Mgawanyo wa mali za Mwanza uko kisheria’

sir.JAPHET

JF-Expert Member
May 18, 2012
699
133
[h=2][/h] Jumamosi, Septemba 08, 2012 08:26 Na John Maduhu, Mwanza

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Wilson Kabwe, amesema suala la mgawanyo wa mali zilizokuwa za Halmashauri hiyo liko kisheria na haliwezi kufanywa kutokana na matakwa au hisia za mtu mmoja kama anavyotaka.
Ufafanuzi huo ameutoa katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri cha kujadili namna ya kugawa mali za Halmashauri ya Jiji la Mwanza katika kutekeleza uamuzi wa kuligawa na kuzaliwa kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.

Alisema kwa mujibu wa sheria, suala la kugawanywa kwa mali limeelezwa kisheria na mwenye uamuzi wa mwisho juu ya suala hilo ni waziri mwenye dhamana.

“Madiwani na wabunge mnapaswa mjiepushe na upotoshaji juu ya ugawanyaji wa mali za jiji, suala hili liko kisheria kwa kuwa kuna mambo muhimu ya kuzingatiwa ikiwa pamoja na madeni, rasilimali na huwezi muda huu kutamka kuwa tugawane kila kilichopo na kuanza maisha mapya.

“Kuna mali nyingi ambazo Halmashauri ya Jiji iliingia mkataba na wawekezaji mbalimbali pamoja na taasisi za fedha, huwezi kukurupuka na kusema kuanzia leo mali hizi ni za Ilemela, hapana, lazima utaratibu pamoja na sheria zifuatwe kuepusha mgongano usio na tija,” alisema Kabwe.

Alisema baada ya vikao kupitisha mapendekezo ya watalaamu, Baraza la Madiwani kwa upande linatakiwa kujadili juu ya mapendekezo kisha suala hilo kupelekwa kwa waziri kwa ajili ya hatua zaidi.

“Madiwani na wabunge mnapaswa msome sheria zilizopo, suala hili si kwamba limeanza leo kwa halmashauri kugawanywa, limeishawahi kufanyika sehemu nyinginezo hivyo Serikali ina uzoefu,” alisema Kabwe.

[h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
 
Back
Top Bottom