Mfupa Uliomshinda Donald Trump

Mfupa Uliomshinda Donald Trump

Seawhale

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2016
Posts
1,708
Reaction score
2,049
Wakuu.

Tokea kurejea kwake madarakani, Rais Donald Trump amekuwa ni kiongozi wa mipasho na kupenda kuabudiwa na kila mtu huku akiamini kuwa yeye ndiye fundi mwenye sauti kuu kwenye kila idara nyeti.

Bwana Jerome Powell mwenyekiti wa Federal Reserve amekuwa ni mwiba mchungu na mfupa pekee ambao Trump ameshindwa kuutafuna. Kwa miezi kadhaa kumekuwa na vuta n'kuvute kati ya hawa wazee wawili, mmoja akishinikiza kushushwa kwa riba huku mwingine akikaza kamba kwa kuendelea kushikilia riba iliyopo kwa miezi zaidi ya 6 bila kumuogopa na kufuata maagizo ya mkuu wake huyo, hali iliyopelekea kurushiana vijembe vya hapa na pale.

Powell amekuwa ni mtu pekee mwenye kutumia mamlaka yake kikatiba na kuweza kumpinga Trump waziwazi juu ya kuingilia majukumu ya Benki kuu. Leo hii ameendeleza msimamo wake kwa kuishikilia riba iliyopo licha ya vitisho vya Trump.
Screenshot_20250730-211127~2.png
Screenshot_20250508-180849~2.png
Screenshot_20250730-213758~2.png
Screenshot_20250730-213906~2.png
 
Nilichoona ni mtoa mada unataka kufananisha uongozi wa USA ufanane na wa Bongo, rais wa USA sio mkuu kwenye kila kitu kama ilivyo hapa bongo
 
Wakuu.

Tokea kurejea kwake madarakani, Rais Donald Trump amekuwa ni kiongozi wa mipasho na kupenda kuabudiwa na kila mtu huku akiamini kuwa yeye ndiye fundi mwenye sauti kuu kwenye kila idara nyeti.

Bwana Jerome Powell mwenyekiti wa Federal Reserve amekuwa ni mwiba mchungu na mfupa pekee ambao Trump ameshindwa kuutafuna. Kwa miezi kadhaa kumekuwa na vuta n'kuvute kati ya hawa wazee wawili, mmoja akishinikiza kushushwa kwa riba huku mwingine akikaza kamba kwa kuendelea kushikilia riba iliyopo kwa miezi zaidi ya 6 bila kumuogopa na kufuata maagizo ya mkuu wake huyo, hali iliyopelekea kurushiana vijembe vya hapa na pale.

Powell amekuwa ni mtu pekee mwenye kutumia mamlaka yake kikatiba na kuweza kumpinga Trump waziwazi juu ya kuingilia majukumu ya Benki kuu. Leo hii ameendeleza msimamo wake kwa kuishikilia riba iliyopo licha ya vitisho vya Trump.View attachment 3425163View attachment 3425164View attachment 3425171View attachment 3425172
Kuna mengi yatamshinda mpaka atakapoondoka madarakani.
 
Kuna mengi yatamshinda mpaka atakapoondoka madarakani.
Hakika mkuu, ila kwa huyo Fed Chair, Trump amepata mpinzani wa kweli. Majuzi wslikuwa wote kwenye makao makuu ya Federal Reserve kufanya tathmini ya gharama ya ukarabati wa majengo, Trump akataja kiasi cha pesa ambacho Fed Chair alikipinga mbele yake kwa kumuambia kuwa hauko sahihi juu ya gharama halisi huku maafisa wengine wakipigwa na mshangao namna Powell anavyojiamini mbele ya Trump.
 
Nilichoona ni mtoa mada unataka kufananisha uongozi wa USA ufanane na wa Bongo, rais wa USA sio mkuu kwenye kila kitu kama ilivyo hapa bongo
Mtoa mada katoa taarifa za Trump hata kichwa cha habari kinajieleza hakuna sehemu ya Tanzania hapo mkuu.
 
Back
Top Bottom