Mfumo wa elimu ya msingi.

Nawaza kwamba mfumo wa Elimu ya msingi hapa Tanzania unashida.
Unahitaji marekebisho makubwa.

1. Naona kwamba ufumo huu una upungufu mkubwa katika matumizi ya Lugha.
Kuendelea kusisitiza matumizi makubwa ya Lugha ya KISWAHILI, naona ni kuwazuia wasomi wetu kuwa washindani wazuri kwenye viwango vya kimataifa.
Lugha ya Kiingereza ni pendekezo langu.

Bwana Exaud, ninakubali kabisa na. 2-4 kati ya mapendekezo yako. Sikubali kuhusu swali la Kiswahili kuwa kizuizi kwa wototo kwenye uwanja wa kimataifa.

A Kwanza kabisa mwanafunzi anayemaliza darasa la saba hatashindana kwenye ngazi ya kimataifa.
B Pili mtoto atajenga akili vizuri zaidi katika lugha yake au angalau katika lugha inayoeleweka kirahisi kwake - hii ni Kiswahili si Kiingereza.
C Mafundisho ya msingi kwa lugha ya kigeni yataacha wanafunzi wengi kubaki nyuma, ni wachache tu wanaoweza kusogea mbele.
D mifano mingi ya kimataifa yanaonyesha ya kwamba watoto wanaopata elimu ya msingi kwa lugha ya nyumbani hawana matatizo kujifunza lugha ya kigeni (kama Kiingereza, kifaransa, n.k.) wakifaulu kutumia Kiingereza kushinda wanafunzi Watanzania. Linganisha wanafunzi Wajerumani au Wasweden wa ngazi ya A-level jinsi wanavyojua Kiingereza na wanagunzi wa A-level wa Tanzania - ingawa wale Wajeumani au Wasweden wanajifunza masomo yao kwa lugha yao isipokuwa Kiingereza kama somo tu. Huko ni pia wengi wanaofaulu masomo mengine kushinda Watanzania.
E Je umeshawahi kutafakari ya kwamba matokeo mabaya ya hisabati katika Afrika ya Mashariki ni tokeo la Kiingereza kama lugha ya mafunzo kwa walimu wasiojua lugha ile ya kutosha? Ya kwamba hali ya kujifunza kwa lugha ya kigeni inakwamisha akili ya walimu na pia ya wanafunzi?
 
Wale wanaosema kwamba watoto wakijifunza kwa Kiswahili ndio wataelimika vizuri wanadanganya. Mbona watoto wengi wamepelekwa shule za Kiingereza na wameelimika vizuri kuliko hao waliosoma za Kiswahili? Ni kweli hizo za Kiingereza zina mazingira mazuri zaidi, lakini nasema kusoma kwa Kiingereza ni sehemu ya mazingira mazuri!

We need to learn basics in primary school. Huu uswahili wa elimu ya vitendo achaneni nao. Vitendo gani? Kwani shule za msingi ni VETA? Mtoto amalize darasa la saba akiwa amefahamu kusoma vizuri, kuandika, mahesabu, jiografia na historia. Si lazima ajue kazi za mikono. Kama itabidi, atajifunza kazi za mikono baada ya kidato cha nne.

You need quite a bit of education before you have enough for application. Hakuna mtoto anatakiwa aishie darasa la saba. Tuache kukumbatia umasikini wa watoto kumalizia darasa la saba. Mtu aliyemaliza darasa la saba tu ni ngumbaru bado.

Tuache vile vile kuwacheleweshea elimu watoto wa Tanzania. Waanze darasa la kwanza wakiwa na miaka 5, na sio 7. Na bora zaidi waanze shule za mwanzo (kindergarten) wakiwa na miaka 4. Inawezekana, na wazazi wengi waliofuta ujinga hawangoji mpaka watoto wao wafike maiak 7 kabla ya kuwaanzisha shule.

Tatizo kubwa kuliko yote katika Elimu Tanzania ni udanganyifu serikalini. Nani anahakikisha serikali inatumuia fedha zilizotengewa Elimu kwa shughuli hiyo? Mwaka huu wa fedha unaomalizika, ELIMU ilitengewa bajeti ya shilingi trilioni 1.2. Niwaonavyo hawa watawala wetu, hawatatumia hata bilioni 700 kwenye Elimu. Watazihamishia kwenye shughuli za uchaguzi, na nyingine wataziiba tu, kimya kimya! Wamefanya hivyo kila mwaka!
 
Last edited:
Wale wanaosema kwamba watoto wakijifunza kwa Kiswahili ndio wataelimika vizuri wanadanganya. Mbona watoto wengi wamepelekwa shule za Kiingereza na wameelimika vizuri kuliko hao waliosoma za Kiswahili? Ni kweli hizo za Kiingereza zina mazingira mazuri zaidi, lakini nasema kusoma kwa Kiingereza ni sehemu ya mazingira mazuri!

MOSHI,
Mawazo yako yalenga huko tunakoelekea sasa.
Na wengine wanatamani sana watoto wao wapate Elimu kwa kiingereza ila garama inakuwa kikwazo.
Uliousema ndo ukweli wa sasa.

Naamini KIPALA na OFFISH wakiwa na hoja zaidi, wataweza kuziweka wazi.
 
Bw. Exaud na Moshi,
ni kweli mkisema ya kwamba watafunzi wa shule za Kiingereza nchini TZ wanamaliza vizuri kulingana na watoto wa shule za kawaida.
Lakini sababu yake si lugha. Kitaalamu jambo limeeleweka kabisa. Ni chaguo cha wanafunzi na mazingira yao kwa njia ya karo kubwa zaidi. Shule za Kiingereza zina gharama kubwa zaidi sivyo?
Kwa hiyo shule hizi zina
a) uwezo mkubwa zaidi wa kifedha kwa hiyo nafasi nzuri zaidi na mazingira bora kwa kazi ya walimu pia wanafunzi
b) kwa wastani mishahara ya walimu inaelekea kuwa vizuri zaidi (na kama ni tu kutokosa/kutochelewa mishahara )
c) chaguo bora zaidi ya wanafunzi; familia nyingi zinazowafundisha watoto wao ya kwamba elimu ni muhimu wakitoa karo kubwa kuliko kawaida;

(Mkipendelea Kiingereza: Social selection of students is a well established explanation for performance)

Kwa hiyo si Kiingereza: ukiwa na hizi a) b) c) shule itaona matokeo bora hata ukitumia Kiarabu, Kilatini au Kituruki kama lugha ya mafundisho (hata Kimasai kama vitabu vingekuwepo).
 
Exaud na Moshi,
Kwa hiyo si Kiingereza: ukiwa na hizi a) b) c) shule itaona matokeo bora hata ukitumia Kiarabu, Kilatini au Kituruki kama lugha ya mafundisho (hata Kimasai kama vitabu vingekuwepo).

KIPALA,
Mawazo yako ni mazuri kwa watetezi wa kiswahili.

Mawazo yangu na hata Bwana Moshi, si kwamba hatukipendi kiswahili ila tunaangalia hali halisi ya Dunia inakoelekea.

Siku hizi hata ukinunua Paketi ya CHUMVI, au Kiberiti, au hata pipi, vyote vina maelezo ya kiingereza. Alama za barabarani karibu zote ni kiingereza, n.k.

Ndiyo maana umuhimu wa kuwaelimisha watoto wetu kwa Lugha ya kiingereza unazidi kuwa wa maana.
 
00e1020f60e991ca.jpg


Inaonekana kuwa wamegoma kuuza aisikirimu za mwalimu.
 
2884531998_ec4608f8e5.jpg


Primary school kids, Tanzania, 1964

Hii picha ni ya mwaka 1964, utaona kuwa kulikuwa na majengo bora kulikohivi sasa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom