TAECOLTD
JF-Expert Member
- Mar 2, 2013
- 1,051
- 1,835
Wahenga walisema "Ukitaka kuchukua kipande cha dhahabu kiurahisi toka kwa kichaa basi mpe kioo, wakati akiwa anacheka na kioo wewe kusanya vipande vyako vya dhahabu na utokomee" Mwanamuziki Fid Q kati ya mashairi yake amewahi kusema "Tunatengeneza tabia kisha tabia zinatutengeneza sisi"..tunaweza tusione madhara ya kile tunachokipanda sasa hivi lakini madhara yake yakawa makubwa sana siku za usoni. Aina ya wanafunzi tunaowatengeneza ndio watakaokuja kusababisha kutengeneza taifa la mambumbu na taifa dhaifu.
Ni jambo jema kuona serikali ikifanya juhudi kuanzisha shule za kata lakini tujiulize kwanini shule hizi daima hushika mkia?
a) Hakuna waalimu wa kutosha
b) Hakuna madarasa ya kutosha
c) Hakuna maabara wala maktaba ya kujisomea
d) Miundombinu ya shule ni mibovu sana
e) Hakuna bajeti ya kutosheleza shule hizi
Unadhani ni kwanini shule binafsi zinafaulisha sana kuliko za serikali? Wao wamejikita kutatua matatizo yote hapo juu ambayo yameishinda serikali, kwanza utaweza vipi kulinganisha matokeo ya shule binafsi yenye wanafunzi 30 na ile shule ya serikali yenye wanafunzi 400 kama Azania? Wakati matokeo yanapotoka tunaanza kumtafuta mchawi ni nani na kujikuta waalimu wakuu wakisulubishwa kwa kosa ambalo hata haliwahusu, kwani mwalimu mkuu ndiye anayeajiri waalimu shuleni, yeye ndiye anayehusika na fedha kuwa ajiamulie nini cha kufanya katika shule yake? Hebu tuwe reasonable hakuna nchi yoyote iliyowahi kupiga hatua kwa kutengeneza wanafunzi hovyo. Nakumbuka miaka ile nasoma sikuwa najua kama mwanafunzi akifeli kidato cha nne anaweza kukimbilia chuo certificate bali nilishuhudia wengi wakirudia mitihani ili waweze kusonga mbele. Leo hii tunatengeneza wanavyuo legelege wa certificate, diploma na degree ambao kwa asilimia kubwa thinking capacity yao ni ndogo na haswa ndio hao wanakuwa mizigo kwa serikali kwenye suala la ajira.
Zamani wakati nasoma unakuta shule ya msingi ina wanafunzi 300 ila wanaochaguliwa sekondari hawazidi 10 hivyo inabidi upigane ili uweze kuwemo humo ila leo hii mwanafunzi ambaye anakuwa wa 250 hana hata wasiwasi maana anajua atapangiwa shule tu ya sekondari.
Siyapingi Maendeleo endelevu ila maendeleo yanayokuja na utatuzi wa changamoto zake ndio maendeleo ninayoyaongelea na sio maendeleo ambayo changamoto zinaziba hadi maendeleo yenyewe yasionekane. Tukianza kukosoa matokeo basi inaibuliwa muvi mpya ya kutusahaulisha na namna wananchi walivyo kama upepo likiibuliwa jambo tu nao haooo wameshasahau la awali mfano vitambulisho vya waalimu, nyumba za Dar kupakwa rangi, baa la njaa, wauza unga n.k
"Tukitaka kupiga hatua lazima tujitadhmini tunaweza kusimama kwa mguu mmoja wakati tukipiga hiyo hatua au la, kama hatuwezi basi tunahitaji magongo ya kutembelea"
Asanteni na niwatakie sabato njema!!
Mtenga Gerald
18/02/2017