Mgogoro stend ndogo Arusha: Katibu wa wapangaji atishiwa maisha

Mwan mpambanaji

JF-Expert Member
Apr 3, 2008
482
131
Mgogoro wa vibanda stend ndogo umechukua sura mpya ya kutishiana maisha.Eneo la Stend ndogo limegeuka uwanja wa vita kati ya wapangaji na wajenzi kwa upande mmoja na wafanyabiashara wapangaji na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha kwa upande wa pili.

Taarifa za uhakika ni kuwa Mkurugenzi ameamuru katibu wa wafanyabiashara wajenzi ambaye ni binti mdogo wa miaka 24 afukuzwe eneo la stend.Chanzo cha uhakika kutoka ofisi ya mkurugenzi ambaye anatuhumiwa kupokea rushwa kubwa kutoka kwa wajenzi,kinasema kuwa Katibu huyo wa wafanyabiashara ana msimamo mkali sana,na Mkurugezi wa Jiji anaamini huyo binti akiondolewa hapo wenzake watakata tamaa.Kwa sasa Mkurugenzi yupo kwenye wakati mgumu sana kufuatia pressure aliyowekewa na hao wajenzi ambao kimsingi ni madalali na ambaoaliwaahidi kuwapatia mikataba jambo ambalo hadi leo halijatekelezwa.

Katibu wa wafanyabiashara hao ameeleza kuwa maisha yake yapo hatarini kutokana na maagizo ya mkurugenzi wa Jiji ndg Athuman Kihamia.Ameendelea kusema kuwa amekuwa akifuatiliwa na kupokea sms za vitisho kutoka kwa wajenzi ambao hudai wamepewa maelekezo na Mkurugenzi wa jiji
Itakumbukwa kuwa mwaka jana Mratibu wa elimu kata ya Ungaltd alitekwa na kuumizwa vibaya kabla ya kutupwa porini,na watekaji walisema kuwa walitumwa na Mkurugenzi.
 
Kuna kitu watuu hawakielewii hapo stand ndogo. Vurugu zote hizii zimekujaa baada ya hice kuhamishiwa kilosa sasa wafanya biashara halii imekuwa ngumu. Biashara imedorora kiasi kikubwa kutokana na kupungua kwa watu. Wengi wao wanamikopo wenye nyumba wanadai kodi zao kwa fujo wakat biashara hakunaa lakini kipind cha nyuma kunae jam ya watu hice zote zinatemea palee mambo yalikuwa supaa wajenz walikuwa wanapewa pesa zao wanatulia na watu kazi kama kawaida. Huo mgogoro ninjaaa nakuyumba kwa biasharaa kuliko sababishwa na hice kupelekwa kilosaa zotee
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Back
Top Bottom