Mfumo wa fedha wa Kiislamu - 1

Mfumo wa fedha wa Kiislamu - 1

GAS STATE

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
1,769
Reaction score
960
Assalam wakuu

Nimependa niwaletee elimu toka kwa mtaalamu kama ifuatavyo

Utangulizi
Bismillah Rahman Rahim. Watu wengi bado wanajiuliza juu ya mfumo huu wa fedha wa kiislamu hususani uendeshaji wake kibiashara.

Mfumo wa fedha wa Kiislamu ni mfumo mtambuka wa uendeshaji na usimamizi wa fedha biashara na uchumi kwa kufuata (comply) sheria za dini ya Kiislam (Islamic shar’iah).
Sheria hizo za Kiislamu zimetokana na Qur’an tukufu na Hadithi za Mtume Muhammad (SAW).

Mfumo huu umejikita katika mambo makuu yafuatayo
i. Uendeshaji wa biashara za kawaida (trade)
ii. Taasisi za fedha (financial institutions) kama vile bima (takaful), benki na
iii. Taasisi zinazofanana nazo kama vile VICOBA.

Kwa uwezo wa Allah kitabu hiki kitajikita katika biashara tu, na toleo lijalo Insh’aalah litaendelea na Taasisi za Fedha.
Insh’allah mwandishi amejikita kutoa elimu kwa Waislamu na Wasio waislamu juu ya namna mfumo huu unavyofanya kazi.

Mwandishi ametumia lugha nyepesi ili kuendana na hadhira aliyoikusudia. Mwandishi anaamini wepesi wa lugha utakifanya kitabu kieleweke zaidi.

BIASHARA ZA KIISLAMU (ISLAMIC BUSINESS)
Ni biashara ambazo uendeshaji wake unaongozwa na kanuni na taratibu za dini ya kiislamu. Bidhaa zozote zilizoharamishwa katika Uislamu ni haramu pia katika mfumo huu. Hii haina maana kuwa sheria za nchi hazifuatwi la hasha.

Mfano Pombe ni haramu katika Uislamu hivyo biashara ya pombe pia ni haramu.
Allah S.W amehalalisha biashara kwa waja wake na kuharamisha ribah hii ina maana kuwa biashara ni kazi/shughuli halali kwa Waislamu lakini lazima ifanywe kulingana na mipaka ambayo Allah kaiweka (IKHLAS) sambamba na Serikali. Suratul Baqarah inafafanua hili katika aya zifuatazo:

276. Wale wanaokula riba, hawatasimama ila kama anavyosimama yule ambaye Shetani humpoozesha kwa kumshika. Hayo ni kwa sababu wamesema, Biashara ni kama riba tu; hali Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na kuiharimisha riba. Na aliyefikiwa na mauidha kutoka kwa Mola wake, kisha akajizuia, basi yake ni yale yaliyokwisha pita, na shauri yake ni kwa Mwenyezi Mungu. Lakini anayerejea (kula riba), basi hao ndio watu wa Motoni, humo watakaa.
​
277.Mwenyezi Mungu Hufuta riba na Hukuza sadaka, na Mwenyezi Mungu hampendi kila aliyethibitika kuwa kafiri na mtenda dhambi mkuu.

Na
TONYA. A. TONYA

ITAENDELEA (No pm kama una lolote mpigie mwenyewe)
Ni (copy & paste)
 
Duniani kuna vitu ukivielewa unaondoka kwenye utumwa wa fikra.
Ogopa sana kushikiwa akili, umezaliwa na fresh mind yako watu wanakuja kukupa limits za kuishi, kucontrol mind yako, your ability & skills, passion na wishes zako.
Am proud of myself being atheist.
Kwa comment hii fupi kuna mtu atapata kitu na kubadilisha maisha
 
Am the one!!! [emoji106]
 
Ulipangwa kwanza kua mwanadam na sio kuku halafu unashangaa kupangiwa limits?
 
haha unajilinganisha na kuku
Ukiwa na akili yako timamu utafahamu kuwa hauna uhuru wa kifikiria,
Unaishi kwa assumption na outdated literature.
Read books you will discover your value and even one minutes doesn't mean to be lost
 
Subiri mada itaendelea hapa utajuwa mengi pamoja na hilo(ila mi sijataja neno galatia hapa)
Umenena vyema yaani yeye anaamini uristo ni dini dhidi ya uislamu kumbe hajui hapa unafundisha elimu juu ya mfumo huo hata mmbudha aweza nufaika.
 
Duniani kuna vitu ukivielewa unaondoka kwenye utumwa wa fikra.
Ogopa sana kushikiwa akili, umezaliwa na fresh mind yako watu wanakuja kukupa limits za kuishi, kucontrol mind yako, your ability & skills, passion na wishes zako.
Am proud of myself being atheist.
Kwa comment hii fupi kuna mtu atapata kitu na kubadilisha maisha
Ni mtazamo wako mkuu ila kutokana na Imani ambayo imetengeneza huo mfumo tajwa hapo juu, mwanadamu kaumbwa ili aabudu(amtii M/Mungu)no more. huenda utakubali or not ila M/Mungu kaumba watu ili wamtekelezee kile anachotaka (ibada) na kama hutaki ndo pale wanaposema Moto utakuhusu. so ni Imani tu na sio lazima uamini pia sio lazima ukomenti.
 
haha unajilinganisha na kuku
Ukiwa na akili yako timamu utafahamu kuwa hauna uhuru wa kifikiria,
Unaishi kwa assumption na outdated literature.
Read books you will discover your value and even one minutes doesn't mean to be lost
Books gani mkuu unataka watu wasome, maana vitabu vya Mungu ndo vinasema hivyo au vya binadamu anaekwambia ulikuwa nyani.
 
haha una uhakika ni vya mungu?? umewahi kumuona mungu?? sembuse kusema vitabu vya mungu.
Acha kushikiwa akili na kuaminishwa uongo
Books gani mkuu unataka watu wasome
soma hiki hutokaa ujute kukisoma
 
Attachments

  • upload_2018-2-24_14-42-35.jpeg
    upload_2018-2-24_14-42-35.jpeg
    15.8 KB · Views: 59
haha una uhakika ni vya mungu?? umewahi kumuona mungu?? sembuse kusema vitabu vya mungu.
Acha kushikiwa akili na kuaminishwa uongo

soma hiki hutokaa ujute kukisoma
ina maana mkuu huamini uwepo wa mungu
 
Assalam wakuu

Nimependa niwaletee elimu toka kwa mtaalamu kama ifuatavyo

Utangulizi
Bismillah Rahman Rahim. Watu wengi bado wanajiuliza juu ya mfumo huu wa fedha wa kiislamu hususani uendeshaji wake kibiashara.

Mfumo wa fedha wa Kiislamu ni mfumo mtambuka wa uendeshaji na usimamizi wa fedha biashara na uchumi kwa kufuata (comply) sheria za dini ya Kiislam (Islamic shar’iah).
Sheria hizo za Kiislamu zimetokana na Qur’an tukufu na Hadithi za Mtume Muhammad (SAW).

Mfumo huu umejikita katika mambo makuu yafuatayo
i. Uendeshaji wa biashara za kawaida (trade)
ii. Taasisi za fedha (financial institutions) kama vile bima (takaful), benki na
iii. Taasisi zinazofanana nazo kama vile VICOBA.

Kwa uwezo wa Allah kitabu hiki kitajikita katika biashara tu, na toleo lijalo Insh’aalah litaendelea na Taasisi za Fedha.
Insh’allah mwandishi amejikita kutoa elimu kwa Waislamu na Wasio waislamu juu ya namna mfumo huu unavyofanya kazi.

Mwandishi ametumia lugha nyepesi ili kuendana na hadhira aliyoikusudia. Mwandishi anaamini wepesi wa lugha utakifanya kitabu kieleweke zaidi.

BIASHARA ZA KIISLAMU (ISLAMIC BUSINESS)
Ni biashara ambazo uendeshaji wake unaongozwa na kanuni na taratibu za dini ya kiislamu. Bidhaa zozote zilizoharamishwa katika Uislamu ni haramu pia katika mfumo huu. Hii haina maana kuwa sheria za nchi hazifuatwi la hasha.

Mfano Pombe ni haramu katika Uislamu hivyo biashara ya pombe pia ni haramu.
Allah S.W amehalalisha biashara kwa waja wake na kuharamisha ribah hii ina maana kuwa biashara ni kazi/shughuli halali kwa Waislamu lakini lazima ifanywe kulingana na mipaka ambayo Allah kaiweka (IKHLAS) sambamba na Serikali. Suratul Baqarah inafafanua hili katika aya zifuatazo:

276. Wale wanaokula riba, hawatasimama ila kama anavyosimama yule ambaye Shetani humpoozesha kwa kumshika. Hayo ni kwa sababu wamesema, Biashara ni kama riba tu; hali Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na kuiharimisha riba. Na aliyefikiwa na mauidha kutoka kwa Mola wake, kisha akajizuia, basi yake ni yale yaliyokwisha pita, na shauri yake ni kwa Mwenyezi Mungu. Lakini anayerejea (kula riba), basi hao ndio watu wa Motoni, humo watakaa.
​
277.Mwenyezi Mungu Hufuta riba na Hukuza sadaka, na Mwenyezi Mungu hampendi kila aliyethibitika kuwa kafiri na mtenda dhambi mkuu.

Na
TONYA. A. TONYA

ITAENDELEA (No pm kama una lolote mpigie mwenyewe)
Ni (copy & paste)
Namba yake?
 
Duniani kuna vitu ukivielewa unaondoka kwenye utumwa wa fikra.
Ogopa sana kushikiwa akili, umezaliwa na fresh mind yako watu wanakuja kukupa limits za kuishi, kucontrol mind yako, your ability & skills, passion na wishes zako.
Am proud of myself being atheist.
Kwa comment hii fupi kuna mtu atapata kitu na kubadilisha maisha
Mr.Kipago ushajinasibu kuwa huamini uwepo wa Mungu.Mbona ulijisumbua kusoma uzi wenye kichwa cha habari kinachoashiria uwepo wa Mungu?Bila shaka umekubaliana na dhana ya kwamba nafsi ya mtu haiwezi kutulia mpaka imtafute aliyeiumba .Hilo litakufanya upambane Sana kutafuta elimu ya Mungu,usibaki kwenye kusoma huh uzi jitahidi upate maandiko matakatifu kabisa ujiridhishe.
 
Back
Top Bottom