Juzi tulielezwa kupitia vyombo vya habari kuwa mfumuko wa bei kwa mwezi huu umepungua. Binafsi siwaelewi kabisa. Kama baadhi ya bidhaa tunazaotumia na hasa zinazotengenezwa na mali ghafi toka nje zimepanda huo mfumuko wa bei unapunguaje?. Nitoe mfano mdogo tu. Sementi Dar ilikuwa inauzwa Tshs.12000 sasa Kigamboni inauzwa Tshs.15500. Kadhalika na hasa vifaa vya ujenzi. Mtueleze kwa uwazi kipimo cha mfumuko wa bei ni nini?.