Mgambo wamzimisha raia ndani ya kituo cha polisi

Mgambo wamzimisha raia ndani ya kituo cha polisi

Abdull Kazi

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2012
Posts
344
Reaction score
306
Watu wanaodaiwa kuwa mgambo, wengine wanawaita Polisi jamii,wakiwa katika kituo cha Polisi cha Tabata Kisiwani, wamemshambulia mwananchi mmoja aliyefika kituoni hapo akiwa ametofautiana na ama ni mkewe au mwanamke wake,hadi kufikia hatua ya kupoteza fahamu huku kituo hicho cha Polisi kikiwa hakina askari hata mmoja wa kusikiliza shida za wananchi Tukio hilo limetokea muda mfupi uliopita ambapo raia huyo baada ya kupigwa na kuporwa shilingi 10000, aliamriwa aondoke kituoni hapo huku akiwa na maumivu sehemu mbali mbali ya mwili wake, hata hivyo jamaa hakuweza kuondoka na badala yake akiwa hatua chache kutoka katika kituo cha Polisi alidondoka chini na kupoteza fahamu hali iliyowalazimu baadhi ya wananchi kumrudisha kituoni na kuwabana mgambo hao kujua sababu za kumpiga na pia wakitaka wapewe pf3 kwa ajili ya matibabu mgambo kuona hali ni mbaya wakaamua kukiacha kituo na kutimua mbio hali iliyowafanya wananchi wawasilianane na OCD wa Buguruni ambaye aliagiza gari la kumbeba majeruhi na kisha kuamuru kituo kifungwe huku askari waliofika kwa agizo la OCD wakiondoka na vitabu vilivyokuwa kituoni hapo NB picha ya jamaa akiwa amelala kchini nje ya kituo cha Polisi ninayo, pia ya polisi waliofika kumchukua ninanyo na nyingine ni yenye kuonyesha kituo kimefungwa ila sijui namna ya kuziweka mnaweza kunisaidia ili mzione
 
Kweli username yako Barabara ya Vumbi na mawazo yako vinaendana.Angekuwa ni ndugu yako ndiye amekula kipigo au wewe mwenyewe kauli yako ingebadilika.Huu uonezi tunaupinga kila siku.Kama huna cha kuchangia kaa kimya.
 
waambie mods watakusaidia mkuu hata mimi nina tatzo la kuweka picha ili iwe kubwa....asante kwa taarifa ma haya ndio yanayoendelea mtaani,kwa upuuzi huu ni kwa nini tusiwakamate hao polisi na kuwapa discipline???time will tell....
 
Back
Top Bottom