BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,769
- 288,337
Barrick kuanzisha mgodi mpya Mwakitolyo Wednesday, 11 May 2011 20:13
Zulfa Mfinanga,
Shinyanga
Mwananchi
KAMPUNI ya African Barrick Gold Mine, ina mpango wa kuanzisha mgodi mwingine wa dhahabu katika Kata ya Mwakitolyo, mkoani Shinyanga mapema mwakani.
Mgodi huo utakajulikana kwa jina la Golden Ridge Project.Akizungumza na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga juzi, Meneja wa Uhusiano wa kampuni hiyo, Philbert Rweyemamu, alisema utafiti uliofanyika katika eneo hilo, umethibitisha kuwapo kwa dhahabu ya kutosha kuanzishwa kwa mgodi.
Alisema kwa sasa, kampuni inafanya tathmini kuhusu athari kimazingira na jamii na kwamba hatua hiyo inawashirikisha wananchi watakaohamishwa ili kupisha mradi huo.Alisema ushirikishwaji wa wananchi hao, unafanyika kupitia katika kamati mbadala inayongozwa na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo.
Kwa mujibu wa Rweyemamu, kamati hiyo pia inajumuisha wawakilishi wa wananchi wa eneo hilo, wawakilishi wa kampuni na wakuu wa idara mbalimbali za serikali.
"Kama utaratibu huu utasimamiwa na kutekelezwa vizuri, nina imani kikubwa kuwa utaondoa malalamiko ya wananchi kuhusu fidia, kwa sababu wananchi watashirikishwa ipaswavyo katika kila hatua,"alisema Rweyemamu
Akizungumza kwa niaba ya madiwani, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Amos Mshandete, alisema ziara hiyo itawasaidia kujifunza mambo mazuri yaliyofanywa katika uanzishaji wa mgodi wa Buzwagi.
Alisema kitendo hicho kitawasaidia madiwani kupata uelewa wa shughuli za mgodi na hatimaye kushiriki kikamilifu katika kusimamia uanzishwaji wa mgodi huo mpya, jambo ambalo litapunguza kero za wananchi.
"Kwa kweli tumepata picha nzuri itakayotusaidia katika kuanzishwa kwa mgodi wa Mwakitolyo utakaoanza kazi hivi karibuni," alisema Mshandete.Mgodi wa Mwakitolyo, upo umbali wa kilometa 100 Kusini mwa Jiji la Mwanza na kilometa 30 kusini Mashariki mwa mgodi wa Bulyanhulu.