Mgogoro NCCR-Mageuzi: Mwenyekiti, Katibu, Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini wapewa siku 3 kujiuzulu

Reucherau

JF-Expert Member
Nov 26, 2014
756
1,740
Faustine Sungura aliyekuwa Mkurugenzi wa uchaguzi wa NCCR Mageuzi amesema Mwenyekiti wa chama hicho James Mbatia ameuza mali za chama kinyume na utaratibu.

Sungura amedai, shamba lililopo Kijiji cha Kirombo, Bagamoyo ni la chama, lakini lipo kwa jina la James Mbatia.

Eneo hilo kwa mujibu wa Sungura, lilinunuliwa kwa ajili ya ujenzi wa chuo, ambapo alionyesha nakala ya gazeti la Nipashe la tarehe 16.2.2002 lililoripoti kuhusu chama hicho kununua shamba hilo.

Mkurugenzi huyo wa zamani ametoa siku 3 kwa mwenyekiti, katibu mkuu na mwenyekiti wa baraza la wadhamini la chama kujiuzulu.



======

MWENYEKITI wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia amepewa siku tatu na mwanachama wa chama hicho akitakiwa kujiuzulu mwenyewe wadhifa huo ndani ya chama kwa madai ya kupora mali za chama na kujimilikisha.

Mwanachama huyo, Faustin Sungura ametoa muda huo jana, Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari. Alisema kuwa hata Katibu Mkuu wa Chama hicho, Martin Danda anatakiwa kujiuzulu kutokana na kutamka asichokijua kuhusu mali za chama hicho.

Kuhusu Mbatia, Sungura amesema Mbatia kama hatachukua maamuzi hayo kwa muda uliotajwa, atakwenda Mahakama ya Wilaya kuomba kibali cha kesi ya jinai na akikipata atamshitaki Mbatia kwa wizi wa mali za chama.

Amesema mali anazomtuhumu nazo Mbatia kuwa ni za chama ni pamoja na shamba la ekari 56 lililopo eneo la Kilomo wilayani Bagamoyo, mkoa wa Pwani na nyumba mbili zilizopo eneo la Bunju B jijini Dar es Salaam.

Kuhusu shamba hilo, alisema lilinunuliwa mwaka 2002 kwa makubaliano ya wanachama waasisi wa chama hicho kuwa litumike kama chuo cha kufundishia makada wa chama hicho ambapo kilitakiwa kuanza kazi Desemba mwaka huo huo.

“Ununuzi wa shamba hilo ni moja ya mpango mkakati wa chama hicho, ambao ulielekeza kuwepo kwa ujenzi huo lakini baadae Mwenyekiti wa chama hicho akawageuka na kudai kuwa shamba hilo ni mali yake, vielelezo vya ushahidi vipo hata katika taarifa zake kwa vyombo vya habari alizungumzia kuhusu suala hilo,” amesema Sungura.

Sungura amesema kuhusu tuhuma hizo kwa kiongozi wake, kuwa Mbatia ni shahidi namba moja kwa kuwa taarifa za ununuzi wa shamba hilo upo katika taarifa zilizoandikwa katika magazeti nchini kwa mwaka 2002 zikimnukuu mwenyekiti huyo.

Alisema “Katika gazeti moja nchini la mwaka 2002, Februari 16, Mbatia mwenyewe akizungumza na waandishi wa habari alibainisha kuwepo kwa haja ya ununuzi wa shamba hilo kwa matumizi ya kuwa chuo, lakini kwa sasa amekuwa akisema shamba hilo ni la kwake na sio la chama.”

Sungura alisema nyaraka za vilelezo vya kuhusu ununuzi wa shamba hilo pamoja na nyumba vipo na wenye kujua taarifa za mali hizo za chama ni wanachama waliobaki katika chama hicho ambao ni waasisi, walioingia wapya hawajui na kudai wamekuwa wakitumiwa na kiongozi huyo kupotosha ukweli.

Kuhusu taarifa hizo kama ni msimamo wa chama, Sungura alisema si msimamo wa chama na kwamba hata inapotokea wanachama wakawa hawana imani na kiongozi wao, katiba ya chama ina utaratibu wa vikao kwa ajili ya suala husika.

Chanzo: Habari leo
 
Walioko kwenyehicho kikao kama vile wamekata tamaaa.
Yaaani upinzani wa tanzania unasikitishaa.

Lakini tatizo ni kwamba watanzania walilazimishwa kukubali vyama vingi nawakati walikuwa hawavitakiii. ndio maaana upinzani kudumu kwake ni kudogo mnooo.
 
Hivi wewe mleta mada unajinyea baada ya kunyimwa buku7 hapo Lumumba? Yaani mwanachama mmoja tena asiyekuwa kiongozi awapatie viongozi siku tatu kujiuzulu? Tokea lini chama kikajiendesha kiuni kiasi hicho hata kingekuwa kile cha majambazi malaika mkuu hawezi kuwataka viongozi wajiuzulu pasipo ya kukaa vikao harali vya chama. Pili unasema akilejea gazeti lilitoa taarifa ya kununuliwa kwa kiwanja hicho .....Are you serious guy? Leo gazeti linahalarisha kitu na sisi tuamini kwa hilo kwa nn huyo sungura njaa asikupatie Hati ya hicho kiwanja tuione?
 
Ile sinema ya Prof wa buguruni imefeli sasa inaletwa ya kijinga zaidi na matokeo yatakua yakuumiza zaidi kwa watesi wa demokrasia
 
MWENYEKITI wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia amepewa siku tatu na wanachama wa chama hicho akitakiwa kujiuzulu mwenyewe wadhifa huo ndani ya chama kwa madai ya kupora mali za chama na kujimilikisha.

SOURCE: HABARI LEO Mbatia apewa siku tatu ajiuzulu
 
Kwa nini sio Lipumba aliyepora huku akivunja ofisi? au kisa alisindikizwa na polisi na analindwa na policcm?!
 
Utasikia eti ni hujuma za sisiemu kudhohofisha upinzani hahahah ngoja niwaachie vyamavyenu
 
Back
Top Bottom