Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Nje ya uwanja vyombo vya habari nchini Mali vimeripoti kukamatwa bwana mmoja aliyefahamika kwa jina la Sinayogo ,ambaye ni Mganga wa kienyeji , hii baada ya kudaiwa kupokea jumla ya €33,500 [Tsh. 97 Milioni] akiwahakikishia watu kuwa Mali itabeba ubingwa wa AFCON.
Sinayogo alikusanya pesa hizo kutoka kwa mashabiki wa timu ya taifa ya Mali, akisema ana uwezo wa kuwasaidia Mali kuwa mabingwa AFCON.
Baada ya timu hiyo kutolewa, watu wenye hasira kali walikusanyika nyumbani kwake ili wamchukue ndipo polisi walipoingilia kati ili kuzuia fujo na kumtia nguvuni.
Baada ya timu hiyo kutolewa, watu wenye hasira kali walikusanyika nyumbani kwake ili wamchukue ndipo polisi walipoingilia kati ili kuzuia fujo na kumtia nguvuni.