WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga wamemjia juu mwenyekiti wao wa mkoa, Khamis Mgeja, wakisema anatumiwa na kundi la mafisadi kujinufaisha kwa maslahi yake binafsi. Katika taarifa yao waliyoituma kwenye vyombo vya habari, wanachama hao walisema wanashangazwa na hatua ya kiongozi huyo kuanzisha malumbano na viongozi wa chama na serikali.