Mgogoro CBE Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgogoro CBE Dodoma

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MwanaCBE, Oct 30, 2009.

 1. MwanaCBE

  MwanaCBE JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2009
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,773
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu niliwahi kusema hapa mabadiliko ya haraka yanatakiwa katika uongozi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dodoma. Sasa hivi chuoni hapa kuna mgogoro kati ya wanafunzi wa shahada wa mwaka wa kwanza na uongozi wa chuo.Wanafunzi waliodahiliwa kusoma shahada za Procurement, Marketing na Business Adminstration wanalazimishwa wasome Accountancy au wahamishiwe campus ya CBE Dar. Sababu ni uhaba wa waalimu wenye vigezo kitaaluma(masters na kuendelea) wanaotakiwa kufundisha shahada. Ikumbukwe CBE walikuwa wanatoa Advanced Diploma ambayo imesitishwa rasmi tangu mwaka jana. Majibu ya uongozi wa chuo kwa wanafunzi hawa ni ya hovyo hovyo tu.Hakuna cha maana kinachofanywa na uongozi wa chuo ili kuleta maelewano.Kibaya zaidi uongozi wa wanafunzi ni kama haupo(umekufa). Si rais (Ali Sichonge), si makamo wa rais (Paschal), si waziri mkuu wala mawazili wa elimu wamechukua hatua yeyote ya maana ili kuwanusuru wanafunzi na huu upuuzi unaofanywa kwa makusudi na uongozi wa chuo.Vice Princple wa chuo KIputiti yuko kimya (eti naye mwakani atagombea ubunge kwa tiketi ya CCM (inakera)). Sasa bunge linaendelea Dodoma, na Waziri Wa Viwanda na Biashara Mama Nagu upo. Saidia wanafunzi hawa kwani CBE iko chini ya wizara yako.Lakini pia Profesa Maghembe (Wazili wa Elimu) saidia hawa wanafunzi dhidi ya ubabaishaji unaofanywa na watu waliochoka kimawazo katika uongozi wa chuo hiki.I submit.
   
Loading...