the U.S. District Court for the District of Massachusetts.
 
HISA ZETU ZA TTCL ; MINARA HAIMO???????????

JE ILE MINARA YA TTCL NA MIUNDO MBINU WATATUMIA YA TTCL?????
 
Mtendaji-Airtel-na-TTCL-620x308.jpg

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Airtel, Diego Gutierrez (kushoto) akiteta jambo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Kamugisha Kazaura
TTCL yafilisika, yapata hasara ya bil 300, haikopesheki



KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL), ambalo ni shirika kongwe la umma, sasa imefilisika kibiashara kutokana na ubia tata kati ya serikali na wawekezaji wenye mgongano wa kimaslahi katika sekta ya mawasiliano. Anaandika Deusdedit Kahangwa … (endelea).

Aidha, ubovu wa menejimenti, ubadhirifu wa fedha za umma, wafanyakazi waliokatishwa tamaa, ukosefu wa mtaji, madeni sugu, na mitambo iliyopitwa na wakati ndivyo vinavyochangia kuliua.

Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura, kampuni hii inachungulia kaburi kwa sababu imekuwa ikipata hasara mwaka hata mwaka kiasi cha kufikia hadhi ya “kutokopesheka.”

Dk. Kazaura ameiambia MwanahalisiOnline kwamba kampuni ya TTCL imepata “hasara kubwa ya kiasi cha Sh. 335 bilioni mpaka kufikia mwaka 2013” jambo ambalo limeifanya “kushindwa kukopesheka huku ikibaki na mtaji hasi wa Sh. 88 bilioni.”

Kwa mujibu wa Dk. Kazaura, “kwa sasa Kampuni ya TTCL ni mufilisi,” hatua ambayo inatokana na “mbia mwenye hisa za asilimia 35, kutofanya uwekezaji mkubwa tangu aingie katika ubia na serikali mwaka 2001.”

Dk. Kazaura aliyasema hayo mjini Dodoma mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi.

Nae Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, amesema mchakato wa kuondoka kwa Kampuni ya Airtel kutoka TTCL “uko katika hatua za mwisho.” Ameeleza kuwa tayari “makubaliano ya bei” ya hisa zinazodaiwa kumilikiwa na Airtel katika TTCL yamefikiwa “katika kikao cha majadiliano kilichofanyika tarehe 20 Novemba 2014.

Akielezea majadiliano yalivyokuwa, Profesa. Mbarawa amesema Kampuni ya Airtel iliafiki kuachia hisa inazomiliki ndani ya TTCL” na kisha Serikali kukubali “kuzinunua hisa hizo kwa Sh. bilioni 14.9” za Tanzania.

Tayari “Baraza la Mawaziri liliidhinisha Serikali kununua hisa hizo” kwa mashrati kwamba malipo hayo yafanywe “baada ya taratibu za kisheria kukamilika” ili hatimaye “Serikali iweze kuimiliki TTCL kwa asilimia 100,” aliongeza Profesa Mbarawa.

Profesa Mbarawa aliyatamka hayo wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya matumizi ya bajeti ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha wa 2015/16, bungeni Dodoma hivi karibuni.

Kufuatia kuibuka kwa taarifa za malipo haya, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kupitia kwa msemaji wake wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, (CUF) Mohamed Habib Mnyaa, imehoji umakini wa serikali na kuitaka itekeleze mambo kadhaa.

·Kwanza, serikali imetakiwa kufafanua matakwa ya mkataba wa awali kati ya Serikali na Kampuni ya MSI na hatua za utekelezaji wa makubaliano ya mkataba huo mpaka sasa.

·Kueleza iwapo mkataba huo ulikuwa unairuhusu kampuni ya MSI kuuza hisa zake kwa makampuni mengine yaliyofuata kama vile Celtel, Zain na sasa Airtel.

·Kutoa ufafanuzi kuhusu uhalali wa maamuzi yake ya kuilipa kampuni ya Airtel Sh. 14 bilioni.

Wadau wapinga malipo ya bilioni 14 kwa Airtel

Wakati mvutano huo ukiendelea kushika kasi wadau mbalimbali wamepinga hatua ya serikali kulipa mabilioni ya shilingi hayo kwa kampuni ya Airtel.

Kwa mfano, kati ya tarehe 16-18 Juni mwaka huu, wadau mbalimbali walikutana mjini Dodoma na Kamati ya Bunge ya Miundombinu kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na mgogoro huu wa TTCL.

Pia, wadau kadhaa waliozungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa majina walisema ni makosa kwa serikali kuilipa Airtel wakati haijawahi kuwekeza hata senti moja katika TTCL.

Kwa mfano, mdau mmoja ambaye ni mhandisi wa muda mrefu ndani ya TTCL, aliyejieleza kwa kirefu, lakini kwa masharti ya kutotajwa, akisema:

“Ndani ya TTCL kuna tabaka la ngazi za mishahara ya watawala (TTCL1 hadi TTCL3), kwa upande mmoja, na tabaka la ngazi za mishahara ya makabwela (TTCL4 hadi TTCL10), kwa upande mwingine.

“Wafanyakazi wengi tulirundikwa katika tabaka la makabwela na tukapewa cheo cha ‘Team member’ lakini bila kuzingatia elimu, weledi, wala uzoefu wetu.

“Katika zoezi la mabadiliko hayo, Menejimenti iliongeza mishahara na kuboresha maslahi ya wafanyakazi wote walio katika tabaka la mishahara ya watawala lakini ikatutelekeza sisi wafanyakazi tulio katika tabaka la mishahara ya makabwela.

“Hata hivyo, sisi wafanyakazi wa ngazi za kawaida ambao hatukuboreshewa malipo ndio wazalishaji wakuu ndani ya TTCL.

“Kwa hiyo, sasa tunashangaa kuona kwamba sisi watu ambao tulisahaulika siku nyingi hatukumbukwi lakini wakati huo kampui ya Airtel ambayo haijawahi kuwekeza hata shilingi inatengewa mabilioni.

“Hivyo basi, kama serikali wanazo fedha za kichezea kiasi hicho waanza na maboresho ya maslahi ya wafanyakazi kabla ya jambo jingine lolote.”

Nae Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni chini ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Tekinolojia, Habib Mnyaa alipinga malipo hayo.

Amesema kampuni ya Airtel hawapaswi kulipwa chochote kwa kuwa, mwekezaji huyu pamoja na watangulizi wake waliahidi kujenga “njia 800,100 za simu lakini wakashindwa, na badala yake hata njia 270,000 walizozikuta zimepungua kufikia njia 158,000 tu.”

“Kwa vile Airtel ilianzishwa kwa fedha, leseni na raslimali za TTCL, na mpaka sasa inatumia miundombinu ya TTCL kama vile jenereta, majengo, na viwanja, basi haipaswi kulipwa hata senti,” alisisitiza Mnyaa ambaye ni mbunge wa jimbo la Mkanyageni, Kusini Pemba.

Aliendelea, “Tukumbuke kwamba mwaka 1998 Kampuni ya Simu ilikuwa na mawasiliano ya simu katika makao makuu ya takribani wilaya zote nchini. Hivyo, tulitarajia kwamba kwa mwaka 2015 kampuni hii ingekuwa imefikisha mawasiliano hayo katika kila Kata ya Tanzania, lakini wapi. Huu ni udhalilishaji kwa Watanzania.”amesema.

Amesema “Tofauti na Taarifa ya Wizara inavyopendekeza, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Hazina kusitisha makubaliano ya utoaji wa fedha hizo. Badala yake, turudi kwenye mkataba wa mwekezaji wa asili, MSI, ambaye amehamisha hisa zake kwa Bharti Airtel. Ufanyike uchunguzi kubainisha makubaliano katika mkataba na kuona kwa kiwango gani mwekezaji alitekeleza masharti ya mkataba.”

Mnyaa anamalizia kwa kusema tunapaswa “kuchunguza (MSI) alitakiwa kufanya nini, amefanya nini mpaka sasa, na kwa hisa 35% alizopaswa kulipia alitoa fedha kiasi gani. Kama matakwa ya mkataba yametekelezwa ndio mambo mengine yaendelee. Vinginevyo Airtel alipwe dola moja tu na kufunga virago haraka.”

Ubovu wa Menejimenti ya TTCL

Kwa upande mwingine, tayari Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Asad, amemfikishia Rais Kikwete taarifa mbaya kuhusu TTCL.

Taarifa hizo zimemfikia Rais kupitia “Ripoti ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu Ukaguzi wa Mashirika ya Umma kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014.”

Profesa Asad na ujumbe wake walikutana na Rais Kikwete 26 Machi 2015 Ikulu na kukabidhi ripoti hiyo.

Ripoti inabainisha mambo kadhaa yanayoashiria ulegevu wa Menejimenti ya TTCL kama yalivyogunduliwa na CAG.

Kwanza, ilibainika Menejimenti ya TTCL imeshindwa kuimarisha mifumo ya udhibiti wa ndani ili kukabiliana na vihatarishi vya usalama wa kampuni.

Pili, Menejimenti imeshindwa kusimamia ipasavyo mfumo wa mishahara jambo ambalo lilitoa mwanya kwa mtumishi mmoja kutumia mfumo huo kuiibia kampuni kwa kujizidishia mshahara wake kwa kiasi cha Sh. 72 milioni.

Tatu, Menejimenti imefanya manunuzi ya bajaji 30 zenye thamani ya Sh. 156 milioni bila ya kuzingatia vyema Sheria ya Ununuzi wa Umma ya 2004. Hapa, Bodi ya Zabuni ya TTCL ilitumia utaratibu wa zabuni zuifu (restricted tendering) kinyume na maamuzi yaliyofanywa na Bodi ya Wakurugenzi walioidhinisha mchakato wa manunuzi wa ushindani wa kimataifa.

Nne, Menejimenti imefanya manunuzi ya magari 10 yenye thamani ya Sh. 1.25 bilioni pasipo kuzingatia vyema Sheria ya Ununuzi wa Umma. Kamati ya Tathimini ya Zabuni ilipendekeza zabuni hiyo itolewe kwa Toyota Tanzania pamoja na kwamba mzabuni huyu hakukidhi vigezo vingi vilivyoainishwa katika zabuni hiyo.

Tano, Menejimenti imeshindwa kudhibiti matumizi ya mafuta ya magari jambo ambalo liliingizia kampuni hasara ya Sh. 73.7.

Sita, Menejimenti imeruhusu manunuzi ya kiasi cha Sh. 45.7 bilioni nje ya mpango wa ununuzi wa mwaka. Hatua hii ni kinyume na matakwa ya kif. 45 cha Sheria ya Manunuzi ya Umma ya Mwaka 2004 na Kanuni ya 25(3) ya Kanuni za Sheria ya Ununuzi ya Umma ya Tangazo la Serikali Na.97 la mwaka 2005. Kanuni hii inazitaka taasisi za umma kuandaa mpango wa ununuzi kwa kuzingatia mahitaji yaliyopo ndani ya mpango mkakati.

Saba, Menejimenti imefanya manunuzi yenye thamani ya Sh. 3.442 bilioni pasina kuzingatia viwango vya ukomo vilivyoainishwa kwenye jedwali la pili la Kanuni za Sheria ya Ununuzi Tangazo la Serikali Na.97 na 98 la mwaka 2005. Kiwango kilichozidishwa ni Sh. 1.742 bilioni.

Ukiukwaji wa matakwa haya ya kisheria unapaswa kupata idhini ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi (PPRA) kama inavyoelekezwa na kifungu cha 31(3) cha Sheria ya Ununuzi ya Umma ya mwaka 2004. Lakini hakuna kibali kilichoombwa wala kutolewa na PPRA kwa ajili hiyo.

Kutokana na kasoro hizo, Mdhibiti na Mkaguzi ametoa mapendekezo makuu matatu:-

Kwanza, Menejimenti ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ifikirie “kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wote ambao ripoti hii imeainisha kuwa wamehusika katika kuisababishia kampuni hasara ya upotevu wa fedha.”

Pili, “Wakurugenzi wa Bodi ya TTCL watoe mwongozo wa uadilifu na kutekeleza sheria za kukomesha udanganyifu.”

Tatu, “TTCL ihakikishe inafanya ukaguzi endelevu na usimamizi mzuri wa miamala inayofanyika katika mfumo wa hesabu wa Sunsystem, ili kudhibiti wizi kama uliofanyika kwenye mfumo wa uandaaji wa Mishahara.”

Ubia wenye utata kati ya serikali na wawekezaji

Taarifa kwamba kampuni ya TTCL sasa inashikilia mkia wa kibisahara katika sekta ya mawasiliano nchini Tanzania kutokana na serikali kuwakaribisha wawekezaji wenye mgongano wa kimaslahi katika sekta hii zinayo historia ndefu sasa.

TTCL ilianzishwa kwa mujibu wa sheria Na.20 ya 1993 na kupata leseni ya kuendesha biashara ya mawasiliano ya simu za mezani. Mwaka 1999 tayari TTCL ilikuwa imefanikiwa kutafuta leseni ya kuendesha biashara ya simu za mkononi pia kupitia kampuni tanzu iliyoiita Celnet Tanzania Limited.

Ofisi za Celnet Tanzania Limited zilikuwa Kijitonyama, Dar es Salaam, mkabala na jengo la Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTEC).

Uanzishwaji wa Celnet Tanzania Limited ilikuwa ni moja ya mbinu za menejimenti kujiimarisha kibiashara ndani ya ushindani zikiwepo kampuni mbili tu – Tigo na Tritel. Kumbukumbu zinaonesha mtaji wa Celnet Tanzania Limited ulikuwa ni Sh. 500 milioni.

Katikati ya harakati hizo, 21 Februari 2001, serikali iliamua kuibinafsisha TTCL kwa kuuza sehemu ya hisa. Serikali iliuza 35 kwa Dola 120 milioni kwa kampuni ya Mobile System International (MSI) ya Uholanzi.

Hata hivyo, kampuni ya MSI ililipa dola 60 milioni tu (nusu ya kiwango halisi) kwa madai kuwa wangelipa kiasi kilichobaki baada ya mahesabu kukaguliwa upya na mkaguzi huru. Hivyo, malipo waliyoyafanya yalikuwa ni sawa na bei ya hisa asilimia 17.5 pekee. Serikali ilikabidhi menejimenti ya TTCL kwa MSI pamoja na kasoro hiyo ya kutekeleza mkataba.

Baada tu ya MSI kushika mamlaka ya TTCL, ilibadilisha leseni na jina la kampuni ya Celnet Tanzania Limited kuwa Celtel Tanzania Limited, ambayo Novemba 2001 ilipewa leseni ya kuendesha simu za mkononi.

Kampuni ya TTCL ilipewa asilimia 40 ya hisa za Celtel Tanzania Limited, ambazo baadaye zilihamishwa na Serikali na kupelekwa Hazina. Profesa Mark Mwandosya alikuwa ni Waziri mwenye dhamana na TTCL wakati huo, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa Andrew Chenge.

Nyaraka mbalimbali zinaonesha kwamba MSI hawakuwekeza hata senti moja katika kampuni ya Celtel Tanzania Limited. Kinachoonekana ni kwamba, kabla ya kampuni ya MSI kuondoka TTCL mwaka 2005, walikuwa wamelipa ziada ya dola za Kimarekani 8 kati ya dola za Kimarekani 55 walizopaswa kulipa kama sehemu ya pili ya malipo ya hisa walizonunua katika TTCL.

Kwa ufupi, tangu kubinafsishwa kwa TTCL mwaka 2001, hisa zake zipatazo 35% zimekuwa zikiuzwa kwa mkopo kupitia utaratibu wa “mpokezano” kwa makampuni tofauti, yote yakiwa yanajitambulisha kama “wawekezaji” katika TTCL.

Mpokezano huo ni kama ifuatavyo: kutoka MSI kwenda Celtel International (2005), kutoka Celtel International kwenda Zain ya Kuwait (2008) na kutoka Zain ya Kuwait kwenda Bharti Airtel ya India (2010). Kampuni ya Bharti Airtel Ltd ya India ndio mmiliki wa Airtel Tanzania Ltd kwa sasa. Kumbukumbu zinaonesha kuwa wawekezaji hawa wote hawajawahi kuwekeza fedha yoyote ili kuimarisha TTCL.

Utafiti zaidi unaonesha MSI, Celtel International, Zain ya Kuwait na Bharti Airtel ya India wamekuwa “wawekezaji” na wakati huohuo “washindani” wa TTCL kibiashara katika sekta ya mawasiliano.

Kwa hivyo, haya ni makampuni yaliyokuwa na mgongano wa maslahi. Kwa sababu hii, wachunguzi wa mambo wanasema mgongano huu wa kimaslahi uliwasukuma “wawekezaji” hawa “kuihujumu TTCL kisayansi.”

Kwa mfano, utafiti wa Mwanahalisionline ndani ya TTCL umebaini kuwa mpaka leo hii, bado kampuni hii inatumia teknolojia ya mawasiliano duni kuliko teknolojia inayotumiwa na makampuni mengine ya mawasiliano hapa nchini.

Wakati Tigo, Airtel na Vodacom wamekuwa wanatumia teknolojia ya kisasa ya “Global System for Mobile Communication” (GSM), TTCL wamekuwa wanatumia teknolojia kongwe ya “Code Division Multiple Access” (CDMA).

Simu zinazotumia “simukadi” za teknolojia ya CDMA haziwezi kupokea “simukadi” za teknolojia ya GSM. Hivyo, wateja wenye “simukadi” za mitandao ya Tigo, Vodacom na Airtel hawaoni sababu ya kununua “simukadi” za mtandao wa TTCL kwani “simukadi” hizi hazingiliani na simu za mikononi zinazotumiwa na wateja hawa wa mitandao ya Tigo, Vodacom na Airtel.

Lakini, kama TTCL wangetumia teknolojia ya GSM kwa muda wote huo, wangekuwa katika nafasi nzuri ya kushindana wakiwa na nguvu katika soko la biashara ya simu za mkononi nchini.

Hivyo, ni wazi kwamba kikwazo hiki cha kitekinolojia kimechangia kuidhoofisha kiuwezo TTCL na hivyo kubaki ikichechemea.

Takwimu za Mamlaka ya Usimamizi wa Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) zinathibitisha jambo hili. Mpaka Desemba 2012 Tanzania ilikuwa na watumiaji wa simu za meani na mkononi wapatao 28,024,611.

Wateja hawa waligawanyika kama ifuatavyo: Vodacom (44%), Airtel (27%), Tigo (20%), Zantel (8.4), TTCL (0.82%), Sasatel (0.18%) na Benson (0.0037%).

Mhandisi mmoja ndani ya TTCL, aliliambia Mwanahalisionline kwamba takwimu hizi ni ushahidi tosha kuonyesha kwamba “wawekezaji katika TTCL wameihujumu kampuni hii kwa sababu ya mgongano wa kimaslahi uliogubika dhamira na maamuzi yao.”

Hoja hii inaimarishwa na ukweli kwamba jitihada za TTCL kuingia katika soko la mawasiliano ya simu za mkononi zinazotumia teknolojia ya GSM mpaka sasa limekwama.

Historia inajieleza vizuri: Muda mfupi baada ya TTCL kupata hisa katika kampuni ya Celtlel Tanzania Ltd, ilinyang’anywa hisa zote na zikahamishiwa HAZINA mara moja, kwa sababu ya madai kwamba, kwa mujibu wa leseni yake, TTCL haikuruhusiwa kuanzisha biashara ya simu za mkononi.

Hata hivyo, baadaye mwaka 2005, serikali iliondoa masharti hayo ya leseni dhidi ya TTCL. Lakini Celtel international, ambaye tayari alikuwa ni mwanahisa katika TTCL na hivyo mbia wa serikali, alipinga wazo la TTCL kujiingiza kwenye biashara ya simu za mkononi. Sababu ni moja tu hapa: alikuwa ni mshindani wa TTCL katika biashara hiyo.

Baada ya kuona hivyo, wafanyakazi wazalendo ndani ya TTCL waliamua kuingiza biashara hiyo kwa siri kupitia teknolojia ya “CDMA” maarufu kama “TTCL Mobile.” Kwa namna fulani, wazalendo waliidanganya Bodi ya TTCL kuwa teknolojia ya “CDMA” ilikuwa ni kwa ajili ya “Fixed Wireless” au “Wireless Local Loop (WLL).”

Lakini, ukweli, kwa siri walikuwa wamebuni “Full Mobile Solution” ili kujitanua kibiashara. Bodi ya TTCL iliruhusu biashara hii kwa kuwa haikufahamu ukweli wote. Hata hivyo baadaye Bodi ilipogundua iliamua kuzuia uwekezaji zaidi katika mradi huo. Kwa hivyo, mradi wa “TTCL mobile” ukashindwa kufanyakazi kama lilivyokuwa lengo wakati wa kubuniwa.

Leo, miaka 15 baada ya TTCL kubinafsishwa, bado kampuni hii inashika mkia katika biashara ya mawasiliano ya simu.
 
Ttcl haina share bharti Ila bharti ndio ilikuwa na share ttcl ambazo serikali ilisema karibuni watazinunua. Kwa hiyo hii haina uhusiano wowote na utendaji wa ttcl, mwandishi Fanya research zaidi
 
Akili za lumumba zulituingiza mkenge sijuwi kama huyu mtumbua majipu kama anaweza tumia uwezo wake binafsi kuiokoa TTcl ili wa Tanzania wazalendo tuanze kutumia mtandao wetu siku wakiweza kuirudisha mikononi mwa Tanzanian 100% ikawa inaendeshwa na wa Tanzania wazalendo wenye kuipenda inchi yetu ndio itakuwa mwisho wangu kutumia huduma za makaburu
 
Ttcl haina share bharti Ila bharti ndio ilikuwa na share ttcl ambazo serikali ilisema karibuni watazinunua. Kwa hiyo hii haina uhusiano wowote na utendaji wa ttcl, mwandishi Fanya research zaidi
KABLA , HAMJANUNUA WAO WASHUZA KWA American Tower ;
JE WASHIRIKA WATAKUWA WANGAPI??
JE MTANUNUA KWA BEI GANI???????

UMESHAJIULIZA MASWALI HAYO.

KWANINI BAADA YA KUSIKIA MNANUNUA HISA ZENU; WAMEKIMBIA NA KUUZA TRANSIMISSION NA FREQUENCY , RADIO (ERICKSON ) NIO GHARAMA KUBWA.

WAMEUZA MAPEMA : BADO UJASHITUKA


KWANINI WASINGEWAUZIA WABIA WENZAO TTCL KABLA YA KUMZIA American Tower????
 
TTCL haina ubia bharti, Cjui kama unaelewa!!! Kwa maana rahisi Ni kwamba bharti Ni mmoja wa wamiliki wa TTCL kwa hiyo akiamua kuuza Mali yake, TTCL haiwezi muuliza chochote maana haimuhusu. TTCL hawana hisa zozote ndani ya bharti au airtel ya zamani
 
TTCL haina ubia bharti, Cjui kama unaelewa!!! Kwa maana rahisi Ni kwamba bharti Ni mmoja wa wamiliki wa TTCL kwa hiyo akiamua kuuza Mali yake, TTCL haiwezi muuliza chochote maana haimuhusu. TTCL hawana hisa zozote ndani ya bharti au airtel ya zamani
Kwa vile Airtel ilianzishwa kwa fedha, leseni na raslimali za TTCL, na mpaka sasa inatumia miundombinu ya TTCL kama vile jenereta, majengo, na viwanja, basi haipaswi kulipwa hata senti,” alisisitiza Mnyaa ambaye ni mbunge wa jimbo la Mkanyageni, Kusini Pemba.
 
Ttcl haina share bharti Ila bharti ndio ilikuwa na share ttcl ambazo serikali ilisema karibuni watazinunua. Kwa hiyo hii haina uhusiano wowote na utendaji wa tmwandishi Fanya research zaidi
Nilivyoelewa kwa mujibu wa mkataba, major shareholder Airtel, walipaswa kuendeleza na kuifufua TTCL lakini wanafanya kinyume kwa kuhihujumu na kuzuia jitihada zote za ttcl kufufuka.
Ni jipu kwa sababu serikali Ina hisa zake na kubebeshwa mzigo wa kuendesha ttcl na madeni.
 
Nilivyoelewa kwa mujibu wa mkataba, major shareholder Airtel, walipaswa kuendeleza na kuifufua TTCL lakini wanafanya kinyume kwa kuhihujumu na kuzuia jitihada zote za ttcl kufufuka.
Ni jipu kwa sababu serikali Ina hisa zake na kubebeshwa mzigo wa kuendesha ttcl na madeni.
Hiyo Ni kweli lkn walishalimaliza miaka michache iliyopita TTCL wakaanzisha mobile zao lkn kwa baadhi ya maeneo, upingufu upo upande wa serikali na watendaji wao, wanaingia mikataba ya kijinga
 
Nilivyoelewa kwa mujibu wa mkataba, major shareholder Airtel, walipaswa kuendeleza na kuifufua TTCL lakini wanafanya kinyume kwa kuhihujumu na kuzuia jitihada zote za ttcl kufufuka.
Ni jipu kwa sababu serikali Ina hisa zake na kubebeshwa mzigo wa kuendesha ttcl na madeni.
NDO MAANA NILIULIZA JIPU NI AIRTEL AU TCCL?????????????

JE AIRTEL ANAUZA MINARA KWA FAIDA YA NANI WAKATI TULITEGEMEA ANGUZIA TTCL '

KAMA SIO JIPU LA TEGETA ESCROW:
VIP ENGINEERING---------- PAP VS TANESCO
AIRTEL.........................AMERICAN TOWER VS TTCL

????????????
LOADING...................................................................
 
KAMPUNI YENYEWE ILIYOUZIWA MINARA NI MAJANGA MAREKANI - ISHASHITAKIWA ;
SWALI

IMEINGIAJE TANZANIA HII KAMPUNI
JE VYOMBO VYA USALAMA VINAHIJUA

KWENYE MINARA NDO RADIO ZA MAWASILIANO ZIPO , NA CHINI UNAKUTANA NA SWITCH NA ROUTER jE MAWASILIANO YETU NA MIPANGO YETU NA CHINA BADO HAIJAINGILIWA TU.
 
Hili la TTCL inabidi Magufuli alifuatilie na alitumbue kwa ustadi mkubwa. Ikiwezekana tuangalie namna ya kuwafikisha Bharti kwenye mahakama za kimataifa za biashara kama vipengele vya mkataba vinaruhusu.

SFO wanaweza kodishwa kufanya uchunguzi wa sakata tete kama hili au wao ni kwa kesi zinazohusu Uingereza pekee?
 
NAUONA MGOGORO KATI:

SERIKALI YA MAREKANI NA SERIKALI YA TANZANIA.
TUSIPO WAWAHI HAWA AIRTEL KABLA YA KUKAMILISHA MKATABA WA KUWAUZIA AMERICA TOWER CO.

NA CHAGUZI ZETU NDO WATAVALIA NJUGA KWELI KWELI; TUKIWASUMBUA WAWEKEZAJI TOKA USA. KWA MKATABA WA UKAJANJA BILA THIRD PARTY KUSHIRIKISHWA
 
Jipu hilo lilianza toka wakati wa BWM. Mzee wa Chato litumbue haraka na katika kitu kinahitaji kutatuliwa nchi hii ni mikataba mingi ni ya magumashi UDA,TAZARA,IPTL,NHC NA developers, Parking system,Vituo vya basi kama makumbusho, fibre optic cable, barrick ikageuka ikawa acacia, Tanzanite one
 
Kama ttcl inekuwa ni nyumba iliyoingiliwa na panya basi mimi nisingehangaika kukimbizana na hao panya humo ndani,ningeipiga tu kibiriti jumla! Nyumba na panya vife pamoja!!! Kumbaff kabisa
 
Back
Top Bottom