Mgao wa umeme Jijini Mwanza

Mgao wa umeme Jijini Mwanza

1952

Senior Member
Joined
Mar 29, 2014
Posts
109
Reaction score
40
Napenda kutoa MASIKITIKO yangu makubwa kwa mgawo wa umeme Jijini Mwanza jinsi unavyokera na kuleta usumbufu mkubwa kwa wananchi. Kwanza kama kuna mgawo wa umeme tunatakiwa kutangaziwa kwenye vyombo vya habari au kupitia magari ya matangazo. Hapa Mwanza maeneo ya Nyakato, Mwananchi sasa imekuwa kawaida umeme kukatwa kuanzia saa moja na nusu asubuhi mpaka saa kumi na mbili jioni na kukatwa tena saa moja jioni mpaka saa nne usiku. Wenyewe wanajua fika kuwa umeme ndiyo maisha kwa kila kitu ukianzia matumizi ya nyumbani kama kupika, kupiga pasi, kuchemsha maji, vyakula kwenye friji, redio, TV, kutengeneza barafu kwa ajili ya sisi wanyonge na kusukuma maji n.k. Hapa nilipo hakuna hata tone la maji kwenye mabomba ya majumbani na kila kitu ni hovyo. Hakuna maji kwa ajli ya matumizi ya nyumbani na hii yote inasabishwa na TANESCO. Tuelezwe wazi kama nchi IMEFILISIKA ili tujue moja. Wakati wa Prof. Muhongo kukatika katika kwa umeme Jijini Mwanza ilikuwa ni ndoto. Tutamkumbuka Prof. kwa msimamo aliokuwa nao kwenye Wizara ya Nishati.
 
ata huku butimba,ikfika saa moja kasoro wanakata wanarudsha saa 4 kasoro,hamna taarfa wala nini,hili shrika linaongozwa na machiz ,nukus tupu,kuna viongoz hawajui ata utaratbu,hawajui ata athari za kukata umeme bila taarfa.
 
Hilo tatizo lipo sehemu nyingi inawezekana kuna kitu wanashughulikia na labda ni emergency. mnaweza taarifiwa any time kama hali bado si shwari, acheni kulalamika huku kwani haitasaida lolote zaidi ya kupiga kelele tu
 
Tulieni

Tanesco inaangaza maisha yenu


Wanakeeeeeeeraaaaaa kweli kweli hawa
 
hii NiDharau !! Tena nasema ni DHAAARRRAAAUUUUUUU kwa wananchi !! (kutowajaali hata kwa uwezo wa pesa/fedha zao)
 
Huo mgao ungekua dar, ungejadiliwa kwenye vyombo vya habari.

Jana mto wa mabibo, leo kila sehemu imeongelewa, utadhani hakujawahi tokea majanga ya moto.
 
Baniani mbaya, kiatu chake dawa. Ya Muhongo sasa ni "Tungejua". "Tungejua" huja baada ya uamuzi kuchukuliwa. Tulipoamua kushabikia kung'olewa kwa Muhongo tulipaswa kujiandaa kisaikolojia kwa ajili ya kukabiliana na adha hizi za mgao wa umeme. Nasema; na bado!!!
 
Hata warembo wangu wa Bwiru gilrs wameniambia kuna shida ya umeme kumbe ni mgao duh...naona hapa iringa hali ni shwarii...poleni wana mwanza
 
Back
Top Bottom